Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ajiuzulu nafasi ya Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni

Hiyo vita ya Kikabila, hakuna logic hapo, ni Urombo vs Machame/Marangu!
Hivi wewe unaweza kuandika barua ya kujiuzulu cheo ambacho hukuwa nacho na wala hakuna aliyekuwa anakutambua kwa cheo hicho? Sasa utakuwa unajiuzulu nini? KAMA ULIKUWA HUJAOA AU KUOLEWA HALAFU UNAANDIKA TALAKA UTAMPA NANI?
 
Maswali muhimu kwa Mh Selasini.Ni karibu miaka 2 imepita .Barua yako ya KUJIUZULU ukeambatanisha na Barua ya kumkumbusha Mbowe juu ya uteuzi wako. Je hujalamba posho yeyote ile ikiwa naibu WA upinzani.
Spika alikuwa anakutaja kama kiongozi wa upinzani ,Kama uteuzi wako ulikuwa na kasoro mbona hukukanusha,hata vyombo vya habari vinca kuja Kama kiongozi WA upinzani bungeni,Ondoka mapema kabla ya uchaguzi 2020
 
..mbona hamuitaji kampuni binafsi inayolinda nyumba za viongozi area D?

..na nani alitoa maelekezo walinzi wa kampuni binafsi waondolewe siku ya tukio la kushambuliwa TL?

..Je, kuna mtu wa serikali aliwaelekeza walinzi wa kampuni binafsi kuwa Sept 7, 2017 viongozi wanaoishi area D walikuwa hawahitaji ulinzi?
Acha kutanua magoli,mtoe dereva asaidie uchunguzi kwanza
 
Sasa hapa nini cha kushangaa?
Kujiuzuru ni big story kama mnavyotaka kutuaminisha?
Kwa hiyo hata J.M akisema hatagombea 2020 kwa kuwa hakuna tume huru mtaandika this way!
Acheni utoto.
Some political parties are stronger than your efforts and you must agree that.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kumwapisha unaita mambo madogomadogo
Bro yani huna tofauti na mpiga vigelegele wa ccm.....
Ongelea perfection... kila kitu kifanyike accordingly....
walioweka utaratibu wa kuapisha nao waliona hayo ni mambo madogomadogo?

Unamtetea Mbowe hadi unajitoa ufahamu
Huenda unachosema kikawa na ukweli, lakini Selasini kamvumilia nani sana? Amevumilia sana kutokutangazwa mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani! Ni kipi anashindwa kukitekeleza akiwa mbunge, lakini angeweza kukitekeleza vizuri akitangazwa mnadhimu mkuu wa upinzani? Je chaguzi nchi hii zinanajisiwa, na hao cdm wanafanyiwa uhuni wa wazi na dola kisa ni yeye hajatangazwa mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni? Kwa hiyo katika matatizo makubwa anayokutana nayo Selasini na kumbidi aivumilie sana cdm ni hiyo kutokutangazwa nafasi ya mnadhimu? Katika matatizo ambayo wananchi wa rombo yeye kama mbunge yanashindwa kutatuliwa, ni kwakuwa hajatangazwa rasmi kuwa mnadhimu? Hapa naona unachoma tu mahindi kwa tochi.

Haya mambo madogo madogo yanaletwa na wanaccm humu jukwaani, lengo hasa ni kuonyesha cdm ina matatizo makubwa na ndio itakuwa sababu ya kushindwa uchaguzi. Kwani ule ushenzi wa juzi wa kunajisi uchaguzi wa SM za mitaa ni kwa sababu cdm kuna kutokuelewana kunakosemwa? Huo uchaguzi mkuu wa 2020 nao utanajisiwa ili ccm wajitangaze washindi, kisa Selasini amekataliwa kutangazwa mnadhimu huko bungeni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ati una majibu kule ya kwann Mbowe hajamtuibitisha 30...

Kweli Mbowe ni mtume...
Hata akikosea wako wanaomtetea.

Sent using Jamii Forums mobile app

Katika watu ambao utetezi wangu ni mwiko kuupata ni huyo Mbowe, na sina popote ninapounga mkono alichofanyiwa huyo 30, lakini huyo 30 sio lolote sio chochote wa kusema eti naye atatishia. Kama hajadhibitishwa apige kimya maana hanaga mchango wowote useme unamashiko ndani ya chama. Analilia madaraka makubwa wakati hata hayo ya msingi hana impact yoyote? Angekuwa amevuliwa ubunge afadhali, sio cheo kisicho na maana yoyote kwa ujenzi wa chama.
 
Acha kutanua magoli,mtoe dereva asaidie uchunguzi kwanza

..kwa maoni yangu, aliyetoa maagizo ulinzi usiwepo Area D ni mtu muhimu sana kwa wachunguzi wa ugaidi ule.

..ningekuwa na mamlaka ningemkamata na kumfungulia mashtaka ya kutakatisha fedha huku uchunguzi ukiendelea.
 
boss achana na personality ma personal values..
1.Kutotuibitishwa ni kosa ... period.
2. Kulalamika ama kujitoa ni wajibu wake kwakuwa haoni sababu ya kutothibitishwa.
3. Mbowe amekosea.

Mengine hayana umuhimu yanakupotezea heshima kaka
Katika watu ambao utetezi wangu ni mwiko kuupata ni huyo Mbowe, na sina popote ninapounga mkono alichofanyiwa huyo 30, lakini huyo 30 sio lolote sio chochote wa kusema eti naye atatishia. Kama hajadhibitishwa apige kimya maana hanaga mchango wowote useme unamashiko ndani ya chama. Analilia madaraka makubwa wakati hata hayo ya msingi hana impact yoyote? Angekuwa amevuliwa ubunge afadhali, sio cheo kisicho na maana yoyote kwa ujenzi wa chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
boss achana na personality ma personal values..
1.Kutotuibitishwa ni kosa ... period.
2. Kulalamika ama kujitoa ni wajibu wake kwakuwa haoni sababu ya kutothibitishwa.
3. Mbowe amekosea.

Mengine hayana umuhimu yanakupotezea heshima kaka


Sent using Jamii Forums mobile app

Ni hivi, hana mchango wowote wa maana ndio maana kapotezewa. Ni kweli Mbowe alikosea, lakini kwakuwa hajadhibitishwa na ameamua kujiuzulu ni sawa, ni bora nafasi yake apewe mtu mwenye tija.
 
Huyu jamaa hakuwa kweli kwenye lile kundi la 'Mbowe must go'? Naona mambo yamekuwa magumu, mwamba karudi sasa ni bora kujihami mapemaaaa.
 
hapo unamtukana aliyemchagua ndio mjinga kuchagua asiye na mchango wowote... Ila Nabii Mbowe tusimlaumu.

Kama mwaka mzima hakukuwa na substitute maana yake chadema wenye akili kidogo ni Mbowe na Lissu...

To make it easy kubali tu kuwa Mbowe alikosea kumchagua ama kutomthibitisha.

Najua wewe sio chadema sana
Ni hivi, hana mchango wowote wa maana ndio maana kapotezewa. Ni kweli Mbowe alikosea, lakini kwakuwa hajadhibitishwa na ameamua kujiuzulu ni sawa, ni bora nafasi yake apewe mtu mwenye tija.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu JokaKuu
Barua ya Mbunge Selasini ina mambo haya
Kwamba,aliteuliwa na Mbowe baada ya tukio la TL kukaimu nafasi
- Hakuna barua rasmi iliyotolewa, yalikuwa ni maneno ya uteuzi.
-Hajapewa onyo la mdomo au maandishi kuhusu utendaji wake
-Amehudhuria vikao vya Bunge vya kamati za uongozi

Hoja: Mbowe alipaswa kumkaimisha nafasi hiyo kwa maandishi ili kuweka kumbu kumbu za kiofisi leo na kesho. Hakuna ajuaye nini kitatokea, hilo ni la muhimu ndani ya taasisi.

Pili, kuujulisha uongozi wa Bunge ili Selasini atambuliwe kama na si mwakalilishi tu

Wapo wanaosema bila barua nini kimeharibika?
Hoja: Bila chochote kuharibika huo sio utaratibu wa ofisi ya taasisi kubwa

Mbowe hapaswi kuongoza kwa maono yake bali kanuni za kiofisi.Hakufanya hivyo

Ipo hoja ya kwamba alishindwa kufanya nini bila kuthibitishwa?

Hoja: Bila kuthibitishwa anakosa uhalali wa nafasi, anabaki kuwa mwakilishi na hivyo kukosa authority na respect hasa ndani ya uongozi wa Bunge.

Chadema wajifunze kutofanya mambo kienyeji kutoka CUF.

Kutofuata taratibu za kiofisi na sheria za chama chao, Maalim aliamini Lipumba kaondoka kwa maneno kama Mbowe alivyomkaimisha .CUF ikashindwa kwa hoja ya maandishi

Taasisi imara na kubwa haziendeshwi kama ''mama ntilie'' anayeamua lolote.

Kwa kitendo cha Mbowe kumkaimisha mnadhimu kwa maneno bila maandishi kinawanyima ''moral authority'' ya kukemea serikali iliyomkaimisha Jaji Mkuu takribani mwaka.

Si huyu Mbowe ndiye aliyepigia upatu suala la Jaji Mkuu?
Je, kwa kukaimishwa nafasi ya Jaji mkuu nini kilikosekana au nini alishindwa kutekeleza?

Na kama hakuna Chadema walipiga kelele za nini?

Kwa Selasini kujiuzulu nakubaliana naye 100%. Ilikuwa kujidhalilisha tu.
Ilimfanya awe ''mtiifu'' na kuuza uhuru wake kwa mtu na si chama.

Selasini anavuna alichopanda, kutengeneza mfumo unaotegemea mtu na si chama.

Jambo hili lazima Chadema walipinge kwa nguvu zao zote, chama kiwe taasisi si mtu.

Kwavile Chadema inapoteza maana ya taasisi, mambo kama uchaguzi yanabaki kuwa kiini macho. Yaliyotokea ni matokeo ya mtu kujenga mtandao wake na si mtandao wa chama.

Ni makosa wanachama kuondoka katika cha hicho kwa kutoridhishwa na uongozi.

Mkono ukikamata uchafu dawa si kuukata ni kuusafisha, na hapa ndipo pa kuanzi.

Lazima wawepo watu wa kumkemea Mbowe na washirika wake hadharani.

Wanachama wadai haki ya chama chao kuongozwa kwa miongozo na kanuni na si mtu anavyojisikia.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom