Mbunge wa Kisarawe kiingereza bado ni alien language

Jamani hizi takwimu mnazipata wapi wapi? Wachina wako billion 2? Ama kweli Jamii Forum!

Salisalum, Kutokana na sensa ya Desemba 31,2012 nchi ya China ilikuwa na watu 1,354,040,000. India ilikuwa na watu 1,210,569,573 kutokana na sensa iliyofanyika Machi 1,2011. Kutokana na sensa iliyofanyika Ogasti 26,2012, Tanzania inasemekana ilikuwa na watu 44,928,923. Nchi ya Vatican ilikuwa na watu 800 tu hapo Julai 1,2012! Dunia nzima ilikuwa na watu bilioni 7.09 hapo mwaka 2012! Kwa uthibitisho zaidi ingia kwenye google.
 
I am listening to Lolensia. Its interesting. Kuna haja ya kureview curriculum yetu ili kuona ni namna gani tunaweza kuboresha somo la kiingereza katika nchi yetu. At a master level kushindwa kujieleza kwa kiingereza, kwa kweli ina mengi ya kutueleza kuhusu elimu yetu.

Wenzao hujifunza kiingereza kuanzia University km option na baadaye kukiongea vyema kuliko wabongo walioanzia primary.
 
kwani kujua kingereza ndo kutaleta mabadiliko???
Mbona wabunge wa china hawakijui na wana maendeleo?

Japo ni vyema kujua kingereza vizuri lakini haimaanishi kuwa eti ndo maendeleo yatakuja
kwanza bunge linaendeshwa kwa kiswahili!

Well,kwa kiasi fulani upo sahihi na kiasi fulani upo very wrong.

-Kushindwa ongea kiingereza,kunaweza sababishwa na,tabia fikra pamoja na uwezo wa mtu ktk kuelewa mambo.

-Wale jamaa wanashindwa kiingereza kwa vile:Kwanza hawajitambui,na ni watu wavivu kujifunza,na wenye mizaha ila wenye kupenda sifa.--Jamaa walikuwa wanakosea (L/R),hilo wanalijua ila hawakupenda jikubali na kufanyia kazi.So wanaachia tuu halafu wanapambana kurembesha sauti ili wasikike km wazungu ingawa bado wananasikika kam wandengereko.

-Hawa jamaa hawajajifunza kabisa kuwa ktk kuongea Lugha, maneno ya kawaida na mepesi,yanayobeba maana kamili ndio vitu sahihi vya kuchagua.Wao km kawaida ya waafrica wana complicate vitu halafu ndio wanaanza vifanya.Walikuwa wakitumia maneno wasiyoyaweza,maneno ambayo hata waingereza wangechukua dictionary ili kuhakiki km litaweka maada wanayohitaji.

-Mara nyingine uchaguzi wa maneno na mpangilio wa Logic ndani ya sentensi unaweza sema uwezo wa mtu kifikra.Ktk science kushindwa jua neno sahihi la process fulani inayopishana kidogo sana na nyingine kunaweza toa tafsiri kuwa huyu mtu hajui hivyo vitu vyema kiasi chw kuweza tenganisha,na pia hajui jinsi hizo process zinafanyika.
 
I am listening to Lolensia. Its interesting. Kuna haja ya kureview curriculum yetu ili kuona ni namna gani tunaweza kuboresha somo la kiingereza katika nchi yetu. At a master level kushindwa kujieleza kwa kiingereza, kwa kweli ina mengi ya kutueleza kuhusu elimu yetu.

Wenzao hujifunza kiingereza kuanzia University km option na baadaye kukiongea vyema kuliko wabongo walioanzia primary.Tatizo si Kiingereza ila watanzania na fikra zao.Fikra zetu hazitusaidii sana,ktk kujua lugha moja, n akuweza itumia vyema kutambua na ku describe mazingira na fani ya mtu binafsi.
 
Huyu dada ni mbunge wa kuchaguliwa na wananchi jimbo moja huko mkoa wa Mwanza.

Kweli Ni mbunge wa kuchaguliwa , jimbo lake lipo mkoa wa Geita.huyu kwa cv yake ilivyo nilidhani ndio atajieleza vizuri kuliko wote. Big up Leticia Nyerere
 
Nina Rafiki yangu amekuwa House Boy wa wazungu karibu miaka kumi na tano sasa japo aliishia la nne ana uwezo wa kuongea kiingereza saa 24 mfulululizo nadhani huyu angepata nafasi ya kuomba kura bungeni tungemsapoti ba ndugu!
 
Lugha yoyote inahitaji kufanyiwa mazoezi ya kutosha ili kuifahamu. Mazoezi ya kuzungumza. Hili ndilo tatizo la kiingereza cha watanzania wengi. Hujifunza lugha hiyo darasani, lakini hakuna mazoezi ya kuzungumza mitaani, makazini, nk. Ole wenu mjaribu kuwasiliana kwa kiingereza ndani ya daladala au mitaani - mtaambiwa mnaringa/mnajisikia sana!
 
Wenzao hujifunza kiingereza kuanzia University km option na baadaye kukiongea vyema kuliko wabongo walioanzia primary.Tatizo si Kiingereza ila watanzania na fikra zao.Fikra zetu hazitusaidii sana,ktk kujua lugha moja, n akuweza itumia vyema kutambua na ku describe mazingira na fani ya mtu binafsi.

Mkuu mengi uliyoelezea ni ya kweli. Lakini mimi nafikiri tatizo letu watanzania liko kwenye elimu. Ni wengi sana hata ukiwaambia waongee kwa lugha ya kiswahili hawawezi kijieleza vitu vya maana. Tumezoea Mwingulu and Lusinde style. Mipansho na matusi. Hoja kwetu hatuziwezi!
 
Nina Rafiki yangu amekuwa House Boy wa wazungu karibu miaka kumi na tano sasa japo aliishia la nne ana uwezo wa kuongea kiingereza saa 24 mfulululizo nadhani huyu angepata nafasi ya kuomba kura bungeni tungemsapoti ba ndugu!

Kule Arusha, wale "Fly Catchers" huwa wengi hawajaenda shule,ila wanajiamini na kujua ni maneno gani wayatumie msikilizaji apate ujumbe hata kama grammer ni mbovu, na muda si mrefu nao hujikuta wanamaster vyote.Hawa fly catcher wanafanya biashara na kukubalika na wageni kuliko wapiga pose,wenye vyeti.

Lugha yoyote ujuayo ,huwezi sema unaijua unless uweze chagua na kupangilia maneno ili yafikishe si tuu maana ila hata hisia zako.Pia kuweza amsha hisia za mwingine....imagine yule mbunge awe anafanya marketing au hata tongoza raia wa nchi nyingine.atmosphere itakuwa so tense.Mbunge hata akiongeacho hakijui?Wapo watu wa mataifa mengi tuu,ambao si wazuri wa lugha ila wakiongeacho unaelewa na kupata maana ktk maneno machache...
 
Nipo ninatazama bunge hapa. Baadhi ya wabunge wanaomba kura kwenye post katika institutions mbalimbali. Dah wale wanaojieleza kwa kingereza mpaka naona aibu. Kingereza kibovu kibovu kibovu...hakuna flow katika kujieleza hata wale wanaojieleza kwa kiswahili. Wengine wanatetemeka. Dah nchi yetu bado sana kama hawa ndo krimu yetu!???? Dah mpaka nimeona aibu ingawa niko mwenyewe ndani. Hawa ndo wanatakiwa kuleta mabadiliko katika jamii yetu?

Nani kakudanganya hao ni "krimu"? "krimu" hawana muda wa siasa!
 
Kuzungumza kiingereza hawezi,maendeleo Kisarawe hakuna..sijui ana faida gani. Mpaka leo Kisarawe haina lami,maji wala umeme.
 
Kuzungumza kiingereza hawezi,maendeleo Kisarawe hakuna..sijui ana faida gani. Mpaka leo Kisarawe haina lami,maji wala umeme.

Anaweza kuongea kiswahili na kushiriki sana ktk issue za viunga vya ponda+vyeti vya kimikakati basi lazima apigie upatu kuwa ni msomi.Na akiachwa kwa kiingereza vurugu linaanzishwa...kuwa kiingereza lugha ya watumwa na blah blah nyingine...Kwa vile hawatataka kukubali km mtu tangu primary hadi chuo kikuu ni miaka mingi sana haafu mtu kushindwa jieleza kwa lugha nyepesi kuna shida kubwa zaidi hata kujua concepts za vitu anavyovisema.
 
Back
Top Bottom