Mbunge wa Ukonga, Chacha Waitara kazi imekushinda

Huyu jamaa nilimkuta sehemu aloo ni mlevi balaa halafu ana kauli chafu sana,
Nataka nipige bei plot yangu maeneo ya huko maana sio siri barabara hazipitiki kweli full kunasa.

Ni katika wabunge ambao 2020 bunge wataliona kwenye Tv tu.
Piga bei hiyo ploti yako kisha mpe hizo hela atengeneze barabara, hawezi kutoa pesa yake mfukoni ajenge barabara.
 
nashukuru sana kwa ushauri...naufanyia kazi..ila msalimu waitara kazi imemshinda...ukonga sio tarime...mjini lazima uwe na pesa ili uongoze ukitegemea kila kitu serikali utakwama....yameshamkuta
Ulitakiwa useme mapema nn wataka, kumbe shida yako n pesa?

Miundombinu ya barabara wasubiri TARURA wao ndio wenye pesa ya kufanya hayo yote.

Kama unahitaji pesa ya Waitara mfate atakupa.
 
Kazi ya mbunge ni kuishauri serikali na kuisimamia kufikisha mahitaji ya wananchi majimboni mwao, na serikali isipotimiza ni wajibu wa mbunge kurudi kwa wananchi kuishitaki serikali kwamba haijakubali kutekeleza lile wananchi wanalotaka. Sasa mbunge wa Ukonga waitara kafanya lipi hapo?
 
Bado sijaona mtu wa kumuondoa Waitara Ukonga 2020.

Ila kwakuwa ni demokrasia tunatarajia kupata mshindani kutoka ccm ili amsindikize.

Kazi za kimaendeleo zilizofanywa na Waitara kwa kipindi cha miaka miwili ni zaidi ya wabunge wote waliomtangulia. Kuanzia kwenye miundombinu ya elimu, afya, barabara, maji, uwezeshaji kiuchumi na kuwasilisha mahitaji ya wana Ukonga serikalini kupitia bunge la JMT na vikao vya baraza la madiwani.

NB:
Waitara hakushinda ubunge kwasababu ya vikao vya Wanywa mataputapu bali kwa hoja muhimu zinazogusa maisha ya wana Ukonga lakini pia na uwezo wake wa mikakati ya ushindi kupitia watu makini katika team yake ya kampeni na pia uimara na mshikamano wa wanachama wa Chadema.

Kuhusu Waitara kutokupatia fedha kwa mambo/matatizo yako binafsi hayana tija kwa muktadha huu na sio maslahi ama mahitaji ya wapiga kura wa Ukonga.

[HASHTAG]#Ukonga[/HASHTAG] ipo katika mikono salama ya Waitara.
 
Acha maneno kuna kiini cha hayo matatizo na sio waitara...hujui kama serikali haifanyi kazi na wabunge wa upinzani??au hujawahi kumsikia mkuu akisema mchague ccm iwaletee maendeleo???

Maana yake mkichagua wapinzani sahau kuhusu maendeleo jombaa,zipiganieni 1.5t kama kweli unataka maendeleo Ukonga.
 
Wao wanaona sifa kuipinga "Serikali" bila kujijua kuwa na wao ni Serikali (Bunge). Wanadhani Meya WA Jiji Isaya ni mjinga anavyoshirikiana name Serikali. Ngojeni wapate sifa mitandaoni but 2020 iko mlangoni mwao.
 

Ukonga hakina Mbunge anayeitwa Chacha Waitara... Pili Mbunge hakusanyi kodi ya Ukonga, kama wanaokusanya kodi ndani ya mwaka Mmoja tu 1.5T hazionekani na huenda zimenywewa Pombe na watu wa aina yako unategemea kitu gani?

Pili wabunge upinzani hawafanyi kazi zao kwa kelele za MaCCM kwani tangu Uhuru hadi 2015 Jimbo LA Ukonga likikuwa mikononi mwa MaCCM.

Ukonga zimejengwa Shule za msingi zaidi 15 ndani ya miaka miwili ya Mbunge Waitara.

Msongamano wa watoto umepungua kutoka 150-200 Kwa darasa moja hadi Chini ya Mwanafunzi 70, mbona hamusemi...

Leo 2018 ndiyo mmegundua UKONGA inahitaji Barbara wakati miaka 50 tangu Uhuru mmelala.

Nendeni mtuambie 1.5T ikowapi?
 
Kura za wananchi Ndio zinampa Ubunge, nyie bakini na vikao vyenu vya usiku kucha bado Waitara atachaguliwa kuendelea kutawala hilo Jimbo

Mkuu nakuhakikishia hakuna wakumchagua waitara tena hata yeye anajua, Mimi nakaa Ulongoni B hali ni mbaya mbunge hata kuipigia kelele serikali wapi, nyumba hadi nyumba wanalaani kwa kumchagua
 
Waitara alipata ubunge sababu ya upepo wa mageuzi, ikumbukwe vyama viliungana kuing'oa ccm na ushawish mkubwa Wa Mzee lowasa
 
Piga bei hiyo ploti yako kisha mpe hizo hela atengeneze barabara, hawezi kutoa pesa yake mfukoni ajenge barabara.
Nyie mvimbisheni tu kichwa ila mwambie na ajue afanye hizo kufuru zake amalize kwani 2020 bungeni ndio bye bye.

Nb: Anajua vizuri sana hata kuchaguliwa kwake alichaguliwa sababu ya kuikomoa kamati ya upinzani wake walipomteua Jerry, kama wangemuweka yule Kanjibai aliyekua anatakiwa na wengi hahaha Waitara bungeni asingepeleka pua yake.
 
Wewe ni mpuuzi, kwa kero za gongo LA mboto waitara akipata tena ubunge nitajua wakaz wa hayo maeneo hawana akili za kutosha, waitara hana mpanga wa kugombea tena na ndo mana amecool, miaka 5 inamtosha kama hana aibu asimame 2020
 
Wewe ni mpuuzi, kwa kero za gongo LA mboto waitara akipata tena ubunge nitajua wakaz wa hayo maeneo hawana akili za kutosha, waitara hana mpanga wa kugombea tena na ndo mana amecool, miaka 5 inamtosha kama hana aibu asimame 2020

Unawez kwenda kuchukua posho yako ya leo kwakuwa umetumiza wajibu uliotumwa hapa JF leo. Gongolamboto watu wana akili zao sio wasaka posho za majungu kama wewe.
 
Mkuu nakuhakikishia hakuna wakumchagua waitara tena hata yeye anajua, Mimi nakaa Ulongoni B hali ni mbaya mbunge hata kuipigia kelele serikali wapi, nyumba hadi nyumba wanalaani kwa kumchagua
Wewe nae huko ulongoni umehamia lin mpaka utake kusikia kelele za mbunge?? Miaka zaid ya 50 hkn barabara hilo daraja tu linawapa shida mvua zikianza.

Ipo cku mtapiga mbizi akili iwakae vzr nn barabara hata daraja hkn
 
Povu la nn, kama unamjua vzr mbunge wako mfate kwake umalizane nae
 
mwita maranya unaleta ukabila katika masula nyeti kabisa ya jimbo la ukonga.....

Kafanya lipi katika miundo mbinu???? Elimu kafanya lipi???? vyumba vya madarasa karibu kata zote hajachangia chochote kama mbunge......

Sihitaji pesa ya huyo jamaa mimi ni mhandisi na nina ajira inayonifanya nipate pesa nzuri tu ya kunitosha ila naangalia maslahi mapana ya wanaukonga ila wewe unaangalia maslai ya ukabila..

Kuhusu kujenga hoja wakati wa kampeni aiseeee Basi tu kwakuwa yule mayor slaa alishaharibu na tulikuwa hatumtaki tena ndo mana hata kama chadema wangeweka jiwe bado tungechagua jiwe kuliko slaaa...ila kwa ujenzi wa hoja mayor silaa alikuwa vizuri kuliko waitara.....

Jimbo la ukonga linapita katika kipindi kigumu haijawai tokea katika kipindi hiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…