Mbunge wa Mtera ndg Lusinde ashutumiwa kumchafua mzee Malecela.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge wa Mtera ndg Lusinde ashutumiwa kumchafua mzee Malecela....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Feb 19, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ....Yule mbunge wa Mtera ndg Lusinde aka Kibajaji ameendelea kushutumiwa kukigawa chama cha mapinduzi jimboni kwake Mtera.Taarifa zinasema kuna kundi kubwa la wanachama wa CCM ambao wameanza kusikitika kwanini walimuunga mkono huyu ndugu Kibajaji...

  Kundi kubwa linalomuunga mkono Lusinde limesema kuwa Ndg Kibajaji amegombana na baadhi ya madiwani wa chama chake na ameendelea kutamba kuwa alimnunua mgombea wa CDM ndg Lameck.L..

  Mbaya zaidi wanachama wa chama cha mapinduzi wameendelea kudai kuwa Ndg Kibajaji anatumia muda Mungu kumchafua Mzee Malecela maana anaonekana kama bado ni kikwazo kwa utawala wake na hasa uchaguzi wa 2015...

  Alipoulizwa Lusinde alijibu yeye hana ugomvi na mtu yoyote maana wote ni ndugu zake.Lakini alitoa mpya kwa kusema kuwa hawezi kwenda kuomba ushauri wala kuiga namna ya kuongoza jimbo kwa watu aliowashinda,hapa akimaanisha hawezi kwenda kuomba ushauri kwa mtu kama Mzee Malecela wakati alimbwaga kwenye uchaguzi.

  ....Huyu ndiye Mbunge wa Mtera ndg Lusinde aka Kibajaji,wana Mtera wanajutia maamuzi yao waliyoyafanya bila kutafakari.

  Source : Mwananchi
   
 2. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa kifupi, Lusinde ni Janga la Taifa!
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Mi niliwashangaa sana wagogo walivyoamua kumtosa huyo dingi. Imekula kwao hapo!
   
 4. D

  Dopas JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wagogo watakuwa wa mwisho kufanya maamuzi magumu ya kuiacha ccm.

  Mzee Malecela ana heshima zake, amelifanyia mengi taifa hili ikiwa ni pamoja na wana Mtera, lakini uamuzi wake wa kutaka kuendelea kuwa Mbunge wa Mtera sikuunga mkono tangu mwanzo. Hivyo hata alivyoangushwa sikusikitika, alipaswa kupunzika kama alivyo sasa. Anapata heshima zaidi sasa kuliko hata alipokuwa katika boti ya malumbano na vijana. Hakuna jipya ambalo angelifanyia jimbo hilo ambalo kwa miaka mingi aliyokuwa madarakani hakuweza kufanya.

  Kwa kifupi Mbunge hahitaji miaka kuonesha uchapakazi au ubabaishaji. Sasa kila mmoja anaweza kusema kwa uwazi ni Mbunge yupi ambaye njia yake ipo wazi kuendelea 2015, na ni yupi kuna walakini, na ni yupi hakuna kitu, aachie ngazi tu, ingawa bado kuna miaka mitatu ya kuweza kurekebisha kitu.

  Lakini pia tukirudi Mtera huyo kibajaj Lusinde sio chaguo sahihi ya kuleta mageuzi ya kifikra na kimaendeleo katika jimbo la Mtera. Wanamtera wakitaka kupiga hatua wafanye maamuzi ya magumu ya kumweka mgombea wa chama makini - Chadema, na wawe na nia thabiti ya kutaka mabadiliko.

  Vinginevyo waendelee kuvaa kofia na khanga za ccm kila mwaka wa uchaguzi, na baadaye waendelee kwenye mateso miaka minne.
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,892
  Trophy Points: 280
  kijana wa tingatinga yupo huko jimboni kuchukua maoni, naamini watakutana 2015.
   
 6. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Mutuuuuz le baharia anakuja kivingine..lusinde ukiweza piga mtu na babake hamna ufalme bongo.
   
 7. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Lusinde ni janga hata hivyo hiyo ni ishara kwamba wananchi wakikuchoka wanafanya maamuzi ya hasira na chuki bila kuangalia kama unao uwezo wa kuongoza ama la. Haya ndiyo yalimkuta mzee Malecela.
   
 8. k

  kuzou JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  angekua mbunge wa cdm si walimwomba ccm 2005 ampishe babu kiundugu.je mngemponda hivi kama angekua cdm
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Siasa chafu zitokanazo na itikadi mbaya ya chama kilichoratibiwa na siasa za majungu, chuki na unafiki.... uzao wa dhuluma na kutoaminiana
   
 10. l

  le comparable Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Simlaumu sana lusinde kwa anayoyafanya coz tatizo sio yeye but ni level ya elimu aliyonayoa.nadhani sasa umefika wakati muafaka wa kuweka minimum educational level kwa mtu anayetaka kugombea ubunge kua angalau form four au six,karne ya 21 bado tunaendekeza wabunge wa darasa la saba hatuwez pga hatua as hata uwezo wao wa hoja ni mdogo sana na at last watu tunapoteza muda mwingi kuwajadili kutona na madudu wanayoyafanya,
   
 11. t

  tenende JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kijana wa CDM anayejiandaa kupambana na huyu Zyapunga - Atoe taarifa mapema tumpe kampani. Tueneze harakati na kummaliza kabla ya 2015. Huyu jamaa hafai. Sikiliza michango yake Bungeni haina hata chembe ya utaifa!.. Busara hana, ni mropokaji, mgomvi, asiyependa suluhu! Hafai ni Sumu!.. Wabunge wa namna hii tuanzishe harakati za kuwang'oa majimboni kwao ili 2015 wasiwe na ubavu!
   
 12. only83

  only83 JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Yule nae ni janga tu,sioni tofauti kati yake yeye na kibajaji....
   
Loading...