digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 7,872
- 14,294
Mbunge wa Temeke Nchini (CCM) Abdallah Mtolea amehoji kwanini Msajili wa Vyama vya Siasa nchini hakifuti chama cha CHADEMA kutokana na kufanya siasa za fujo na chuki licha ya kupewa meno na sheria iliyopitishwa na Bunge ya kumpa nguvu.
Mbunge huyo ambaye aliwahi kuwa Mbunge kupitia CUF katika jimbo hilo kabla ya kuhamia CCM mwaka 2018, ametoa kauli hiyo leo Aprili 3 2020 wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
“Mwaka jana tuliboresha sana Sheria ya Vyama vya Siasa na kumpa nguvu sana na meno Msajili wa vyama vya siasa, sasa ni lini atakuwa amejiridhisha kwamba matukio ya fujo, siasa za chuki kuamshwa mihemko ya hasira kwa wananchi zinazofanywa na Chadema kuwa ni sababu za kutosha kukifuta chama hicho,” amesema.
Amesema chama hicho kimesababisha fujo nyingi na miongoni ni fujo zilizosababisha kifo cha mwanafunzi Akwilina Februari 16, 2018 baada ya kukataa amri halali ya polisi na hakionyeshi kujutia jambo hilo.
“Baada ya humu yao Wakafanya vikao vingi wakilia kwa furaha wakati wao wakilia kwa furaha mama wa Marehemu Akwilina analia kwa uchungu. Mama yake Akwilina hana mtu wa kumfuta machozi. Kama sisi sio wa kumsemea ni nani aliyemsemeha,” amesema.
Amesema mbwembwe za kuchanganishana fedha hazikuwa zikifanywa dhidi ya CCM wala Serikali bali ni dhidi ya mama yake Akwilina ambaye amepoteza mtoto.
My take:
Chadema wajihadhari tofauti na hapo tutaongea mengine baada ya uhakiki wa vyama vya siasa kumalizika
Have a good day.