Mbunge wa Ruangwa alazwa ICU

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
MBUNGE wa Ruangwa mkoani Lindi,Sigfrid Ng`itu, jana usiku alihamishiwa katika wodi ya wagonjwa mahututi(ICU) katika hospitali ya Taifa Muhimbili,kwa kuwa hali yake ilizidi kuwa mbaya.

Mbunge huyo amelazwa hospitalini hapo, Dar es Salaam akisumbuliwa na Ugonjwa wa Kiharusi.

Mbunge huyo alipelekwa Muhimbili Jumatatu mchana kutoka Hospitali ya Masanna, Mbezi, Dar es Salaam akalazwa katika wodi ya Mwaisela namba 313.

Kuna taarifa kwamba,ugonjwa unaomsumbua umesababisha apooze upande mmoja wa mwili wake.

Ofisa Uhusiano wa Muhimbili,Jezza Waziri amesema,Mbunge huyo alihamishiwa ICU jana usiku ili apate uangalizi maalum wa daktari baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya.

Mke wa Mbunge huyo, Prisca Ng'itu, jana alisema, mumewe alipatwa na kiharusi Jumapili usiku akapelekwa katika hospitali ya Masanna.

http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3624
 
Back
Top Bottom