Mbunge Waitara aitwa kwa RCO Dodoma kwa mahojiano juu futari aliyomwalika Lowassa

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,841
Kuna taarifa nimezipata mbunge wa ukonga Waitara ameitwa Polisi ofisi ya RCO Dodoma kuhojiwa juu ya futari aliyoandaa Ukonga Dar na kumualika mh Lowassa.

Inasemekana Waitara kaomba mahojiano hayo yakafanyikie Dar wamekataa na kusema wameelekezwa mahojiano yafanyike hapo hapo Dodoma.

Nchi ya viwonder!

======

Dodoma. Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara amehojiwa na ofisa wa polisi katika viwanja vya Bunge kwa kile alichokieleza ni kutokana na futari aliyoiandaa jimboni kwake.

Mwita amesema mahojiano hayo yanatokana na futari ambayo alimwalika Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, ambaye alitoa maneno yanayodaiwa yalionyesha kuikera Serikali.

"Amejitambulisha kwangu kuwa ni polisi, lakini jana (Julai 4) pia nilipigiwa simu na ofisa upelelezi Mkoa wa Dodoma akinitaka niende kwa mahojiano," amesema Waitara.

Mahojiano kati ya Waitara na ofisa huyo yamefanyika eneo la mapokezi katika jengo la utawala la Bunge muda mchache baada ya mkutano wa saba wa Bunge kuahirishwa leo (Julai 5).

Chanzo: Mwananchi
 
Kuna taarifa nimezipata mbunge wa ukonga Waitara ameitwa Polisi ofisi ya RCO Dodoma kuhojiwa juu ya futari aliyoandaa Ukonga Dar na kumualika mh Lowassa.
Inasemekana Waitara kaomba mahojiano hayo yakafanyikie Dar wamekataa na kusema wameelekezwa mahojiano yafanyike hapo hapo Dodoma.
Nchi ya viwonder!
Wanashindwa kibiti wanahangaika na upinzani
 
Kuna taarifa nimezipata mbunge wa ukonga Waitara ameitwa Polisi ofisi ya RCO Dodoma kuhojiwa juu ya futari aliyoandaa Ukonga Dar na kumualika mh Lowassa.
Inasemekana Waitara kaomba mahojiano hayo yakafanyikie Dar wamekataa na kusema wameelekezwa mahojiano yafanyike hapo hapo Dodoma.
Nchi ya viwonder!
Vyombo vya dola vinafanya kazi sana jamani, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, hivi Ndugai aliponaje siku alipopiga mtu mpaka kuzirai?
 
Walisema Kikwete ni Rais dhaifu kuwahi kutokea Tz. Baba wa watu kwa upole na hekima zake kawaletea Rais shujaa sasa wanamuita dictator. Mm simo!
Nabda kutokana na hilo ndio maana wakwita dhaifu maana asingekuwa hivyo angemleta mtu mwingine
 
Back
Top Bottom