Mkuu
JokaKuu
Barua ya Mbunge Selasini ina mambo haya
Kwamba,aliteuliwa na Mbowe baada ya tukio la TL kukaimu nafasi
- Hakuna barua rasmi iliyotolewa, yalikuwa ni maneno ya uteuzi.
-Hajapewa onyo la mdomo au maandishi kuhusu utendaji wake
-Amehudhuria vikao vya Bunge vya kamati za uongozi
Hoja: Mbowe alipaswa kumkaimisha nafasi hiyo kwa maandishi ili kuweka kumbu kumbu za kiofisi leo na kesho. Hakuna ajuaye nini kitatokea, hilo ni la muhimu ndani ya taasisi.
Pili, kuujulisha uongozi wa Bunge ili Selasini atambuliwe kama na si mwakalilishi tu
Wapo wanaosema bila barua nini kimeharibika?
Hoja: Bila chochote kuharibika huo sio utaratibu wa ofisi ya taasisi kubwa
Mbowe hapaswi kuongoza kwa maono yake bali kanuni za kiofisi.Hakufanya hivyo
Ipo hoja ya kwamba alishindwa kufanya nini bila kuthibitishwa?
Hoja: Bila kuthibitishwa anakosa uhalali wa nafasi, anabaki kuwa mwakilishi na hivyo kukosa authority na respect hasa ndani ya uongozi wa Bunge.
Chadema wajifunze kutofanya mambo kienyeji kutoka CUF.
Kutofuata taratibu za kiofisi na sheria za chama chao, Maalim aliamini Lipumba kaondoka kwa maneno kama Mbowe alivyomkaimisha .CUF ikashindwa kwa hoja ya maandishi
Taasisi imara na kubwa haziendeshwi kama ''mama ntilie'' anayeamua lolote.
Kwa kitendo cha Mbowe kumkaimisha mnadhimu kwa maneno bila maandishi kinawanyima ''moral authority'' ya kukemea serikali iliyomkaimisha Jaji Mkuu takribani mwaka.
Si huyu Mbowe ndiye aliyepigia upatu suala la Jaji Mkuu?
Je, kwa kukaimishwa nafasi ya Jaji mkuu nini kilikosekana au nini alishindwa kutekeleza?
Na kama hakuna Chadema walipiga kelele za nini?
Kwa Selasini kujiuzulu nakubaliana naye 100%. Ilikuwa kujidhalilisha tu.
Ilimfanya awe ''mtiifu'' na kuuza uhuru wake kwa mtu na si chama.
Selasini anavuna alichopanda, kutengeneza mfumo unaotegemea mtu na si chama.
Jambo hili lazima Chadema walipinge kwa nguvu zao zote, chama kiwe taasisi si mtu.
Kwavile Chadema inapoteza maana ya taasisi, mambo kama uchaguzi yanabaki kuwa kiini macho. Yaliyotokea ni matokeo ya mtu kujenga mtandao wake na si mtandao wa chama.
Ni makosa wanachama kuondoka katika cha hicho kwa kutoridhishwa na uongozi.
Mkono ukikamata uchafu dawa si kuukata ni kuusafisha, na hapa ndipo pa kuanzi.
Lazima wawepo watu wa kumkemea Mbowe na washirika wake hadharani.
Wanachama wadai haki ya chama chao kuongozwa kwa miongozo na kanuni na si mtu anavyojisikia.