Mbunge wa Moshi vijijini aibia Wananchi Milioni (240)

Mbunge wa Moshi vijijini aibia Wananchi Milioni (240)

Jamaa ameshakata tamaa ya kurudi tena madarakani!

Jimbo hili lina historia ndefu,Pamoja na waakazi wake kuwa na hamu ya maendeleo, Bado wako ktk lindi la umaskini uliokithiri.
 
Kwa hiyo hawajitambui!hii ni hatari sana!

Sio kwamba hawajitambui,wanajitambua lakini hakuna kiongozi mwenye weledi wa maendeleo,Hospitali kuu ktk hili jimbo ni moja tena ya kanisa, shule za msingi na sekondari zipo lakini ni majengo hakuna walim,Maabara,umeme,Barabara,
 
Sasa na nyie wananchi msiwe mambulula, mmeshafanya kosa la kwanza msirudie tena, mlichagua CCM mtu wao amewaibia, labda wana sera za Chukua Chako Mapema mtajuaje? Ni muda muafaka wa kutafakari mtu wa chama kingine kinachotoa upinzani wa kweli TZ na kumuweka agombeee.
 
Mbunge wa Moshi vijijini amewaibia wananchi wa jimbo hilo takribani milioni (240),zikiwa ni fedha za maendeleo ya jimbo zinazotolewa na mfuko wa jimbo kila mwaka kwa miaka (8).

Aidha mbunge Cyril Chami amesitisha kuwatembelea wananchi wake huku akipokea fedha za kuwatembelea wananchi wa jimbo hilo ambazo ni takribani milioni (2,880,000)

Inasikitisha ubadhirifu wa fedha za umma kumilikishwa mtu mmoja kama mfalme hali inayochangia maendeleo kuwa hafifu,

Ni matumaini yangu Mbunge chami atatoa maelezo fedha za walipa kodi zimekwenda wapi??

Ni wakati umefika wananchi tuache kuambiwa tu bali tufanye uchunguzi wa fedha zetu.
@cc
Aisee imndu li njilisuo pata...Nku ai wai? Aarake Msuru na iiwa lyake
 
Sasa na nyie wananchi msiwe mambulula, mmeshafanya kosa la kwanza msirudie tena, mlichagua CCM mtu wao amewaibia, labda wana sera za Chukua Chako Mapema mtajuaje? Ni muda muafaka wa kutafakari mtu wa chama kingine kinachotoa upinzani wa kweli TZ na kumuweka agombeee.

Jimbo hili lina safari ndefu sana, ukizingatia nguvu kazi ya vijana hakuna sababu miundombinu hakuna, vijana wanakimbilia miji iliyojengwa tiyari maana kuna kila kitu.
 
maccm wote wezi tuu ukoo wa panya wezi wote
 
Hivi chami yupo nchi hii kweli? Ana hasira na wananchi kwani ndio waliomnyang'anya uwaziri? Sijawahi kumwona bungeni toka atoswe uwaziri. Na anapokea mshahara wa ubunge kila mwezi wakati kazi ya ubunge hafanyi tena...hii inatia hasira kwa kweli...na hapa ndipo tunahitaji katiba mpya.
 
Hivi chami yupo nchi hii kweli? Ana hasira na wananchi kwani ndio waliomnyang'anya uwaziri? Sijawahi kumwona bungeni toka atoswe uwaziri. Na anapokea mshahara wa ubunge kila mwezi wakati kazi ya ubunge hafanyi tena...hii inatia hasira kwa kweli...na hapa ndipo tunahitaji katiba mpya.
Tunahitaji mageuzi ya sheria wakati huu kuliko wakati mwingine
 
Mbunge wa Bahi, Omar Baduwel, anatuhumiwa kutafuna fedha za Mfuko wa Jimbo zilizokuwa zikirejeshwa na wananchi baada ya kukopeshwamajembe ya kukokotwa na ng’ombe.

Mbali na hilo pia Mbunge huyo anadaiwa kutafuna fedha za mradi wa maji wa kijiji cha Chibelela ambao serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo ilitenga Sh. milion nne kwa ajili ya mradi huo ambao wananchi pia walichangia Sh. milioni 1.7.

Akiwasilisha hoja binafsi katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Bahi, Diwani wa Kata ya Lamaiti, Donald Mejitii (CCM), alilitaka Baraza la Madiwani kuunda kamati kwa ajili ya kuchunguza fedha hizo baada ya halmashauri kushindwa kusimamia makusanyo ya fedha za Mfuko wa Jimbo kwa mwaka mmoja.

Alisema hatua ya kuwasilisha hoja binafsi imefuatia taarifa kuwa kuna mtu anayepita kuzikusanya fedha hizo wakati si mfanyakazi wa serikali na hazifikishwi halmashauri.

“Kinachonishangaza hata hizi pia Mbunge huyo aliamua kuchukua fedha hizo na mpaka sasa hazijulikani zilipo na wananchi bado hawana huduma ya maji … kwa mwaka huu peke yake Mfuko wa Jimbo ulitoa kiasi cha Sh. milioni 17 na wananchi wamerejesha kiasi cha Sh. milioni 8.5 ambazo zimeshakusanywa, lakini hakuna hata kiasi kidogo kilichoingia halmashauri,” alisema Mejitii.

Alibanisha kuwa katika kata yake pekee alipokea majembe 15 na mpaka sasa wamerejesha zaidi ya Sh. milioni 1.5, lakini kwa taarifa alizonazo ni kuwa fedha hizo hazijafikishwa halmashauri.

Mejitii alisema fedha za Mfuko wa Jimbo zimekuwa zikitumiwa vibaya na mbunge huyo kwani amekuwa akizitumia kama fedha zake binafsi hali inayowafanya wananchi kuamini kuwa fedha hizo hutolewa na mbunge na siyo kutoka serikalini.

Aliongeza kuwa wamekuwa wakishuhudia mara kwa mara mbunge akizitumia fedha hizo na kuzipa jina la ‘Kopa kwa mbunge lipa kwa jirani’, hali inayowafanya wananchi kuamini kuwa fedha hizo zinatoka mfukoni mwake na siyo serikalini.

Diwani huyo alisema wananchi wengi hawajui kama fedha hizo zinatoka serikalini kwa kupitia Mfuko wa Jimbo kwani wengi wao wanajua kuwa hutolewa na mbunge na ndiyo maana anapofika kuzikusanya au kumtuma msaidizi wake, wanampa bila ya wasiwasi wakijua ni zake.

“Kwa kuthibitisha hili, hata wananchi wanapotakiwa kurejesha fedha hizo mbunge huyo huzichukua na hazijulikani matumizi yake kwani hazifiki hata halmashauri,” alisema.

Aidha, alitolea mfano katika mradi wa majembe ambao ulianzishwa na Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kuwakopesha wakulima na baadaye walipe nusu ya gharama, lakini makusanyo hayo hayajafikishwa halmashauri.

Alisema anasikitishwa na kitendo cha kumuona msaidizi wa mbunge akipita kwa wananchi kukusanya fedha hizo wakati siyo mtendaji wa serikali na hajawahi kufikisha kiasi chochote halmashauri.

“Hakuna hata shilingi moja iliyofika kwenye halmashauri, sasa nataka kujua kama huo mradi ni wa Mfuko wa Jimbo au ni kwa ajili ya kuwanufaisha watu wachache,” alisema.

“Pia kikundi kilichopewa jukumu la kukopesha majembe cha Basada kimekuwa kikiwatoza wananchi kiasi kikubwa cha fedha kuliko bei halisi ya kununulia majembe ya kukokotwa na ng’ombe wakati bei halisi ya jembe moja ni kati ya Sh. 180,000 hadi 170,000, lakini wananchi wanatozwa Sh. 110,000 kama nusu ya bei ya jembe badala ya Sh. 80,000 au 85,000 ambacho ndiyo kiasi sahihi kwani mwananchi anatakiwa kutoa kama nusu ya bei,” alifafanua Mejitii.

Baada ya Diwani huyo kuwasilisha hoja hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Hussein Kamau, aliwahoji madiwani na baadhi yao walisema kwamekuwa wakiona fedha hizo zikikusanywa, lakini hawajui zinapokwenda.

Kamau baada ya kusikiliza hoja hiyo, aliamua kuunda kamati kwa ajili ya kuchunguza tuhuma hizo na kuwateua wajumbe wanne. Kati yao wawili ni madiwani na wawili ni watumishi wa halmashauri.

Alipoulizwa na NIPASHE kuhusiana na tuhuma hizo, Mbunge huyo alisema: “Mkienda Chibelela mtakuta maji yanatoka, hakuna shida yoyote katika kijiji hicho.”

Kuhusu fedha za mradi wa majembe, alisema kuwa yeye hakusanyi fedha za majembe kwani siyo kazi yake na kuwa kazi yake ni kukabidhi, hivyo waulizwe waliozikusanya.

“Msaidizi wangu wana uhakika gani kama nimemtuma, wangeniuliza mimi kama nimemtuma, watu wanaongea tu wala hawajui mimi nina matatizo gani na msaidizi wangu. Kiukweli maji yanatoka Chibelela na fedha za majembe mimi sijakusanya,” alisema na kuongeza:

“Najua kuna mtu anataka ubunge ndiyo maana wanasema hivyo.”

Mbunge huyo angali anakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa.
CHANZO: NIPASHE
 
CCM ni UKOO wa PANYA...ni chama cha wauaji wangoa meno na kutoboa macho.
 
CCM ni UKOO wa PANYA...ni chama cha wauaji wangoa meno na kutoboa macho.

Wananisikitisha sana, na huyu mbunge ana tuhuma za rushwa alikamatwa red handed na takukuru lakina CCM haijamchukulia hatua yoyote...upuuzi kabisa
 
Hivi huyu si wakati ule alikamatwa laivu akipokea rushwa? Nilidhani alisimamishwa! Kweli ukoo wa panya!
 
Huyu Takukuru walikuwa wamemkamata muda fulani, wakamwachia
Waandishi Wetu

Toleo la 242
6 Jun 2012
HALI ya kisiasa na kiutawala imeendelea kuwa tete nchini kutokana na matukio mbalimbali na uamuzi wa viongozi wakuu kuhusu namna ya kupata suluhu ya matukio hayo ambayo baadhi ni hatari kwa amani ya nchi.

Kwa baadhi ya matukio na hasa vurugu za hivi karibuni visiwani Zanzibar zilizohusisha uchomaji wa makanisa na baadhi ya vitega uchumi vya watu binafsi, unasubiriwa mwongozo wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Mwongozo huo unasubiriwa ili kupimwa na wananchi pamoja na viongozi wa dini ili kujiridhisha kama utaibua suluhu ya matukio hayo kujitokeza tena.


Lakini wakati mwongozo huo ukisubiriwa, kwa upande mwingine, hatua ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kumkamata na kumfungulia mashitaka Mbunge wa Bahi, mkoani Dodoma, Omar Badwel wiki hii, l imewasilisha ujumbe tofauti miongoni mwa wabunge na viongozi wengine wa kitaifa.


Kuna hali ya wasiwasi miongoni mwa viongozi hao, hasa wale ambao wamekwishakuwahi kuhojiwa na maofisa wa TAKUKURU kuhusu baadhi ya taarifa zinazowahusisha katika vitendo vya rushwa.


Kama vile ni mwendelezo wa hali ya sintofahamu, mawaziri takriban wapya nao wanakabiliwa na mtihani mzito wa kutetea bajeti zao ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikielezwa kuwa, kutokana na udhaifu sugu katika wizara hizo, mawaziri hao bila kujali kuwa ni wapya, watakumbana na mazingira magumu pindi bajeti za wizara wanazoongoza zitakapokuwa zikijadiliwa bungeni.
 
Ccm ni kama ukoo wa Chenge. Wanaiba na kufisadi bila huruma.
 
Back
Top Bottom