TAWA
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 3,673
- 1,571
Salamu wana jamvi,
Habari inayochukua nafasi ya juu ndani ya bunge kwa sasa ni mgogoro uliopo kati ya wabunge wanaounda umoja wa UKAWA dhidi ya naibu spika wa bunge dr. Tulia Ackson, jambo linalopelekea wabunge hao kutoka nje kila bunge lioongozwa na naibu spika huyo
Tabu yangu kubwa ni kwa mbunge wangu. Mbunge aliyepewa ridhaa na wananchi wa jimbo la Morogoro kusini kuwawakilisha bungeni. Mbunge huyu amebeba agenda nyingi za sisi wananchi wake.
1. Tuna matatizo ya barabara inayounganisha wilaya ya morogoro vijijini na manispaa ya morogoro. Barabara hii ni ya vumbi yoka mkoloni mpaka ninapoandika habari hii.
2. Huduma za elimu ni duni sana katika jimbo hili. Hakuna hata shule moja ya sekondari ya juu(advance level).
3. Wanayoiita hospital ya wilaya katika jimbo hili ni sawa na kituo cha afya cha tandale kwa mtogole pale wilaya ya kinondoni.
Kinachonishangaza pamoja na changamoto zote hizi, mbunge wetu hayupo bungeni au labda yupo lakini domo limejaa mate, domo zege . Lakini mbunge wetu sisi ni wa chama cha mapinduzi ccm. Kwa hiyo ninamini yumo bungeni lakini ama kwa makusudi au kwa sababu yeye binafsi anazozijua ameamua kukaa kimya.
Mzee kama umeshindwa basi tupishe tutakuja wananchi wote maana naona huwezi Kuku akilisha.
Uvumilivu sasa basi.