Mbunge Zambi ashitakiwa mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Zambi ashitakiwa mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dm2000inter, Jun 15, 2012.

 1. d

  dm2000inter Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Mbunge wa CCM Jimbo la Mbozi Mashariki, Mheshimiwa Godfrey Weston Zambi Jumatano wiki hii mjini Moshi amefunguliwa kesi ya madai na kampuni ya Lima Limited akidaiwa fidia ya shilingi 2.4 bilioni kwa tuhuma za kutoa matamshi ya kuikashifu kampuni hiyo.

  Katika gazeti la Mwanahalisi la Juni 13-19,2012, Mheshimiwa Zambi anadaiwa kutamka" Lima imekuwa ikiwashawishi wakulima kuuza kahawa mbivu kwa bei ndogo sana".

  Kampuni hiyo inamtuhumu Zambi kuanzisha kampeni mbaya dhidi ya kampuni hiyo ili kuondoa ushindani wa soko ili kuvipa fursa vikundi vya wakulima ambavyo Zambi ana maslahi navyo visipate ushindani wowote katika soko la Kahawa. K

  esi hiyo namba CC 7/2012 imefunguliwa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi,Eric Ng'maryo ambaye pia ni Advocate Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa.
   
 2. M

  Mzee wa fund JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 520
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mfamaji huyo.mwache atapetape.
   
 3. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Mbona sioni tatizo la hiyo kauli, kama kweli wanafanya haki na siyo dhuluma kwa nini waogope? hapo lazima kuna ulaghai wanafanya na hivyo wameona wameumbuliwa.

  Halafu siku hizi bana Tanzania hizi kesi za kupuuzi zimezidi eti kesi 2.4 bill, yaani mtu anajitamkia tu kiasi cha fedha anachotaka. Hii laana imetoka wapi? Lengo nini kama siyo kutaka kuwanyamazisha watu wasikemee maovu kwa kuogopa kesi za billions?

  Ee Mungu iokowe nchi yangu niipendayo ya Tanzania, na mikono ya wanyanganyi hawa wasio hata na huruma wala haya.
   
 4. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ukisoma ile makala ya Mwanahalisi between line juu ya mtazamo wa Zambi utaona wazi kuwa Zambi yupo sahihi zaidi ya 100% hata kama huyu Eric anataka kutumia mahakama kumziba mdomo.Board ya kahawa wajumbe wake JK na Waziri wake wa Kilimo wamechemka kwenye uteuzi wa Board Members.Total Conflicts of interest between board members.
   
 5. S

  Sakane Member

  #5
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tatizo ni Zambi ama alieteua Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi, halafu tatizo lipo wapi kwakuwa sasa ni soko huria
   
 6. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mkuu Kanga, sakata la Zambi na kampuni ya Lima ni la mbunge Zambi kuwa na fikra za ki-ccm yaani kuwanyonya wanyonge kwa mrija usio na huruma. Hapa Mbozi kampuni la Lima linalipa bei nzuri kuliko vikundi vya wajanja wa kiswahili, lakini kwa mashart ya kuiboresha kahawa katika vinu vyao vinavyo process kahawa mbivu. Mwanya huu unampa jeuri Zambi kutengeneza uongo mwingi dhidi ya Lima. Kiujumla wakulima wa kahawa Mbozi wanapenda kuuza kahawa yao kwa Lima, lakini Zambi kutumia ubunge wake anataka kuidhinisha wakulima wawe wananyonywa.
   
 7. Walikughu

  Walikughu Senior Member

  #7
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi Sija soma hilo Gazeti lakini ukweli ni kwamba Kampuni ya Lima Kuendelea kununua kahawa Mbichi Yaani "Cherry" huu ni wizi, kwa sababu wananunua kwa Bei ndogo sana alafu hawana mpango wowote wa kufufua zao la kahawa zaidi ya kuwaibia wana mbozi Mimi naungana na Mh. Zambi katika hili la kuwapiga vita walanguzi wa zao la kahawa katika Wilaya yetu ya Mbozi Na kwingineko.
   
 8. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,054
  Likes Received: 1,440
  Trophy Points: 280
  Imperialism....The Highest stage of Capitalism! Ng'maryo, Zambi wote sawa!
   
 9. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mkuu, tatizo ni mbunge Zambi anataka kuwafadhili wanunuzi wa kizalendo ambao hawana uzalendo wanotaka kuwapunja wakulima kwa kuwapa bei ndogo. Isitoshe jamaa hawa ndiyo walio kuwa ma-cmpainer wa Zambi wakati wa uchaguzi wa ubunge, lakini kura hazikutosha ilibidi wachachue kumpa ubunge Zambi.
   
 10. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watu wanataka maendeleo ya nchi wengine wameona mahakamani ni sehemu inayofaa. Then mtasema Mungu anawalaani au mmejitakia wenyewe?

  Tushachoka na propaganda za uswazi kama hizi.
   
 11. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mkuu usitutukane watu wa Mbozi kana kwamba sisi tutachagua kumwuzia kahawa yetu Lima anayetupunja. Wewe na Zambi wako tuacheni soko lituamlie wapi tuuze kahawa yetu kuliko kutulazimisha tuwauzie waswahili wanaochukua kahawa yetu kwa kutukopa kutulipa inakuwa taabu.
   
 12. Walikughu

  Walikughu Senior Member

  #12
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi sijawatukana ila wewe ndiye unaye taka matusi, Ngoja nikupe shule kidogo kahawa ya cherry unauza kwa lima kiasi cha sh.200 kwa kilo ambayo ukichukua kilo 5 za cherry ni sawa na kilo 1 ya kahawa kavu yani Parchments, hapo either mnakuwa mmeshaachana na lima kwa sh.1000 tu.

  Ambayo unakuwa umelipwa yeye akienda kuuza sokoni wastani wa kili moja tena parchment ni sawa na $ 3.5 kwa kilo hilo ni soko la Moshi bado hajachakachua ule mtindo wa kujinnulia kahawa yake na kuipeleka nje ya nchi, cha msingi ni kuwa hata kama soko unataka liwe forced na demand and supply lazima kuwa na sheria ambazo zitasimamiwa na serikali maana yake ni kwamba ukiwaacha hawa wafanyabiashara peke yao watakaa na kupanga bei.

  Mwisho wa siku atakaye umia ni Mkulima, kuhusu hivyo vikundi vya kahawa ni sawa baadhi ni kero lakini vingine vinafanya vizuri na naomba usije ukasema mimi na Mh. Zambi tunakula pamoja kama unavyo taka kujipambanua hapo kuna wizi labda wewe binafsi kuwe na maslahi unayoyapata kupitia lima maana tunawafahamu sana kwa uchakachuaji wenu wa kahawa kwa kumwibia mkulima.
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nimesoma articles mbili kuhusiana na hii saga. Mwanahilisi na Mwananchi. Yangu mimi ni maswali mawili tu:

  1. Kwa nini Lima wananunua kahawa mbichi (cherry)?

  2. Uteuzi wa Board unazingatia nini?
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Wacha mahakama itatupatia majibu
   
 15. Walikughu

  Walikughu Senior Member

  #15
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ananunua kahawa mbichi ili ajifaidishe, ananunua kwa bei ndogo na kisha kuiuza kwa bei kubwa.

  Kuhusu Uteuzi wa Board Nadhani kuna vigezo ambavyo vimewekwa na wizara ya kilimo ili kuwapata hao wakurungezi bodi ya kahawa na hizo nafasi hasa mkurungenzi mtendaji huwa inatangazwa na wenye sifa wanaomba.
   
 16. m

  matengo Member

  #16
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatua iliyochukuliwa na Lima naipongeza ili iwe fundisho kwa yeyote atakayetumika kwa kulipwa vijisenti au kupigania wadhamini wake wa uchaguzi. Mheshimiwa Zambi amejidhihirisha wazi kuwa ana maslahi binafsi tena pengine huu ni ushahidi wa maneno ya mh. Kafulila mbunge wa Kasulu kuwa anapenda rushwa(Soma Mwanahalisi ya tarehe 13/06/2012).

  Biashara ya kahawa mbichi inafanyika Tanzania nzima na hakuna mgogoro, hata Mbozi biashara hiyo imekuwa ikifanyika tangu mwaka 2006 na hatukuwahi kumsikia Mh. Zambi akilalamika. Matatizo yalianza mwaka 2008 baada ya kuingia Mkurugenzi Mkuu mpya wa Bodi ya kahwa Bw. A. Kumburu. Huyu mkurugenzi ndiye aliyefuta leseni za Red Cherry kwa maagizo toka maboss wake wa zamani Technoserve(Bado ni maboss wake wa siri). Alifanya hivi kinyume cha taratibu kwa vile maamuzi ya kuruhusu kuwepo leseni ya Red Cherry yalitoka baada ya vikao kati ya Wizara mbili za kilimo na uwekezaji pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri Mbozi na Bodi ya Kahawa. Hivyo ili kufuta leseni ilibidi apate kwanza kibali cha waziri mwenye dhamana.

  Baadae yakaendelea malalamiko toka kampuni ya Lima kwani waliwekeza kwa mwaliko wa serikali ili kuboresha zao la kahawa lipate bei nzuri katika soko la dunia. Serikali iliona kuna sababu za msingi wakaruhusu leseni itolewe.

  Kuhusu kuandaa kanuni mpya uliandaliwa mchakato wa kuhusisha wadau ambapo mwezi wa sita 2011 kilifanyika kikao cha baadhi ya wadau chini ya uenyekiyti wa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya kahawa. Kikao hiki kilipitisha leseni ya kununua kahawa mbivu itolewe. Mwenyekiti alikubali kwa vile wajumbe walimzidi tena kibaya zaidi katika kikao hicho mabosi wake wa kwenye mabano wakishuhudia na mh. Zambi naye pia alikuwapo.

  Baada ya njama za Bw. Kumburu kugonga mwanga ndipo akaanza mkakati wa kuwatumia akina Mh. Zambi ambaye kwenye hicho kikao wala hakuonekana kupinga biashara ya Red Cherry. Hatujui alimshawishi kwa njia hipi labda ni pamoja na kutumia njia alizotaja mh. Kafulila. Bw. Kumburu kinyume cha maamuzi ya wadau aliandika barua wizarani kupinga biashara ya Red Cherry.

  Sasa baada ya kuona Waziri wa Kilimo amejua ukweli na kuruhusu leseni ndipo mh. Zambi akaendesha kampeini aondolewe wizara ya Kilimo na hasa akitegemea atamwokoa Kumburu ambaye anaendesha Bodi ya Kahawa bila ya kufuata sheria. Waziri alipobadilishwa akategemea sasa Bodi mpya itakuwa kama bodi ya zamani imfumbie macho Adolf Kumburu kinyume chake Bodi mpya ikaonyesha ina nia ya kumaliza matatizo ndani ya sekta ndogo ya kahawa.

  Mkutano mkuu wa wadau wa kahawa Morogoro uliazimia itolewe lesni ya kununua kahawa mbivu ili mkulima mwenyewe ndiye aamue kama auze au aache. Huu pia ndio ulikuwa msimamo wa waziri mkuu alipoenda Mbeya.

  Sasa unyonyaji anaosema Mh. Zambi uko wapi? Au anataka kusema Lima itakuwa inashika bunduki kuwalazimisha wakulima wapeleke kahawa kwenye vinu vyao. Kama Zambi anaona kuuza kahawa mbivu ni kuwanyonya wakulima kwa nini asifanye kazi kuwaelimisha wasimuuzie Lima ili Lima ikiona inakosa kahawa iache biashara hiyo yenyewe.

  Mh. Zambi anajua akifanya hivyo kwa kuwaahidi wakulima bei ya juu mwisho wake watakapouza wakakuta bei imeporomoka watamuua hivyo hawezi kufanya hilo.

  Mwenyekiti wa Bodi yuko sahihi kwa kutamka kuwa mwenye uhuru wa kuchagua ni mkulima. Jukumu la kumwelimisha mwenendo wa soko ili mkulima afanye maamuzi sahihi ndilo linatakiwa kutekelezwa na serikali na wala siyo kuzuia baadhi ya masoko.

  Sasa Mh. Zambi aliyeenda Morogoro na wenzake kuhakikisha wanalazimisha kuzuia biashara ya kahawa mbivu ambayo yeye anaipinga Mbozi ili izuiliwe nchi nzima( Kwingine kote inafanyika) kugonga mwamba akaja na ajenda mpya ya kumpinga mwenyekiti mpya wa Bodi na wajumbe wake.

  Swali la kujiuliza alipata je ubunge mtu asiyekubali maoni ya wengi. Au anaogopa kutema pesa alizoahidiwa na wafidhili wake akiwemo Adolph ambaye anamtumia ili Bodi yote ingolewe yeye aendelee kuedesha shirika la umma kama mali yake.

  Huku ni kujidanganya kwa vile matatizo ya Kumburu hayawezi kuisha kwa kufukuza viongozi wake, kinyume chake matatizo ndani ya sekta ya kahawa yanaweza kuisha kama Kumburu chanzo ch
   
 17. B

  Belik Member

  #17
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naomba kusema kuwa naenda kutafuta data halisia ila haya yote yanasababishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Bw Adolph Kumburu akiwasaidia wazungu kummaliza mkulima waziri wa kilimo chukua hatua haraka
   
 18. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,793
  Likes Received: 3,880
  Trophy Points: 280
  Wangekuwa wameogopa wasingefungua kesi! mahamani ndipo mahali sahihi pa kupata ukweli , utakuwa au huelewi katiba au unaidharau unaposema kesi za kipuuzi! kikatiba kila mtu anapohisi hajatendewa haki mahali pa kuipata haki hiyo ni mahakamani! Kama Zambi au hiyo kampuni ipo sahihi ni kazi ya mahakama kutafsiri na kama fidia iliyoombwa ni sahihi au sio pia ni wajibu wa mahakama kutafsiri! Inaonekana una maslahi binafsi na hii kesi ndio maana umeanza ku rule out kabla hata hearing haijaanza!!
   
 19. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ngoja tusubiri tuone nani mkweli mahakama tendeni haki
   
 20. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Wakulimaaaaaaa, mnalima mkishavuna mnamuachia mnunuzi awapangie bei ya mazao yenu!!!! ndiyo maana ujinga umefungamanishwa nanyi.
   
Loading...