Mbunge wa Moshi vijijini aibia Wananchi Milioni (240)

Mbunge wa Moshi vijijini aibia Wananchi Milioni (240)

Alvin Slain

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
6,375
Reaction score
3,665
Mbunge wa Moshi vijijini amewaibia wananchi wa jimbo hilo takribani milioni (240),zikiwa ni fedha za maendeleo ya jimbo zinazotolewa na mfuko wa jimbo kila mwaka kwa miaka (8).

Aidha mbunge Cyril Chami amesitisha kuwatembelea wananchi wake huku akipokea fedha za kuwatembelea wananchi wa jimbo hilo ambazo ni takribani milioni (2,880,000)

Inasikitisha ubadhirifu wa fedha za umma kumilikishwa mtu mmoja kama mfalme hali inayochangia maendeleo kuwa hafifu,

Ni matumaini yangu Mbunge chami atatoa maelezo fedha za walipa kodi zimekwenda wapi??

Ni wakati umefika wananchi tuache kuambiwa tu bali tufanye uchunguzi wa fedha zetu.

Wananchi wengi wa eneo hili ni watu/raia wema wenye mitizamo ya kutarajia maendeleo.

Licha ya wananchi wa jimbo hili kuwa 99% ni wakulima,kilimo hiki hakiwalipi ujira.

Hii ndio sababu watu wenye mashamba ya kahawa wameyasahau kwa sababu,
Kahawa imekua ni soko la kisiasa, Mbunge Cyrili alipopata ridhaa ya wananchi aliahidi mengi kuyatekeleza ikiwa ni pamoja na kumaliza tatizo la maji baadhi ya maeneo ya jimbo hili,
Cha kushangaza huu mwaka wa 8 hakuna chochote kilichpfanyika zaidi ya kituo cha polisi ambacho wananchi walijichanga ili kufanikisha, Hiki kituo cha polisi kiko kata ya okaoni,kituo ambacho kinadaiwa kutumia takribani milioni (500) za kitanzani,
Na kuna deni ambalo wananchi watahitajika kulipa.
 
Mbunge wa Moshi vijijini amewaibia wananchi wa jimbo hilo takribani milioni (240),zikiwa ni fedha za maendeleo ya jimbo zinazotolewa na mfuko wa jimbo kila mwaka kwa miaka (8).

Aidha mbunge Cyril Chami amesitisha kuwatembelea wananchi wake huku akipokea fedha za kuwatembelea wananchi wa jimbo hilo ambazo ni takribani milioni (2,880,000)

Inasikitisha ubadhirifu wa fedha za umma kumilikishwa mtu mmoja kama mfalme hali inayochangia maendeleo kuwa hafifu,

Ni matumaini yangu Mbunge chami atatoa maelezo fedha za walipa kodi zimekwenda wapi??

Ni wakati umefika wananchi tuache kuambiwa tu bali tufanye uchunguzi wa fedha zetu.
@cc

Huyo ni mwizi hana huruma na wananchi wa jimbo lake. Nenda kata za old moshi magharibi tella mande sehemu za weruweru chini uone wanavyotaabika kuhusu maji. Nenda kibosho yote kindi kirima nenda uru sango mbokomu sehemu za mabogini ujionee kulivyo na shda ya maji. Huyu chami hatufai kabisa.
 
Unadhani ni nini kifanyike ili fedha za umma zirudi
 
Wabunge wengi hizi fedha za MFUKO WA JIMBO hawazitumii kwa malengo yaliyokusudiwa. Kaka Zitto kamati yako isiishie kwenye ukaguzi wa ruzuku kwa vyama vya siasa tu, ifike mpaka huku kwenye MFUKO WA JIMBO, nazo hizi si fedha za walipakodi?
 
Last edited by a moderator:

Hili suala haliitaji zitto aje ndipo tugundue huu ufisadi, kwani wananchi tiyari wamecomfirm
 
Last edited by a moderator:
Ukiacha hoja ya msingi pembeni, naomba nisahihishe udhaifu mkubwa wa kuandika kuhusu fedha hapa JF. Shilingi 2,880,000 na shilingi milioni 2,880,000 ni vitu viwili tofauti.

Tujitahidi tuongeze umakini.
 
Mbona iko sawa mkuu,
 
Wakati muswada wa kuanzisha huo mfuko wa maendeleo ya majimbo ukijadiliwa bungeni, nilisikitishwa na wabunge wote walioshabikia kuanzishwa mfuko huo akiwemo Dr Slaa na Zitto niliotegemea kuwa wangeupinga. Hakuna mbunge hata mmoja anayeweza kusimama leo na kusema hajawaibia wananchi kupitia mfuko huo. Kwa serikali inayofahamu majukumu yake na kuyasimamia vyema, inapitishaje hela ya maendeleo kwa mbunge? Yote majizi tu, hakuna CCM wala CDM.
 
Sio sawa. Kwa mfano, shilingi elfu 1,000 ni shilingi elfu elfu moja, yaani milioni moja. Ukitaka kuandika shilingi elfu moja unaandka aidha sh.1,000 au shilingi elfu 1.
 
Ukiacha hoja ya msingi pembeni, naomba nisahihishe udhaifu mkubwa wa kuandika kuhusu fedha hapa JF. Shilingi 2,880,000 na shilingi milioni 2,880,000 ni vitu viwili tofauti.

Tujitahidi tuongeze umakini.
Mkuu umeambiwa iko sawa. Usifikiri wote walipata bahati ya kufundishwa na walimu waliokufundisha. Teh teh...
 
Hakuna Mbunge hata mmoja wa CCM aliye msafi.
CCM na Ufisadi ni Mapacha!

Yaani ndio maana tunataka mamlaka yawe kwa wananchi sio viongozi na fedha za umma zinapopitishwa ziwekwe hadharani
 
Huyu jamaa anastahili kucharazwa viboko. Wasukuma mtu akiiba hulowekwa kwenye tope na viboko. Wachaga tunamcharaza viboko tu. Tunakufa njaa huku jamaa anafisadi? Hakianan asubiri viboko
 
Back
Top Bottom