Mbunge wetu Prosper Mbena, nawe ni mbunge UKAWA?

Mbunge wetu Prosper Mbena, nawe ni mbunge UKAWA?

Jaji naongea jambo ninalolifahamu wala si kumtetea mtu.
Pili sipo Dar kama unavyosema na nafuatilia kwa karibu jinsi anavyojitahidi kisaidia wananchi.

Tatu mimi sio manaccm wala hata mfuasi kama unavyodhani.

Hapa ninapoandika mimi nipo mtamba kata ya kisemu tarafa ya matombo, haya niambie wewe mwenzangu upo wapi nije unioneshe walau mawili matatu ambayo huyu mbunge kayafanya toka aingie madarakani. We sema tu hata kama upo kibungo juu mimi nitakuja sababu nina boxer
 
Huyu mzee ni jembe la ukweli nyie acheni majungu. Hamjamjua tu vizuri. Fuatilieni kwa makini mpaka sasa amefanya mangapi mazuri kwa wananchi wake tena tangible things.
Taja hivyo vitu alivyovifanya, inaonyesha hata wewe huvijui unataka kudanganya watu hapa. vItu vingi vitu vingi wapi?
 
Huyu Mbena ni kati ya watu walioomba ubunge ili wawe mawaziri , mwingine ni adadi rajabu , mbena aliomba ubunge akiwa na ajenda hiyo tu , huyu alishafanya kazi ikulu miaka kadhaa , amewahi kusaidia nini kwenu ? Mliamua kujipendekeza sasa subirini mkomeshwe .

Yani tumeingia choo cha kilema, mguu ndala mkono ndala
 
Tawa, ebu niambie kwa mfano unataka afanye nini uone anafanya kazi zake vzr.

Wewe unaona kabisa hali ya barabara yetu jinsi ilivyo bajeti ya wizara ya ujenzi imepita hata kuchangia ili kuikumbusha serikali hakuna. Majumba yamewekwa X kwa tulivyowajinga tayari tumeridhika tunajua barabara inakuja.
Sina hakika na elimu yako, lakini kuna kitu kinaitwa advanced level schools, jimbo zima hakuna hata moja alafu unaniuliza unataka afanye nini.
Sikia bro, kama wewe una manufaa naye sisi anatuchosha huyu mzee
 
kuna watu wnakula kwa mbunge kwa hiyo hata kumsema mitandaoni wanaona tabu
 
Salamu wana jamvi,

Habari inayochukua nafasi ya juu ndani ya bunge kwa sasa ni mgogoro uliopo kati ya wabunge wanaounda umoja wa UKAWA dhidi ya naibu spika wa bunge dr. Tulia Ackson, jambo linalopelekea wabunge hao kutoka nje kila bunge lioongozwa na naibu spika huyo

Tabu yangu kubwa ni kwa mbunge wangu. Mbunge aliyepewa ridhaa na wananchi wa jimbo la Morogoro kusini kuwawakilisha bungeni. Mbunge huyu amebeba agenda nyingi za sisi wananchi wake.

1. Tuna matatizo ya barabara inayounganisha wilaya ya morogoro vijijini na manispaa ya morogoro. Barabara hii ni ya vumbi yoka mkoloni mpaka ninapoandika habari hii.

2. Huduma za elimu ni duni sana katika jimbo hili. Hakuna hata shule moja ya sekondari ya juu(advance level).

3. Wanayoiita hospital ya wilaya katika jimbo hili ni sawa na kituo cha afya cha tandale kwa mtogole pale wilaya ya kinondoni.

Kinachonishangaza pamoja na changamoto zote hizi, mbunge wetu hayupo bungeni au labda yupo lakini domo limejaa mate, domo zege . Lakini mbunge wetu sisi ni wa chama cha mapinduzi ccm. Kwa hiyo ninamini yumo bungeni lakini ama kwa makusudi au kwa sababu yeye binafsi anazozijua ameamua kukaa kimya.

Mzee kama umeshindwa basi tupishe tutakuja wananchi wote maana naona huwezi Kuku akilisha.

Uvumilivu sasa basi.
Ni vema mkaboresha kale ka wimbo chenu...oooooohhhh ni ile ile.............mtaisoma namba......lakini bado nina stahajabu maajabu ya Musa hivi kweli zaidi ya Miaka 55 ya Uhuru chama hicho kimeshindwa kuleta Maendeleo kwa wananchi wake kulingana na rasilimali tulizo nazo.
Si vema kumjadili Mh. huyu maana kapanda basi Bovu huwa halifikagi safari zake zote toka enzi za TANU na ASP (1950's-Karne ya 19), na hadi leo CCM (1970's-Karne ya 21).
 
Kiranjamkuu acha kutetea ujinga.
Wewe upo lumumba unazungumza kutokea dar wakati wanaolalamika wapo jimboni.

Acha uchawi wa maneno!
Wana matombo tupo pamoja,Tujifunze kuchagua mtu si chama,2020 akijalia Mungu tusirudie ujinga wa mwaka hu
huyu sijui ni baba ake. mpaka anachefua watu humu
 
Tatizo la watanzania ukifikaga uchaguzi sijui wanalewa pombe ya wapi wana wapigia kura watu wale wale chama kile kile, baada ya hapo vilio mtindo mmoja.
 
Tatizo la watanzania ukifikaga uchaguzi sijui wanalewa pombe ya wapi wana wapigia kura watu wale wale chama kile kile, baada ya hapo vilio mtindo mmoja.

We acha tu. Tatizo wazee wengi kaka huku
 
ha ha ha ha ha ha ha ha ha haha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha watu walipokuwa wanazungusha mikono muliwaona kama vichaaa vile haya.
 
Unalalama kitu gani wakati ile chorus maarufu isemayo tumeipenda wenyewe,mtaisoma namba sijui mbele kwa mbele mliimba nyinyi.
 

Attachments

  • 1465568520843.jpg
    1465568520843.jpg
    58.5 KB · Views: 78
Mkuu hufahamu kuwa kazi ya mbunge wa ccm ni kugonga meza,kusema ndio na kuitetea serikali?

Kazi yakutetea wananchi ni ya UKAWA.
 
Tawa nenda ofisi ya kata yako ya Kisemu Jtatu onana na WEO wako muulize mipango ya ujenzi wa barabara na ujenzi wa shule za A level kwa wilaya ulivyo kwa mwaka huu wa fedha.

Usiwe unasema tu kwenye mitandao kiongozi, anzia kufuatilia kuanzia ulipo.

Pia ukifika ofisi ya kata ulinza tangu MP ameingia madarakani amefanya mambo gani kwenye jimbo lake.

Ukishaenza njoo hapa tujadiane.

Nahisi hujui vizuri majukumu ya MP unadhani kuongea sana bungeni ndo uchapakazi.

Mbunge anashiriki vikao vingi vinavyofanya maamuzi ya mambo unayosema sio lazima akige kelele bungeni.
 
Back
Top Bottom