Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,047
- 79,390
MBUNGWA: NGOMA YA MASHETANI NA WENYE MAPEPO. KULA CHUMA HICHO.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Narudisha miaka yangu nyuma kidogo. Kumbukumbu zinanichukua na kunipeleka kwa kasi kisha zinapunguza mwendo kwa kasi, polepole naanza kuyaona matukio ya mwaka mpaka mwaka kuanzia miaka ya 1995 mpaka 2005. Kama Sinema ya kihistoria iliyobeba matukio yenye visa vya ajabu na kushangaza, na baadhi yenye kutisha. Macho yangu yanashuhudia sio kama shuhuda bali kama miongoni mwao wahusika matukio yanayoupa moyo wangu majonzi.
Sivutiwi na matukio ya UKIMWI ugonjwa mbaya na hatari sana ambao watoto wa 2000 watanibishia na wala hawauogopi kwani hawakuwahi kushuhudia balaa lake. Miaka ya 1998-2005 UKIMWI uliumiza, kutesa, kudhalilisha, kunyanyasa na kuua watu kikatili na kibabe sana.
Nazipuuza kumbukumbu za matukio hayo na sasa napitishwa karibu na mwaka 2001 kuelekea 2003.
Sasa hii ni sinema inayonivutia na ambayo ningependa kuisimulia. Sikutegemea kama bado ningekuwa na faili la kumbukumbu za tukio hili;
Usiku wenye mbalamwezi katika Kijiji cha Makanya, Same, Mkoa Kilimanjaro katika nchi ya Tanzania.
Upepo wenye husda uliendelea kuvuma pasipo kizuizi kama ilivyoada. Upepo huu ulikuwa kero kwa wageni waliofika katika kijiji 'chetu wakati sisi wenyeji tukiwa tumeuzoea na hatukuwa na habari nao. Kiini cha upepo huu ni tabia ya nchi ya eneo la Makanya ambayo ni Nusu jangwa, walisoma wanaita Semi Arid Desert. Hali inayofanya nyakati za usiku kuwa na hali ya hewa isiyo rafiki, ubaridi na upepo mkali ambao kuna misimu huchanganyika na vumbi na kufanya eneo hili kuwa kama kanda maalum ya kuzimu.
Anga likiwa tupu! Naam uchi kabisa likionyesha maungo yake ya siri na fahari yake; nyota na Mbalamwezi vikiwa vimetanda kotekote. Mwezi ukiwa Duara ukimulika kwa shani ya kipekee, huku mapaa ya nyumba, miti na ardhi ya wakazi wa kijiji vikiwa vimejawa na hofu, mashaka na kitisho.
Naam kitisho! Cha Ngoma! Mbungwa! Ngoma ya mashetani na watu wenye mapepo ambayo ilikuwa ikiendelea kurindima katika anga la Makanya na kufanya mji mzima uzizime kwa hofu.
Pengine uliwahi kuona ngoma za ina nyingi sana. Hata mimi nimewahi kuziona.
Nimeshahuhudia Sindimba ikichezwa na Wamakonde asilia. Nyakati zile nilipopita maeneo ya Mtwara nilipoenda kwa mambo yangu ya biashara ya korosho. Ile ngoma watu wanacheza nyie. Wanawake wanaweza nyie. Hasa mwanamke halisi wa Kimakonde.
Sitaki nikuhadithie habari ya ngoma ya Madogoli. Unaijua hiyo. Mtafute Mngoni kutokea Songea huko atakueleza ikoje.
Najua ngoma ziko nyingi sana.
Lakini kwa habari za ngoma zilizoniacha mdomo wazi, huku moyo wangu ukiwa umehamanika ni ngoma Mbili tuu. MBUNGWA, na ya pili ni Ngoma ya Lugwadu. Dadadeki! Huko sio pouwa.
Kama haujawahi kuzishuhudia basi unaweza kuzitafuta bahati nzuri zinachezwa kwa usiri mkubwa siku hizi na usiku ukiwa mnene. Kwa watu maalum.
Basi!
Mimi na watoto wenzangu kipindi hicho niko shule ya msingi. Tukiwa kama sita hivi tulikuwa nyuma ya Ua wa malingoti. Kwa wasiojua malingoti ni miti inayotokana na Katani. Sasa kule Maeneo ya Same na Mwanga na hata Tanga tunatumia miti hiyo(milingoti) kujengea Uzio(ua wa nyumba).
Basi tukiwa kwenye Uzio wa malingoti nje ya Ukumbi katika nyumba ya Mama mmoja maarufu, nitaweka jina bandia, kwani watoto na wajukuu zake wapo ingawaje yeye sasa ni marehemu. Tumuite Zakia Rangisaba.
Huyu Mama Zakia Rangisaba alikuwa mashuhuri mwenye kuogopwa na kuogopeka kutokana na sifa zake za kichawi, kiganga na kishetani.
Yeye ndiye alikuwa Tuseme Kuhani katika kuhakikisha Mashetani na wenye mapepo wakija pale kwake sherehe ya ngoma ya Mbungwa inafanikiwa kwa kiwango kikubwa sana.
Alikuwa Mama mwenye ubin wa kisukuma, Mrefu, mwenye rangi ya kahawia labda ile Robusta inayoenda kuwa nyeusi. Mwenye umri wa Makamo kama miaka hamsini kwa kipindi kile.
Uso wake ulikuwa mkali, wenye macho yenye maarifa mengi ya kiganga na kichawi, lakini asiye na dalili ya huruma.
Nyusi za macho yake zilikuwa zinamchangiko wa mvi na weusi ambazo ziliongeza nafasi katika utisho wa wajihi wake.
Zakia Rangimoto hakuwa Mwongeaji sana lakini aliheshimika hata kila kivuli chake kilipokuwa kimefika. Alikuwa na ushawishi bila kushawishi watu. Walimwogopa na sio wao tuu hata mimi nilijifunza kumwogopa baada ya tukio nililoliona katika usiku ule wa Mbungwa. Ngoma za mashetani na wenye mapepo.
Wengine walimuita Mganga, wengine mchawi, wengine walimuita Kiboko ya Majini, wengine walimuita Maji Marefu.
Mimi nilikuwa mdogo sikujua nimuite nani isipokuwa Mama Zakia Rangimoto.
Nyuma ya Uzio wa malingoti tumejificha kwa sababu haturuhusiwi kuona mambo hayo na wenye ngoma yao. Lakini pia hata wazazi na walezi wetu walikuwa wakitukataza kufika maeneo hayo wakati ngoma hiyo ikipigwa.
Hivyo tulikuwa pale kimagendo, kwa siri kutazama mambo ya siri .
Nikiwa nyuma ya Uzio wa malingoti na wenzangu, nikaona watu wakija na kuingia katika ukumbi ule. Wengi wao wakiwa wamevaa Kaniki nyeusi na wamejifunika vichwa vyao na vilemba vyekundu.
Wengine walikuwa wamevaa hijabu na majuba gubigubi wala usingewatambua.
Nikawaona wengine wakiwa wamevaa vinyago vya wanyama kama paka, nyoka, na mafuvu.
Uvaaji wa wengi ulikuwa wa kujificha wasionekana ni kama walijua kuna watu watakuja kutazama hata kwa siri. Na baadhi ya watu hao mimi nilikuwa mmojawapo.
Wachache sana waliacha sura zao waziwazi na tuliziona. Mmoja wapo ni hiyo Zakia Rangisaba na wengine wawili ambao walikuwa maarufu na wenye majina ya ajabu na vitendo vya kutisha vya kichawi.
Sitawataja kwa majina yao halisi lakini ili kuwapa utambulisho hapa kwenye simulizi itabidi niwape majina bandia yanayoendana na majina yao halisi.
Wakwanza aliitwa Kausimba Kambaulaya, huyu ni mwanaume, mzee wa makamu.
Wapili aliitwa Sharifa wa Bombo, huyu ni Mzigua kutokea Tanga huko. Hatari sana.
Wapiga ngoma wao walikuwa wapo vifua wazi lakini chini wamevaa sketi za rangi nyeusi. Kichwani wamefunga vitambaa vyekundu na kuchomeka manyoya ya ndege, sikujua ni kuku au kanga, au ndege gani lakini yalikuwa Manyoya marefu sana. Kichwa kizima. Walikuwa wapiga ngoma watatu. Na mmoja alikuwa anapiga chekeche. Mwingine akawa anapiga kitu mfano wa kinubi hivi.
Ubaridi bado ulikuwa ukitupiga huku mbalamwezi likimulika.
Ilipotimu saa sita na madakika, watu wakiwa wamejaa na ni kana kwamba wamekoma waliokuwa wakija.
Zikachinjwa kuku saba hivi zikiachwa zikimbiekimbie bila vichwa. Basi wale watu wakawa wanapiga vigelegele na vifijo jinsi wale kuku walivyokuwa wanapaparika. Kumbe kuku atakapoangukia kwa mtu basi mtu yule anamkamata kuku yule na kuanza kunyonya damu shingoni. Mmmh! Tukio hilo liliongeza hofu yangu na wenzangu. Haikuwa kawaida mtu kunyonya shingo ya Kuku ikiwa ni damu mbichi kabisa
Kisha walipomaliza tukio hilo. Wale watu saba walioangukiwa na wale kuku saba waliokatwa vichwa, wakasogelewa na Zakia Rangisaba. Ambaye alikuwa amebeba usinga mkononi wa kuume, wakati tunguli ndogo yenye ushanga ikiwa mkono wa kushoto. Akachukua ule usinga na kuuchomeka kwenye mdomo wa tunguli kisha akawa anaongea kwa maneno ya kiajabu ambayo sio lugha ya kibinadamu. Alafu akawachapa na ule usinga usoni mwao wakawa wanatetemeka kama wamepandisha maruhani(mapepo) kisha wanadondoka hovyohovyo na kujirusha rusha hovyohovyo na kujibamiza bamiza chini.
Kisha Zakia Rangisaba akaanza kuimba. Nakumbuka sehemu ya maneno yake machache yaliyokuwa yanajirudia rudia kama sijui ni kibwagizo au korasi sijui;
Akaanza kuimba polepole huku na waitikiaji wakiitikia polepole;
"kanga"
Waitikiaji wanajibu "anamadoa meupe"
"kanga"
Waitikiaji " anamadoa meupe"
Hivyo hivyo huku akipandisha sauti na waitikiaji nao wakawa wanafuatisha kupandisha sauti.
Akishusha nao wanashusha.
Kisha ngafla kinaletwa chungu kikawekwa katikati ya uwanja wakiwa wamekizunguka.
Zakia Rangisaba akachapa kwenye mdomo wa chungu na ule usinga wake palepale moshi ukaanza kutoka katika mdomo wa kile chungu na hapohapo wapiga ngoma wakaanza kuzipiga ngoma zao polepole kwa kufuata mapigo ya wimbo wa Kanga .... Anamadoa meupe.
Ngoma polepole
Wale watu ambao nilisema wengi wao wamejifunika nyuso zao kwa namna ya kujificha ili wasitambulike na wengine wakiwa wamevaa vinyago na barakoa wakaanza kutingishika lolepole. Polepole kwa kufuata ngoma. Polepole wakiimba.
Kisha wakaanza kuzunguka kama duara lakini wakitembea polepole wakifuata mdundo wa ngoma. Muda huo Zakia Rangisaba alikuwa akiongea kwa kasi maneno usiyoyajua wala tusiyoyajua huku Sharifa wa Bombo akimsaidia kuimba kile kipande cha Kanga... Na wengine wakiitikia anamadoa meupe.
Zakia Rangimoto akawa anaongea mpaka ikafikia macho yanaangakia juu kama mtu anayekataa roho na jicho linakuwa jeupe pee bila Retina wala ile rangi ya kahawia kuonekana.
Alitisha kama nini.
Muda huo ngoma nayo ikawa inazidi kuchanganya walichanganya ngoma za kisambaa na madogoli ya kingoni.
Kadiri ngoma ilivyokazana kupigana ndivyo watu walivyozidi kupagawa na mapema. Walipagawa na kuanguka hovyohovyo lakini wakicheza katika kuanguka kwao pasipo kupoteza mdundo wa ngoma.
Kuna ambao walikuwa wanaanguka kama wamezimia wakawa wanawamwagia ndoo ya maji pwaaa!
Kisha Zakia rangisaba naye akawa anacheza akizunguka kile chungu huku akiimba kama mwehu kisha kwa ajabu ya maajabu moshi ukiwa mkubwa Zakia Rangisaba anaingia ndani ya chungu na alipoingia anapotelea humo chunguni na moto mkubwa unalipuka kwenye ule mdomo wa chungu. Hali inayoifanya eneo lote nuru kuongezeka na wale wanawake waliovaa Kaniki wakiwa wameficha sura zao kupiga makelele ya kishetani na sasa haikuwa ngoma tena bali ilikuwa ni zaidi ya ngoma.
Wapiga ngoma wanachachamaa kuzipiga ngoma. Wenye mapepo wanazidi kupagawa na sasa mzee Kambaulaya anaingia ndani ya nyumba na kutoka na kuku anawatupa uwanjani watu wanaanza kukimbizana kama wamepagawa wakikimbiza kuku. Ngoma inaendelea lakini imebadilika midundo yake na filimbi sijui kinubu na chekeche inapigwa, watu wanakimbizana kunyang'anyana yule wale kuku na wanawanyima damu wazima wazima. Kelele za kuku hazifui dafu mbele ya kelele za ngoma na mayowe ya wenye mapepo.
Mzee Kambaulaya anarusha kuku wengine. Mchezo ni uleule kukimbiza kuku na kunyang'anyana huku wakiwa ng'ara shingo na kunyonya damu zao.
Kipande hicho kilinisisimua na ninakikumbuka mpaka kesho.
Ghafla bin Vuu wale wenye mapepo wakiwa na hekaheka pakiwa vumbi linatimuka, Zakia rangisaba anatokea kwenye chungu kama upepo wa kisulisuli. Alafu ukimtazama ni kama unaona maruerue au unahisi upo kwenye ndoto au kama unapoteza fahamu au kupatwa na usingizi.
Ngoma inaendelea, mara kwa ajabu mmoja wa wanawake anachomoka akipiga makelele ya kipepo anakimbia mlangoni, nyuma yake anafuatwa na mapaka watatu. Moja likiwa jeusi tii, lapili likiwa jeupe pee, la tatu liliwa jeusi kenye baka jeupe kwenye baja na baka jeupe usoni. Yote yalikuwa mapaka wakubwa yale yenye mashavu manene.
Sisi kuona yule mwanamke amekimbia na anafuatwa na yale mapaka tukajua anakuja kule nyuma ya uzio wa Malingoti, nje tulipokuwa timejificha. Tukatoka nduki kila mmoja akijihami na kujinusuru asijekutwa na hatari za tukio lile.
Tulikimbia kila mtu akichukua njia yake..
Nini kiliendelea, kwa kweli stori imeishia hapo. Hiyo ni Mbungwa, ngoma ya mashetani na wenye mapepo.
Kwenu ngoma hizo zinaitwaje?
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam