Mbunge wa TEMEKE, Abdallah Mtolea (CUF) alala Korokoroni, Bima ya gari yamponza

Vyombo vya polisi vinamchafulia sana Magufuli na kumtengenezea sifa mbaya.

Lengo nadhani kila mtu atii sheria sio kukamata kwa kujisikia kisa raisi anataka wafanye kazi yao bila kumuacha mvunja sheria yoyote.

Civil matters ya kukamata gari tu mtu anaenda jela
Nini adhabu ya mtu kukimbia polisi? Polisi waache majukumu yao wakufute wewe hadi kwako, wachome mafuta yao na muda halafu bado wakupige fine tu? Itakua ukiwa unaongea na mwanao halafu akaondoka kwa dharau mbele yako kabla hamjamaliza unampa zawadi
 
Safi sana jeshi la polisi, mtu akileta dharau ashughulikiwe kikamilifu, huyo mbunge alitakiwa awe kioo cha jimii, lakini analeta dharau. Hatumrudishi tena bungeni, hana lolote analotusaidia wana tumeke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hizi jela zetu zipo kwa ajili ya rehabilitation au kukomoana?gari bila bima ni kosa la kukulaza ndani?polisi wetu naamini wanafundishwa jinsi ya kutumia busara wanapokabiliwa na mtuhumiwa mwenye hasira as far haatarishi usalama wa polisi,raia wengine na yeye mwenyewe,na kuendesha gari bila bima lina hasara zaidi kwa mwenye gari hasa linapohusika kwenye ajali sio kosa la kumpeleka mtu rumande,again narudia tunazidi kujenga chuki kati ya raia na polisi na kutengeneza generations ya ghasira,visasi na chuki,time will tell.
Hujazungumzia kosa la pili la kukimbia polisi. Kosa la kutokuwa na bima ni fine la kukimbia polisi je? Maana huyu mbunge kafanya yote mawili
 
Sipendagi kurumbana na polisi maana wanaweza kukulaza ndani ili wakuoneshe wao wanaweza kufanya hivyo.
Na ndio maana huwa wakinikamata nawaambia waniandikie au wachukue rushwa, kupotezeana muda kisa 30000 hapana

Tujitahidi kuwa makini maana hawa watu wana hasira na sifa juu
na mkulu kashawapa go ahead,saiv wanatamba wao tu.
 
Hivi hizi jela zetu zipo kwa ajili ya rehabilitation au kukomoana?gari bila bima ni kosa la kukulaza ndani?polisi wetu naamini wanafundishwa jinsi ya kutumia busara wanapokabiliwa na mtuhumiwa mwenye hasira as far haatarishi usalama wa polisi,raia wengine na yeye mwenyewe,na kuendesha gari bila bima lina hasara zaidi kwa mwenye gari hasa linapohusika kwenye ajali sio kosa la kumpeleka mtu rumande,again narudia tunazidi kujenga chuki kati ya raia na polisi na kutengeneza generations ya ghasira,visasi na chuki,time will tell.
umesoma vizuri maelezo lakini?
 
Nini adhabu ya mtu kukimbia polisi? Polisi waache majukumu yao wakufute wewe hadi kwako, wachome mafuta yao na muda halafu bado wakupige fine tu? Itakua ukiwa unaongea na mwanao halafu akaondoka kwa dharau mbele yako kabla hamjamaliza unampa zawadi
Kutokuwa na bima sio criminal offence hujui polisi walikuwa wanamletea upuuzi gani mwingine

Polisi sio mungu akisema fanya hivi iwe ivyo kazi yao ni kwa mujibu wa sheria. Na raia analindwa na sheria izo izo sasa kuondoka Kama watu wanakuletea upuuzi sidhani kama ni kosa ukizangatia kosa lenyewe ni la civil.

Mbona alisimama aliposimamishwa mara ya kwanza kam kweli aeshimu polisi. Anyway mazingira halisi ayajulikani lakini polisi waache kutumia nguvu zao vibaya.
 
Kutokuwa na bima sio criminal offence hujui polisi walikuwa wanamletea upuuzi gani mwingine

Polisi sio mungu akisema fanya hivi iwe ivyo kazi yao ni kwa mujibu wa sheria. Na raia analindwa na sheria izo izo sasa kuondoka Kama watu wanakuletea upuuzi sidhani ukizangatia kosa lenyewe ni la civil.
Vizuri kamwambie korokoroni kwamba aendelee kukimbia polisi na wewe endelea hivyo hivyo. Ndo maana mnamtaka Lowassa sababu hakutakuwa na utawala wa sheria nchini?
 
Nawauliza tu waungawana, hivi Mbunge Nagu alilala rumande juzi? Ikiwa Nagu alilala rumande juzi kwa hizo saa 48 kama alivyoamuru DC nitakuwa sina neno na nitawapongeza serikali na polisi, lkn ikiwa Nagu hakulala rumande, nitakosa imani kabisa ba serikali na jeshi la polisi.

BTW, gari kuisha insurance na mmiliki kujisahau ni jambo la kibinadamu na wala sio kosa la kumlaza dereva ndani, labda kama kuna makosa mengine.

Vv
Mwendesha gari mwenye mafunzo timamu kuendesha gari bila bima ni kosa kubwa sana.Ikitokea ajali umekwisha.
Tuache siasa.
 
Vizuri kamwambie korokoni kwamba aendelee kukimbia polisi na wewe endelea hivyo hivyo. Ndo maana mnamtaka Lowassa sababu hakutakuwa na utawala wa sheria nchini?
Nonsense kama huna hoja kaa chonjo sio kuandika upuuzi.
 
mwananchi.PNG
mwananchi 1.PNG

Chanzo: Mwananchi
 
Ni kweli kabisa, ukidharau mamlaka nayo itapenda kukuonyesha makucha yake.

Mimi nilikamatwa sehemu za Mafinga nikiwa nimepigwa tochi juu ya 50km/hr!
Sikuwa na wasi wasi maana spidi ilikuwa kama 58km/hr, nikamwambia askari mbona hayo mambo madogo, ninawahi Mbeya na kwa kweli nilikuwa nimepunguza spidi.

Askari akasema hebu nione leseni yako.
Bila tatizo na kujiamini nikitoa na kumpa.
ALAHAULA!!!
Kumbe leseni imeisha mizi sita!!!!

Askari alipokuja juu, nikamwambia chonde chonde mzee.
DSM tunaendesha kwa mazoea na sijacheki leseni yangu muda wa kuisha, niko chini ya miguu yako na hapa katikati ya pori, huruma yako tu.

Na kwa kweli sikuwa na ujanja.
Yule askari aliona point, akanipiga fine na kunielekeza kitu cha kwanza ukifika Mbeya ifufue leseni, usije pata ajali na yakakupata mabaya Zaidi.
Nilimshukuru na nikaondoka.

SOMO:
Jamani uungwana ni kitu cha bure na haifundishwi darasani!
Ningemwonyesha Mapembe yule askari wa cheo cha chini, lazima angeniripoti kwa mkubwa wake mwenye mamaka ya kunichukulia hatua kubwa zaidi.
Uungwana ni ubinadamu.
Hongera sana Boss. Hukutaka kutumia ukubwa wako. Kudo!
 
Back
Top Bottom