Mbunge wa Nkenge, Asumpta Mshama lazima ung'oke 2015!

Nashangaa kuona mkoa wa Kagera wenye historia ndefu wa wasomi waliobobea katika sekta mbalimbali bado wanaendelea kuikumbatia CCM, CCM híi ya leo ambayo ndio imekuwa JANGA LA TAIFA wameua bei ya kahawa miwa na vyama vya Ushirika kufa, viwanda kufa na kilichobaki kwa mwananchi ni Ardhi ambayo pia kwa sasa tumeanza kudhulumiwa kwa kile kinachoitwa uwekezaji haya bado kidogo raia tuanze kuuzwa Manamba
 
Napenda kitu kimoja tu kutoka kwa huyu mama,ni wale mabinti zake wanaoimba Gospel wakijulikana kam,a J-Sisters,vingine ni upuuzi mtupu!
 
Mie kipekee siridhishwi na utendaji kazi wake na just put her get her facts right kunae mtu anajiandaa vilivyo kwa harakati za ndani ya chama na akija kupata ridhaa basi ajue jamaa anakuja kwa kasi ya moto wa gesi!nae hatakua na nafasi tena

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Padri wa Parokia ya Kanyigo Medelicus Kyaruzi amewataka waumini wa eneo lake kumsusia Mbunge wao Ansupter Mshama mpaka atakapolipa vitu alivyochukua kwa mkopo kwenye mnada wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa na kutoa ahadi la shilingi milioni mbili tangu mwezi March na kuweka mgomo wa kuvilipa.

Ameyasema jana wakati wa Misa ya Jumapili.Padri alidai suala hilo lilifikishwa CCM Wilaya na Mkoa na Mbunge ameendelea kuweka mgomo wa kulipa deni.

Chanzo.Radio Karagwe
 
Mkuu mleta mada kwa hiyo unataka kutwambia kwamba Mhe shimiwa alijipatia mali kwanjia ya Udanganyifu .Hapo wa mkamate tu arudishe vitu alivyochukua na liwe fundisho kwa viongozi wadini wenye tabia ya kutumia viongozi wa kisiasa kama ATM na kuchafua hadhi ya Kanisa.

Mungu si masikini kiasi hicho wasipende kuombaomba wajikamue na kupiga kazi kwa kutumia kile walichonacho na Mungu atawaongezea .Hii kupenda miteremko ndo inawagharimu
 
Hivi hawa wabunge wanawake wa CCM mbona wameanza kujidharirisha hivi wamekumbwa na nini? juzi tu tumesikia mwingine kamtamani mwanae mpaka kafunga naye ndoa,mbona mnachafuka na mshakuwa vibibi hivyo hekima mmepeleka wapi?
 
hilo ni jimbo la uchaguzi la nkenge,m4c faster peleka wavunaji ili 2015 tukakomboe jimbo.
 
CCM bwana .Yaani kila kukicha wanaiba sirini na kuchukua kwa nguvu watu wanaona .Kwani alilazimishwa kuchukua viti hivyo ?Hadi kanisani ?
 
Hivi hawa wabunge wanawake wa CCM mbona wameanza kujidharirisha hivi wamekumbwa na nini? juzi tu tumesikia mwingine kamtamani mwanae mpaka kafunga naye ndoa,mbona mnachafuka na mshakuwa vibibi hivyo hekima mmepeleka wapi?

Mmemsahau mama Tibaijuka aliyeanza kumwaga ubwabwa Muleba ili kuhamasisha mahudhurio ya mikutano yake ya kisiasa, afadhari angepeleka chakula hicho shuleni kuhamasisha mahudhurio ya watoto wanaotoka katika familia zilizoathirika na ukosefu wa chakula kutokana na ugonjwa wa mnyauko wa migomba
 
Daaah,yani nilikuwa najiuliza hivi ni kwanini mapadri wanamwagiwa tindikali na wengine wanapigwa risasi sikuwa na napata majibu! lakini kwa huyo padri anachokifanya ni dhahiri kuwa anatumiwa kisiasa,yani padri mzima badala ya kumtumikia Mungu anakubali kutumia madhabahu ya Mungu kuchafua watu kwa maneno ya uongo,sijui amelipwa sh. ngapi?Eti asipigiwe kura!!!!!!!!Wampigie nani sasa???? Ana mpango wa kuacha altare na kugombea ubunge? Kweli mwisho umefika......unafiki,chuki kila kona hata kwa mapadri
 
Mkuu mleta mada kwa hiyo unataka kutwambia kwamba Mhe shimiwa alijipatia mali kwanjia ya Udanganyifu .Hapo wa mkamate tu arudishe vitu alivyochukua na liwe fundisho kwa viongozi wadini wenye tabia ya kutumia viongozi wa kisiasa kama ATM na kuchafua hadhi ya Kanisa.

Mungu si masikini kiasi hicho wasipende kuombaomba wajikamue na kupiga kazi kwa kutumia kile walichonacho na Mungu atawaongezea .Hii kupenda miteremko ndo inawagharimu

Mi naona sasa tunakoenda siko. Jamani mbona huyo mbunge mwenyewe hakuwepo siku ya tukio la harambee!!!! Alituma mtu na huyo kijana alishapewa michango akalipe. Huyu padri nina wasiwasi naye pia pengine anatumiwa na watu kumchafua huyo mama. Maana hata kama mbunge angekuwa hajachangia, si amtafute kuliko kuja kwenye hadhara!!! Hii ina kitu ndani yake, sio bure... Tumuogope MUNGU na tusitumie makanisa vibaya. Mapadri waeneze injili na siyo fitina na wanasiasa. Hizo fitina sio dhumuni la kuanzisha kanisa.... Kanisa ni kwa ajili ya kuhubiri..
 
Mi nadhani taifa linaelekea kubaya, na awa viongozi wetu wa dini ndo watakua wa kwanza kuliangamiza. Kama tunaisahau kazi ya Mungu na kuamua kuwatumikia wanasiasa tunamkosea sana Mungu. Mama Asumpter namfahamu sana na sisi tulomchagua tunamwamini na tutaendelea kumwamini, maana kamwe hawezi kufanya ayo mnayomtuhumu nayo. na kama kweli Mama kashindwa kutimiza ahadi iyo, basi sisi vijana wake tupo tiari kumchangia na kulipa.

wasiwasi wangu ni kwamba, hivi wale wote wanaoshindwa kutimiza ahadi wanatangazwa wakataliwe na kanisa au padre ana yake......
 
Alipe deni la kanisa sio vizuri wanasiasa wanavyofanya kipindi cha uchaguzi wana ahidi mambo mengi wakishashinda wanaanza kuyayuka
 
Padri wa Parokia ya Kanyigo Medelicus Kyaruzi amewataka waumini wa eneo lake kumsusia Mbunge wao Ansupter Mshama mpaka atakapolipa vitu alivyochukua kwa mkopo kwenye mnada wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa na kutoa ahadi la shilingi milioni mbili tangu mwezi March na kuweka mgomo wa kuvilipa.

Ameyasema jana wakati wa Misa ya Jumapili.Padri alidai suala hilo lilifikishwa CCM Wilaya na Mkoa na Mbunge ameendelea kuweka mgomo wa kulipa deni.

Chanzo.Radio Karagwe

Mmh sijashangazwa sana na hii taarifa maana kwa jinsi mambo yanavyokwenda jimbo la Nkenge, watu wana ha ha, joto na presha juu kuelekea uchaguzi 2015,tuangalie tu jamani tusije kutoana roho maana kama padri anakuwa na ujasiri wa kumchafua mtumishi mwenzake kwa maslahi binafsi,tusije kuona makubwa zaidi ya hayo!
 
Mi naona sasa tunakoenda siko. Jamani mbona huyo mbunge mwenyewe hakuwepo siku ya tukio la harambee!!!! Alituma mtu na huyo kijana alishapewa michango akalipe. Huyu padri nina wasiwasi naye pia pengine anatumiwa na watu kumchafua huyo mama. Maana hata kama mbunge angekuwa hajachangia, si amtafute kuliko kuja kwenye hadhara!!! Hii ina kitu ndani yake, sio bure... Tumuogope MUNGU na tusitumie makanisa vibaya. Mapadri waeneze injili na siyo fitina na wanasiasa. Hizo fitina sio dhumuni la kuanzisha kanisa.... Kanisa ni kwa ajili ya kuhubiri..

Mkuu kama unaijua issue basi funguka au mwambie mbunge kwamba huku watu wanachafua anyooshe maelezo labda huyo aliyetumwa hakufikisha ujumbve na alichukua baadhi ya vitu kwenye mnada kwa jina la Mbunge bila Mbunge kuwa na taarifa
 
Katika kipindi chote cha miaka 4,aliyo kaa bungeni hakuna alichokifanya kuwatetea wapiga kura wake wa jimbo la nkenge zaidi ya kutukana viongozi wa upinzani bungeni,wananchi wa kiziba wamedhamilia kutomchagua huyu mama,naye analijua hilo.
 
Akiwa ni miongoni mwa wabunge wa CCM waliopita bila kupingwa, mbunge huyu amekua kama mtalii katika bunge letu mjini Dodoma.
Aliyekua mgombea wa ubunge kupitia CDM maarufu kwa jina la " Focus" alijitoa dakika za mwisho na kumfanya mama huyu kupita bila kupingwa. Lakini cha ajabu huyu mama hajawai kuisimamia serikali kutokana na ahadi alizozitoa mh Rais ikiwamo kuunganishwa kwa jimbo la Ngenge katika gridi ya taifa.
Sasa basi sisi kama vijana tunakuahidi mh Mbunge kwamba hautorudi mjengoni tena baada ya 2015!
TUMECHOKA
kwani kakwambia atagombea tena?
pili huyu pichani unampa ushauri gani kuhusu kugombea ubunge 2015?

IMG_9913.JPG
 
Daaah,yani nilikuwa najiuliza hivi ni kwanini mapadri wanamwagiwa tindikali na wengine wanapigwa risasi sikuwa na napata majibu! lakini kwa huyo padri anachokifanya ni dhahiri kuwa anatumiwa kisiasa,yani padri mzima badala ya kumtumikia Mungu anakubali kutumia madhabahu ya Mungu kuchafua watu kwa maneno ya uongo,sijui amelipwa sh. ngapi?Eti asipigiwe kura!!!!!!!!Wampigie nani sasa???? Ana mpango wa kuacha altare na kugombea ubunge? Kweli mwisho umefika......unafiki,chuki kila kona hata kwa mapadri

unatokwa povu kutetea nini? Huyo mbunge tapeli anayetapeli hadi kanisani? Utakuwa na tatizo la ubongo wewe!
 
Mi naona sasa tunakoenda siko. Jamani mbona huyo mbunge mwenyewe hakuwepo siku ya tukio la harambee!!!! Alituma mtu na huyo kijana alishapewa michango akalipe. Huyu padri nina wasiwasi naye pia pengine anatumiwa na watu kumchafua huyo mama. Maana hata kama mbunge angekuwa hajachangia, si amtafute kuliko kuja kwenye hadhara!!! Hii ina kitu ndani yake, sio bure... Tumuogope MUNGU na tusitumie makanisa vibaya. Mapadri waeneze injili na siyo fitina na wanasiasa. Hizo fitina sio dhumuni la kuanzisha kanisa.... Kanisa ni kwa ajili ya kuhubiri..

umeambiwa kuwa wameshafika ofis za ccm wilaya na mkoa bila mafanikio yoyote,wewe ulitaka wafanye nini? Kwa vile Mmezoea kuishi kwa uongo ulitaka wampambe kwa nyimbo na mapambio!? Nyaambaafffu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom