Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea ataka CHADEMA ifutiwe usajili

Ni kweli, hiyo itafanyika kwa hujuma kwakuwa rais ana nongwa na chuki binafsi dhidi ya cdm, hivyo anaweza kutumia madaraka yake vibaya kunajisi box la kura, ila sio kwa ridhaa ya wananchi. Madai ya tume huru ya uchaguzi yasisite baada ya Katazo la mikusanyiko kutokana na Corona. Toka hapo tutaelewana tabia. Kulazimisha kukaa madarakani kutaigharimu ccm na nchi kwa ujumla. Muda utaamua.
Uchaguzi ujao CCM Wana kazi kubwa ya kufanya maamuzi magumu wang'ang'anie madarakani nchi Ife Kama Zimbabwe au wakubali kushindwa chama kife Kama KANU au UNIP ya zambia
 
Kitafutwa tu. Mark my words!

Ni kweli kitafutwa, na sababu hasa ni ccm kuendelea kukosa mvuto kwa umma huku cdm ikiendelea kuteka nyoyo za watu. Jambo hili linaiumiza sana ccm, kwani ilitaraji umma uiunge mkono, lakini imejikuta inatumia nguvu kubwa kulazimisha umma kuikubali, huku cdm ikizidi kupata mvuto. Hofu kubwa ya ccm ni iwapo cdm itaendelea kushikilia madai halali ya tume huru ya uchaguzi, wanajua fika ikibidi kuwepo na tume huru watakosa ushindi wanaoutaka. Na iwapo watahujumu uwepo wa tume huru ya uchaguzi, wapiga kura watakuwa wachache mno, na jumuiya ya kimataifa itazidi kuiweka nchi kwenye mazingira magumu.
 
Wakuu habari za Leo?

Mheshimiwa Abdaallah Mtolea mbunge wa jimbo la Temeke ametoa pendekezo lake bungeni kuwa haoni sababu ya Chadema kuendelea kuwa chama cha siasa nchini,amemtaka msajili wa vyama vya siasa kukifuta chama hicho Mara moja

Amedai kuwa chadema ni chama kinacho penda Fujo na vurugu hivyo haoni thamani ya chama hicho nchini

My take : chadema wajihadhari tofauti na hapo tutaongea mengine baada ya uhakiki wa vyama vya siasa kumalizika

Have a good day.

Sent using Jamii Forums mobile app


CCM kinakaa madarakani kwa kutumia dola - Dr Bashiru

CCM kimepata hati chafu - CAG Kichere

Msajiri futa CCM nchi ikwepe umasikini, iendelee kwa kasi.
 
Huyo mbunge nadhani alistahili kuwa hospitali ya Mirembe, siyo bungeni.
 
Ni kweli kitafutwa, na sababu hasa ni ccm kuendelea kukosa mvuto kwa umma huku cdm ikiendelea kuteka nyoyo za watu. Jambo hili linaiumiza sana ccm, kwani ilitaraji umma uiunge mkono, lakini imejikuta inatumia nguvu kubwa kulazimisha umma kuikubali, huku cdm ikizidi kupata mvuto. Hofu kubwa ya ccm ni iwapo cdm itaendelea kushikilia madai halali ya tume huru ya uchaguzi, wanajua fika ikibidi kuwepo na tume huru watakosa ushindi wanaoutaka. Na iwapo watahujumu uwepo wa tume huru ya uchaguzi, wapiga kura watakuwa wachache mno, na jumuiya ya kimataifa itazidi kuiweka nchi kwenye mazingira magumu.
Ahahahah! Hata farasi anapokuwa anakata roho hurusharusha miguu kwa matarajio ya kukipiga teke kifo! Agahahaha! Rusha teke! Rusha kwa nguvu!
 
Yaani Dula Mtolea kawa zuzu kiasi hiki? Badala ya kuuliza yule polisi aliyemuua Akwilina alifanywa nini yeye anaisakama CDM! Badala ya kuhoji yule Mkurugenzi alichukuliwa hatua gani yeye yupo na CDM tu! CCM wanadhani wananchi tu mazuzu kama wao!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndomana mtaalamu mmoja alisema "Dawaamulhaal minalmuhaal "
Sio kwamba wanahimiza mapigano, wamechoka kuporwa kura zao, na ccm wameshaona kabisa watu hawaitaki hivyo inajua kitendo cha cdm kuendelea kuwepo kitaamsha hasira za watu na kuiweka ccm kwenye wakati mgumu. Hivyo namna pekee ni kutumia nguvu yake ya dola iliyo nayo sasa kuifuta cdm. Lakini napenda ufahamu, kwa sasa ccm ni chama kilicho nje ya mahitaji ya wakati, hata ifanye nini sio rahisi tena kuwavutia wananchi. Hiyo cdm hata kama haijafanya kitu, watu hasa kizazi cha sasa kitaipenda cdm, kwani kizazi kilichoipenda ccm muda wake umeshapita.

Hivyo ni vyema uwashauri ccm kuwa tatizo lao kwa sasa sio kuwa hawajafanya kitu, bali wakati ukuta. Hakuna namna kitaendelea kubaki madarakani tena kwa ridhaa ya wananchi walio wengi, sana sana itaishia kumwaga damu za vijana, na huko tuendako itaingiza nchi hii kwenye vikwazo vya kiuchumi kwa kitendo chake cha kung'ang'ania madaraka. Hiyo ccm naifananisha na mwanamme au mwanaume mzee anayelazimisha kupendwa huku akijipamba na kuhonga sana ili apendwe. Lakini kimsingi atakuwa hapendwi na vijana zaidi ya kuliwa hela zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbunge wa Temeke Nchini (CCM) Abdallah Mtolea amehoji kwanini Msajili wa Vyama vya Siasa nchini hakifuti chama cha CHADEMA kutokana na kufanya siasa za fujo na chuki licha ya kupewa meno na sheria iliyopitishwa na Bunge ya kumpa nguvu.

Mbunge huyo ambaye aliwahi kuwa Mbunge kupitia CUF katika jimbo hilo kabla ya kuhamia CCM mwaka 2018, ametoa kauli hiyo leo Aprili 3 2020 wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

“Mwaka jana tuliboresha sana Sheria ya Vyama vya Siasa na kumpa nguvu sana na meno Msajili wa vyama vya siasa, sasa ni lini atakuwa amejiridhisha kwamba matukio ya fujo, siasa za chuki kuamshwa mihemko ya hasira kwa wananchi zinazofanywa na Chadema kuwa ni sababu za kutosha kukifuta chama hicho,” amesema.

Amesema chama hicho kimesababisha fujo nyingi na miongoni ni fujo zilizosababisha kifo cha mwanafunzi Akwilina Februari 16, 2018 baada ya kukataa amri halali ya polisi na hakionyeshi kujutia jambo hilo.

“Baada ya humu yao Wakafanya vikao vingi wakilia kwa furaha wakati wao wakilia kwa furaha mama wa Marehemu Akwilina analia kwa uchungu. Mama yake Akwilina hana mtu wa kumfuta machozi. Kama sisi sio wa kumsemea ni nani aliyemsemeha,” amesema.

Amesema mbwembwe za kuchanganishana fedha hazikuwa zikifanywa dhidi ya CCM wala Serikali bali ni dhidi ya mama yake Akwilina ambaye amepoteza mtoto.

My take:
Chadema wajihadhari tofauti na hapo tutaongea mengine baada ya uhakiki wa vyama vya siasa kumalizika

Have a good day.
Stupid Idiot topic, hivi alieua Akwiline na Chadema au Polisi wa ccm ??, polisi aliyefunzwa akafunzika anashindwaje kulenga shabaha akapiga mguu wa mtuhumiwa na akapiga risasi Akwiline, halafu mahakama inajitoa akili inawafutia kesi polisi, na nyie kwa akili zenu mnakubali kulishwa ujinga na ufedhuri, chama kinachotakiwa kifutwa na ccm kwa sababu wameshindwa kufanya siasa na kuamua kuwa watekaji na wauaji.
 
Ahahahah! Hata farasi anapokuwa anakata roho hurusharusha miguu kwa matarajio ya kukipiga teke kifo! Agahahaha! Rusha teke! Rusha kwa nguvu!

Kwa taarifa yako ccm sio chama tena cha kuiua cdm kwa ushindani wa kisiasa, kinaweza tu kutumia nafasi ya mwenyekiti wake kwa kofia ya urais kuifuta cdm, ila sio kura zipigwe kisha ccm ipate kura za kuiua cdm.
 
Back
Top Bottom