ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,898
- 50,629
Sawa ila kwenye FAO la kujitoa Kwa Wafanyakazi wa private sector ambao hawana permanent terms hakuna Haki kabisa.Pension unapokea maisha yako yote ni uha8 wako tu hiyo miaka 12.5 ni mambo yao tu ya mahesabu yao.Lakini pension ya mwezi utapokea mpaka unafariki mfano kuna waliostaafu 1990 hadi leo miaka 34 bado wanalipwa pension yao ya kila mwezi .Hiyo kusema ni miaka 12.5 sio sahihi kuwa baada ya muda huo inakatika sio kweli
Tatixo unakuta hata baadhi ya wabunge unakuta kakomaa hana akijuacho kichwani anaongea kwa kujiamini na ujinga wake anasema pension kulipwa mwisho miaka 12.5 yaani mpaka nasikitika kwa kweli baadhi ya wabunge waliomo mule labda waliingia kwa kuloga sio kwa sifa za weledi.Mbunge akamalia hilo mbishi .Si aulize hata wazee wastaafu tu wamwambie walioko mitaani? Ndio maana wengine wanssema wabunge wengi mule wanawakilisha nafsi zao sio mawazo ya wananchi.Kitu kidogo tu hicho mbunge alipaswa akijue.Kuwa pension ya kila mwezi mtu hulipwa kila mwezi hadi kifo chake.Ndio maana ya mwezi ikiwa kubwa ni bora zaidi kwa mstaafu sababu ndio maisha yake yatakuwa huko ili asije kusumbua ndugu na mikelele kuwa ohh hamnitunzi au kulaumu serikali kuwa ohh tulifanya kazi jwa 8aminifu serikali imetusahau kikotoo kimezingatia hilo.kuogopa lawama mbele ya safari mtu akiwa kikongwe asijiweza
Wengine wako Sekta ya Umma ila sio permanent terms Ajira zao zikikata Huwa hawatendewi Haki Kwa kuwa FAO la kujitoa halipo.