idawa
JF-Expert Member
- Jan 20, 2012
- 25,298
- 38,438
Mh.Silinde leo ameomba rasmi kujiunga na Chama Mapinduzi, na amesema yupo tayari kukitumikia Chama Cha Mapinduzi kwa nguvu zote.
Spika Ndugai amemkaribisha na kumhamisha kwenye viti vya Upinzani kumpeleka kwenye viti vinavyokaliwa na wabunge wa CCM.
Hivyo kuanzia leo rasmi Silinde ni mbunge wa CCM na atakaa upande wa wabunge wa CCM. Davidi amekuwa mbunge kwa tiketi ya CHADEMA tangu mwaka 2010
Mbunge huyo alijiuzulu nafasi zote za uongozi ndani ya CHADEMA mwezi Mei, baada ya wabunge wenzake kumtaka kufanya hivyo kwa kutotii agizo la kutokwenda bungeni
Wakati anajiuzulu alisema wananchi ndio walimtuma bungeni, hivyo hata akikosa udhamini wa CHADEMA, atatumia chama kingine
Live kutoka bungeni.
Pia soma
Silinde: Maamuzi ya kutufukuza ni ya kitoto. Kuna udikteta CHADEMA, Mbowe ajitafakari na kuachia Uenyekiti
Mbunge wa Momba, David Silinde awatolea uvivu CHADEMA, asema yeye hapelekeshwi na Mbowe bali wapiga kura wa Momba
Spika Ndugai: Hakuna Mbunge aliyefukuzwa Ubunge. Vikao vya majungu havifanyi kazi hapa, Msajili tazama vyama vya namna hii