Mbunge wa Ukonga upo likizo?

Mbunge wa Ukonga upo likizo?

I agree! Na hilo ni iwapo kutajitokeza wagombea wengi. Lakini kama atajitokeza mmoja kama ambavyo mara nyingi huwa inakuwa, basi haitakuwa shida kusema fulani endelea.

Mkuu nachotaka kukuhakikishia ni kwamba mwaka 2015 Ukonga litakuwa ni mojawapo ya majimbo yatakayokuwa na mchuano mkali ndani ya chama chetu. So far kuna watu sita wameshatangaza waziwazi nia ya kuutaka ubunge wa Ukonga, hadi kufikia mwaka kesho naamini list itakuwa ni ndefu kweli kweli.

Muhimu ni sisi wenyewe tu kujipanga jimbo hili ni letu kabisa. Ukirudi tutafutane mkuu.
 
Ama hivi Ukonga ni Jimbo? Miye nikadhani lilibadilishwa jina kuwa Segerea.....ni taabu sana kuwa na jimbo lina jina la gereza aisee
 
Kamanda Lukolo mimi nipo Mongolandege.
Mstahiki meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa kama kuna mambo umejaribu kumtumia yakafanikiwa basi una bahati nzuri.

Mimi niliwahi kumfuatilia sana kuhusu ufunguzi wa zahanati ya Mongolandege, ambayo ujenzi wake ulikamilika mwishoni mwa mwaka 2010 kabla ya uchaguzi mkuu lakini haukuwahi kutoa huduma kwa takribani mwaka mzima hadi pale wananchi walipopiga kelele sana.

Baada ya kubana nae, nakumbuka alinijibu siku moja kuwa kuendesha manispaa kubwa kama ilala ni sawa na kuendesha meli, kwakweli nilicheka tu kimya kimya. Nikajiuliza kama Jery alikuwa anatambua ukubwa na uzito wa kazi ya umeya aliyokuwa anaililia.

Anyway, hata hivyo zahanati imefunguliwa mwaka jana, ingawa haina vifaa tiba, wameleta wauguzi na manesi kama watatu au wanne ambao wanatibu kwa "kupiga ramli" kwakuwa hakuna kifaa chochote cha kufanyia kipimo, hata kipimo cha maleria hakuna. Na kichekesho zaidi ni kwamba zahanati hiyo inafunguliwa Jumatatu hadi Jumamosi, na siku za Jumapili inafungwa!!! Sasa jiulize kama jumapili watu hawaumwi ama hawahitaji matibabu???... eti meya aliyeshindwa kazi naye anafanya kampeni za kutaka kuwa mbunge.

Btw, tutafutane weekend moja tuone ni namna gani tunaweza kuunganisha nguvu na viongozi wa Chadema jimbo la Ukonga ili tuhakikishe kuwa 2015 hatupotezi jimbo kwa kuliacha kwa wauza sura wa magamba, ambao wamethibitika pasipo shaka kuwa hawawezi kutukwamua kamwe.

Mkuu mimi pia ni mkazi wa ukonga,na nimetamani siku nyingi sana kupata watu wa kusaidiana nao,kuhakikisha 2015 tunamsimamisha mtu makini kuchukua hili jimbo,na jinsi huyu mama alivyo unga hata 2010 kama chadema tungekuwa makini tungechukuwa jimbo,naomba kwenye hicho kikao mkakati nishirikishwe na tena kisichelewe,kamanda Mwita vipi watu wanakutaka ugombee,jimbo jeupe hili.
 
Last edited by a moderator:
Nimekua ukonga tangu 80s hili jimbo letu halijawahi kuwa na mbunge makini hata siku moja tangu enzi za Rupia hadi sasahivi chondechonde 2015 tusirudie makosa
 
Ama hivi Ukonga ni Jimbo? Miye nikadhani lilibadilishwa jina kuwa Segerea.....ni taabu sana kuwa na jimbo lina jina la gereza aisee

Mkuu Safari_ni_Safari tafadhali tuheshimiane kidogo.
Sasa mbona unalifananisha jimbo la Ukonga na Segerea ambayo yote yanatumia majina ya magereza!!? au ndio sababu ya kukosa mwakilishi makini? au wananchi wake wanajiona kama vile wako maagereza wamefungwa...???
 
Last edited by a moderator:
Nimekua ukonga tangu 80s hili jimbo letu halijawahi kuwa na mbunge makini hata siku moja tangu enzi za Rupia hadi sasahivi chondechonde 2015 tusirudie makosa

Wana wa Ukonga tujipange vizuri ili mwaka 2015 tusiruhusu kwa namna yoyote kupoteza miaka mingine mitano bila muwakilishi bungeni.
 
Mkuu Safari_ni_Safari tafadhali tuheshimiane kidogo.
Sasa mbona unalifananisha jimbo la Ukonga na Segerea ambayo yote yanatumia majina ya magereza!!? au ndio sababu ya kukosa mwakilishi makini? au wananchi wake wanajiona kama vile wako maagereza wamefungwa...???

Mkuu nisamehe bure.....niliangalia kwa context hiyo tu ya majina ya magereza.....no disrespect to anyone....hivi kuna jimbo la Keko?
 
Tumpe Mwita Maranya, kama hatakuwa tayari; basi mimi nitagombea kwa tiketi ya CHADEMA.
Huyu ni Mwita Maranya ni huyu aliyekuwa mwenyekiti wa FOS?baadae akawa raisi wa DARUSO?any way awe yeye au siyo yeye nitamuunga mkono kwenye mchakato,yaani ile barabara jamani mvua zikinyesha haipitiki,kitunda yetu jamani tutaindeleza sisi yenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Ama hivi Ukonga ni Jimbo? Miye nikadhani lilibadilishwa jina kuwa Segerea.....ni taabu sana kuwa na jimbo lina jina la gereza aisee

leo utakuwa umevuta,huandikagi ujinga kama huu!kwani segerea hamna gereza?umenishangaza kweli!au unatania?
 
leo utakuwa umevuta,huandikagi ujinga kama huu!kwani segerea hamna gereza?umenishangaza kweli!au unatania?

Ni kweli leo nimevuta cheki yangu ya mafao....thanks...sijasema Segerea hakuna gereza nisome vizuri...hoja yangu kwa nini majimbo mawili yanayopakana yapewe majina ya magereza kwa nini yasiitwe jimbo la TABATA na KIPAWA?
 
Mkuu mimi pia ni mkazi wa ukonga,na nimetamani siku nyingi sana kupata watu wa kusaidiana nao,kuhakikisha 2015 tunamsimamisha mtu makini kuchukua hili jimbo,na jinsi huyu mama alivyo unga hata 2010 kama chadema tungekuwa makini tungechukuwa jimbo,naomba kwenye hicho kikao mkakati nishirikishwe na tena kisichelewe,kamanda Mwita vipi watu wanakutaka ugombee,jimbo jeupe hili.

Mkuu sisi sote kama wana Ukonga tuna wajibu wa kuunganisha nguvu zetu kuhakikisha kwamba tunapata mbunge bora kuanzia mwaka 2015. Haya madhila tunayokutana nayo ya kutokuwa na muwakilishi makini lazima tuondokane nayo kwa kuhakikisha kwamba tunashirikiana kwa hali na mali ili kufikia malengo ya kuwa na muwakilishi bora.

Hebu fikiria tangu alipotangazwa kuwa mbunge wetu huyu mama hajawahi kuitisha mkutano japo mmoja tu kuzungumza na wananchi anaowawakilisha.
 
miaka 5 sio mingi waungwana waacheni wabunge watulie wafanye maendeleo yao ili wasiporudi mjengoni waweze kuendelea na mishe mishe zingine! mnakaba sana wananchi!
 
Mkuu nisamehe bure.....niliangalia kwa context hiyo tu ya majina ya magereza.....no disrespect to anyone....hivi kuna jimbo la Keko?

Hakuna shakaa mkuu tuko pamoja, najua what you meant if one reads between the lines!!
Jimbo la keko sijawahi kulisikia, nimewahi kusikiia kata ya keko. Pia nimewahi kusikia kata ya maweni-Tanga!!
 
Huyu ni Mwita Maranya ni huyu aliyekuwa mwenyekiti wa FOS?baadae akawa raisi wa DARUSO?any way awe yeye au siyo yeye nitamuunga mkono kwenye mchakato,yaani ile barabara jamani mvua zikinyesha haipitiki,kitunda yetu jamani tutaindeleza sisi yenyewe.

Mkuu Azote huyu ni Mwita Maranya wa JF na huyo wa FOS na UDSM ni Mwita Mwikwabe.
Kwakweli mkuu tunahitaji kuunganisha nguvu zetu this time ili kuhakikisha kwamba tunapata mbunge mwenye uwezo wa kuhamasisha na kutoa msukumo mkubwa wa maendeleo hasa katika upande wa miundombinu ya barabara, maji na afya.
 
Last edited by a moderator:
Jamani wakazi wa ukonga nawapa pole kubwa sana, sijawahi ona urojo kwenye kituo cha daladala hii nimeiona ukonga. Nawapa tena pole jipangeni!
 
Mwingine ni makongoro mahanga,huyu ni mwiz wa kura na hautosikia hata siku 1 anaongea co mjengon wala jimbon
 
Mkuu nachotaka kukuhakikishia ni kwamba mwaka 2015 Ukonga litakuwa ni mojawapo ya majimbo yatakayokuwa na mchuano mkali ndani ya chama chetu. So far kuna watu sita wameshatangaza waziwazi nia ya kuutaka ubunge wa Ukonga, hadi kufikia mwaka kesho naamini list itakuwa ni ndefu kweli kweli.

Muhimu ni sisi wenyewe tu kujipanga jimbo hili ni letu kabisa. Ukirudi tutafutane mkuu.
wow! good news. Sikujua kabisa kama kuna list kubwa kiasi hicho. Inapendeza na inatia moyo sana mkuu. Thanks kwa info hii.
 
Back
Top Bottom