Mbunge wa Ngara: Vijana wengi waliomaliza chuo hawataki kulima wala kushika kinyesi cha Wanyama (mbolea)

Yeye anashika hicho kinyesi au anapiga meza Dodoma huko bila hata kuchangia na anapata 300k kwa siku?
 
Mambo mengine yanashangaza sana na kustaajabisha. Yaani leo ndo wanashangaa SUA kufundisha ualimu! Tuliyasema kwa mfano kwamba vyuo vya ufundi viendelee kuwepo na kutoa mafundi mchundo "technicians" ambao ni maalum kwa kuunda vifaa mbalimbali vya kiufundi.

Badala yake karibu vyuo vyote vya ufundi sasa vinatoa shahada na matokeo yake tuna idadi kubwa sana ya wenye shahada kulinganisha na fundi mchundo.

Walitaka pia kubadili Chuo cha MADINI Ile kiwe kinatoa shahada lakini kwa umakini wa Waziri aliyekuwepo hili halikutokea. Kwa nchi za wenzetu katika kila mhitimu mmoja mwenye shahada, kuna fundi mchundo wanne, hapa petu ni shahada kwa wingi.

Vyuo vya Mipango sasa karibu vyote vinatoa shahada za namna mbalimbali. Tumelikoroga hatuna budi kulinywa hivyo hivyo lilivyo.
 
sokoine mdogo mdogo inaanza kupoteza uhalisia wake, koz walizozpachka sijui ualimu.baada ya kuondoka mwal nyerere watoto wamejisahau,Mambo mengi yamepinduliwa kabisa.
SUA hawakuwa tayari kuanzisha kozi za Ualimu,ila kipindi cha JK walilazimisha kila chuo kiwe na kozi za Ualimu. Basi wakakubali kuanzisha ila kwa shingo upande.
 
Impact ya SUA kwa nchi hii ni sawa na bure kabisa.
Mwenye akili finyu anaweza dhani SUA haina mchango wowote katika nchi hii, ila mwenye akili timamu ya kujiongeza anajua mchango mkubwa wa chuo cha Sokoine katika maendeleo ya nchi hii. Tatizo kubwa ni serikali kukwepa wajibu wake wa kuwasaidia wahitimu hasa kwa kuwasaidia mitaji,ardhi na masoko.Nchi zingine duniani kote hufanya hivyo. La sivyo tutaendelea kutoona tija ya wasomi wetu.
 
Mimi nahisi serikali ndio haijui jinsi ya kutumia Elimu/harness elimu wanayopata/itolewayo kwa vijana wanaofika vyuoni,..vijana wanakuja na energy/drive, ambitions na creativity.....kinachoonekana ni serikali kuwa transform wasaidie society kupitia Elimu, sasa unasema mtu hawezi kushika mbolea, je mbolea ndio challenge tunayo face wananchi???..na sio may be mwana ugavi wa mambo ya kilimo??,au afisa masoko ???..................ni mpaka hapo tutakapojua kuitumia Elimu especially vyuoni ku benefit Tanzanians ndipo tutasonga mbele kama taifa..hizi statement ziko general sana na hazisaidii...
 
Iwapo inawezekana kula na kunywa bila kugusa kinywaji au chakula, Je ni lazima mkulima ashike kinyesi au mbolea kwa mikono?

Kilimo hakijapewa sifa au heshima yake.
Fuatilia ushuru wa mazao sokoni.

Pumba za mpunga ambazo kwa uhalisi ni takataka zinatozwa ushuru wa kati ya sh.500/= hadi 1,000/= kwa kila gunia.

Hivi hatuna vyanzo vya mapato hadi tunatoza ushuru takataka?

Wapeni fursa/nafuu wakulima ili wazalishe kwa gharama nafuu.

Fuatilia bei za mbegu za mazao mbali mbali.
Zipo juu sana licha ya kutokuwapo maelekezo ya namna ya kuzipata na kuzitumia.

Iwapo hakutachukuliwa hatua madhubuti za kukipa hadhi kilimo, vijana hawatajiingiza kwenye mradi huu wa "kukata mtaji" na "kula muda" wa vijana.

Kilimo kitaendelea kuendeshwa na wazee au watu ambao hatuna "namna" au "uchaguzi" wa jambo la kufanya.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom