Mbunge wa Ukonga huoni haya?

Mbunge wa Ukonga huoni haya?

kimaus

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
584
Reaction score
707
Kama mkaazi wa Kivule/Kitunda, inaumiza sana kuona tuna mbunge ambaye haona aibu jimbo lake kuwa na barabara mbovu kuliko zote Dar esalaam.
Barabara ya kutoka Ukonga Banana kupitia Kitunda, Kivule hadi Msongola ni kama haipitiki, imejaa mahandaki, madimbwi ya maji kiasi kwamba kutoka Banana kufika Kivule fremu 10 unaweza kutunia saa nzima au zaidi!!
Ulisema kwa kuwa ulikuwa upinzani ndio maana hukuwa unatengewa bajeti za maendeleo, sasa umerudi chama tawala, mbona barabara hii haijengwi?
Jisikie aibu hata kidogo, kama huwezi kushawishi tukajengewa hii barabara then 2020 go back to Rorya, this is Dar es Salaam in 2019, we don't deserve to have roads like this one!
 
Vipi umeanza kampeni? Mbona mapema sana?
 
Mbagala ndy usiseme njoo stendi ya mabasi ya mjini utaomba poo mitope yaani uku atutaki mvua maana ni shida
 
Tuache utani,hii barabara tangu masika ya mwaka jana inajengwa.Hebu angalia Mbagala Road haina hata miezi miwili,imefika Aziz Ally.
 
Tafadhari tunajenga Reli ya kisasa na kwa sasa asilimia 75 imeshakamilika
Kuweni wavumilivu hatuwezi kutekeleza miradi yote kwa wakati mmoja
 
Ni yule yule ambae bilioni 43 + bil 18 ni sawa na bilioni 1
 
Kidaraja kilichopo hapo kitunda kinajengwa huu mwaka wa 6 hakijakamilika

Hii barabara nadhani ni makusudi yanafanyika
 
Sio huko tu, ukweli kata yote ya ukonga haina barabara, nimezunguka huko kivule, nimepita mpaka majohe kunaitwa bwela, dah unaweza kufanya mradi wa kufuga samaki kwenye hizo barabara.
 
Vipi umeanza kampeni? Mbona mapema sana?
Grow up!
Mi ni mwananchi ninayekerwa na maendeleo duni jimboni kwangu. Hayo ya siasa ni yako! Hoja ya msingi, barabara ya Banana Msongola ni mbaya!
 
Sio huko tu, ukweli kata yote ya ukonga haina barabara, nimezunguka huko kivule, nimepita mpaka majohe kunaitwa bwela, dah unaweza kufanya mradi wa kufuga samaki kwenye hizo barabara.
Mm nadhani miradi mingi ya barabara kwa sasa daresalam imesimama sijui wanangoja campaign 2020! kutoka wazo hadi kwa kawawa madale lipoishia lami ya kutoka njianne goba ni balaa,unaweza dhani unaenda Nanjilinji
 
Maeneo hayo hayana shida ya maji kwa kuwa wananchi wengi wana visima vyao na wanawasambazia mabomba majirani zao, lakini cha ajabu baadhi ya fedha za maendeleo zimetengwa kwenye miradi ya maji. Haya ni matumizi mabaya ya rasilimali chache zilizopo.
 
Vipi umeanza kampeni? Mbona mapema sana?
Ndugu yangu usilolijua ni sawa na usiku wa giza leo Nimeenda kukagua shamba langu kama kilometa 1.5 kutoka fremu kumi karibia na shule ya dady nimejuta yan nimehurumia gari yangu. Huwezi amini kuna madimbwi unaingia boneti inafunikwa. Yani nadhani hii sio bure. Ndio maana waitara amehama kwake kitunda shule na kuhamia gongolamboto baada ya madai ya kulamba 200m kama zawadi ya kuunga juhudi mkono
 
Back
Top Bottom