Mbunge wa Nkenge, Asumpta Mshama lazima ung'oke 2015!

Mbunge wa Nkenge, Asumpta Mshama lazima ung'oke 2015!

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
Akiwa ni miongoni mwa wabunge wa CCM waliopita bila kupingwa, mbunge huyu amekuwa kama mtalii katika bunge letu mjini Dodoma.

Aliyekuwa mgombea wa ubunge kupitia CHADEMA maarufu kwa jina la " Focus" alijitoa dakika za mwisho na kumfanya mama huyu kupita bila kupingwa.

Lakini cha ajabu huyu mama hajawahi kuisimamia serikali kutokana na ahadi alizozitoa mh Rais ikiwamo kuunganishwa kwa jimbo la Ngenge katika gridi ya taifa.

Sasa basi sisi kama vijana tunakuahidi mh Mbunge kwamba hautorudi mjengoni tena baada ya 2015!

TUMECHOKA
 
Wanaotakiwa kung'oka sio huyo mama tu ni wabunge wote wa kipande ile nyingine karibia wote
 
Huyo Focus kwa nini alijitoa dakika za mwisho?? Fikiria, chukua hatua!!!

nadhani alihongwa hela nyingi sana au alihaidiwa something profitable, kuna kitu alishawishiwa. hilo jimbo lingeenda CHADEMA lakini huyu jamaa alituangusha
 
Huyu mama namjua. Kwa kweli upeo wake uko chini sana. Hata CCM walimuweka kumkomoa Kamala, sijui Kamala aliwaudhi nini mpaka baadhi yao wakaapa kwamba harudi bungeni.

Kwa kweli Assumpta ni kimeo! Yatosha tu kusema ni kimeo basi. Mimi sio msemaji hivyo nakosa hata jinsi ya kumuelezea!
 
nadhani alihongwa hela nyingi sana au alihaidiwa something profitable, kuna kitu alishawishiwa. hilo jimbo lingeenda CHADEMA lakini huyu jamaa alituangusha
Bora huyu mama alishinda, maana angeshinda huyo ''Focus'' angeiyumbisha sana CHADEMA.
Anakubali vipi kuhongwa na CCM halafu hapo hapo unataka sisi wananchi tumwamini?
 
'vijana' mnaotaka kumuondoa asumpta mko wangapi? Usikute mpo hamsini....nusu hawajajiandikisha na nusu ya waliojiandikisha majina yao hayatoonekana siku ya kupiga kura.....hivyo mbunge atapita kama analia vile taratiiiiiiibu
 
'vijana' mnaotaka kumuondoa asumpta mko wangapi? Usikute mpo hamsini....nusu hawajajiandikisha na nusu ya waliojiandikisha majina yao hayatoonekana siku ya kupiga kura.....hivyo mbunge atapita kama analia vile taratiiiiiiibu

omba uzima na ujionee mwenyewe yatakayomkuta 2015
 
msifanye makosa tena! peni kura kwa wingi,lindeni kula zenu,na na huyo alie hongwa pigeni mawe! hakiki sheni mna chagua mtu sahihi kutoka M4C!
 
Nkenge ndo nyumbani kwetu. Nilikuwepo juzi christmas kweli mama kachokwa. Lakini kilichonisikitisha zaidi ni jinsi Kagera yetu inavyozidi kudidimia. Si mjini wala vijijini aisee Uhayani tumechoka. Watu wako hoi na nadhani ni kuendekeza sana UCCM ndo maana tunaporomoka sana.
 
Akiwa ni miongoni mwa wabunge wa CCM waliopita bila kupingwa, mbunge huyu amekua kama mtalii katika bunge letu mjini Dodoma.
Aliyekua mgombea wa ubunge kupitia CDM maarufu kwa jina la " Focus" alijitoa dakika za mwisho na kumfanya mama huyu kupita bila kupingwa. Lakini cha ajabu huyu mama hajawai kuisimamia serikali kutokana na ahadi alizozitoa mh Rais ikiwamo kuunganishwa kwa jimbo la Ngenge katika gridi ya taifa.
Sasa basi sisi kama vijana tunakuahidi mh Mbunge kwamba hautorudi mjengoni tena baada ya 2015!
TUMECHOKA
Huyu mama nimewai muona kama mara mbili hivi akichangia bungeni cha kwanza huwa anatoa lawama kwa wapinzani na pili huwa anaunga mkono hoja na kuwashukuru wananchi wa Nkenge kwa kutochagua upinzani.
Baada ya uchaguzi katika kipindi cha jambo kinachorushwa na TBC asubuhi alikuwa akihojiwa yeye na mbunge wa Mbozi Magharibi David Silinde(CHADEMA)
alisema hakuna Mtanzania anayeshindwa kunywa chai na kama yupo ni mvivu, kipindi hicho sukari ilikua haipatikani na bei ilikuwa juu sana.
 
yetu macho 2015.
haya ndugu zetu kina iwe kazi kwenu kuchagua mwanga au giza 2015. ukiangalia takwimu utaona jinsi mkoa unavyodidimia kwa kasi ya ajabu katika umaskini. Wahaya wa siku hizi ni tofauti na wazamani. Wahaya wa siku hizi wanakubali kudidimia katika dimbwi la umaskini.

Wakati wahaya wa zamani walijitahidi kukumbuka nyumbani na kupeleka maendeleo lakni wa siku hizi wamebaki kuwa mabishororo mjini. kibaya zaidi na baadhi ya wahaya waliopo vijijini wamepumzisha akili zao, wamekuwa wavivu na kupeleka akili zao likizo na kusubiri wakati wa uchaguzi ili kuchumia tumbo kwa kuhongwa vitu vidogo vidogo bila kuangalia athari zake.
pole sana ndugu zangu, ila 2015 chukua hatua
 
Mimi nashangaa sana watanzania wenzangu kuwachagua wabunge aina ya asumta,sijui ni upeo wetu mdogo,ushabika wa kisiasa,rushwa au nini? Watanzania wenzangu tujue kura zetu zina thamani kubwa, tujipange 2015 tuchague viongozi wenye uzalendo wa kweli bila kujali chama.
 
Mhudum wa ndege tu ya rais then ubunge unafikilia atafanya nini hapo? hana haraka zozote za ugumu wa life.

Kanda ya ziwa magharibi yote ni lazima CDM isimame 2015.
 
ndio maana tunapenda kupitapita humu mara kwa mara,eeeh umesema alikuwa mhudumu wa fastjet? kwa style hizi tutahitaji sana kujua historia za wabunge wetu mali wanazomiliki kabla ya ubunge na baada ya ubunge
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom