Wagogo watakuwa wa mwisho kufanya maamuzi magumu ya kuiacha ccm.
Mzee Malecela ana heshima zake, amelifanyia mengi taifa hili ikiwa ni pamoja na wana Mtera, lakini uamuzi wake wa kutaka kuendelea kuwa Mbunge wa Mtera sikuunga mkono tangu mwanzo. Hivyo hata alivyoangushwa sikusikitika, alipaswa kupunzika kama alivyo sasa. Anapata heshima zaidi sasa kuliko hata alipokuwa katika boti ya malumbano na vijana. Hakuna jipya ambalo angelifanyia jimbo hilo ambalo kwa miaka mingi aliyokuwa madarakani hakuweza kufanya.
Kwa kifupi Mbunge hahitaji miaka kuonesha uchapakazi au ubabaishaji. Sasa kila mmoja anaweza kusema kwa uwazi ni Mbunge yupi ambaye njia yake ipo wazi kuendelea 2015, na ni yupi kuna walakini, na ni yupi hakuna kitu, aachie ngazi tu, ingawa bado kuna miaka mitatu ya kuweza kurekebisha kitu.
Lakini pia tukirudi Mtera huyo kibajaj Lusinde sio chaguo sahihi ya kuleta mageuzi ya kifikra na kimaendeleo katika jimbo la Mtera. Wanamtera wakitaka kupiga hatua wafanye maamuzi ya magumu ya kumweka mgombea wa chama makini - Chadema, na wawe na nia thabiti ya kutaka mabadiliko.
Vinginevyo waendelee kuvaa kofia na khanga za ccm kila mwaka wa uchaguzi, na baadaye waendelee kwenye mateso miaka minne.