Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdulaziz Abood ashiriki mahafali ya kidato cha 4 Sekondari ya Mafiga

Oct 8, 2023
37
17
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Mhe. Abdulaziz M. Abood

20/10/2023 amekuwa Mgeni Rasimi kwenye Mahafali ya kumi na tatu 13 ya wanafunzi wa kidato cha nne kwenye Shule ya Secondary Mafiga. Mbunge amefika shuleni hapo na kupokelewa na maelfu ya wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, Shule na Chama cha Mapindunzi.

Mhe Mbunge baada ya mapokezi hayo aliingia ofisini kwa mkuu wa Shule kwaajili ya kusahini kitabu cha wageni na baada ya kusaini kibatu Mbunge akaongozana na viongozi mbalimbali kuelekea jukwaa kuu. Wakati wakiingia jukwaa kuu maelfu ya wananchi pamoja na wanafunzi walisimana na kukatawaliwa na vifijo, ndelemo, vigeregere na miluzi kwa Mbunge wao kipenzi Mhe Abood .

Baada ya Mhe Mbunge kuketi kwenye jukwaa kuu, shughuri ikaendelea kwa utambulisho wa viongozi mbalimbali na baada ya utambulisho huwo, Mbunge akashuhudia michezo mbalimbali iliyoandaliwa na wanafunzi ili kuchagiza sherehe hiyo.

Baada ya yote ikafika wakati wa Risala, risala ikasomwa mbele ya Abood naye akawa makini sana kusikiliza risala hiyo. Risala hii ilibeba mambo mengi zikiwemo shukurani kwa serikali ya Mhe. Rais Samia pamoja changamoto walizonazo.

Risala hii imemshukuru Rais Samia kwa namna ambavyo amekuwa shupavu na jasiri namna ambavyo anapambana kuleta maendeleo kwenye sekta ya elimu, pamoja na hayo wamemshukuru Mhe Rais Samia kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa tisa 9 pamoja na thamani zake, ujenzi wa jengo la utawala, ujenzi wa jengo la maabara na ujenzi wa jengo la maktaba.

Kwa upande wa changamoto, risala hii imetaja changamoto zinazoikabiri shule kama ifuatavyo; UKOSEFU WA BWENI (HOSTEL), UKOSEFU WA UKUMBI WA MIKUTANO (BWALO), ENEO LA KUJENGA UKUMBI PAMOJA NA BWENI,
UCHAKAVU WA BAADHI YA MAJENGO, UKOSEFU WA VIFAA VYA TEHAMA KAMA VILE PROJECTA NA KOMPYUTA MPAKATO (LAPTOP), UZIO (RING FANCE) NA VITI PAMOJA NA MEZA ZA WALIMU.

Baada ya risala hiyo kusomwa ikakabidhiwa kwa Mhe Mbunge, na baada ya Mhe Mbunge kupokea risala hiyo akaijibu kama ifatavyo.

Kwanza Ameanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu pili akaishukuru Serikali na kumshukuru Mhe. Rais Samia kwa namna ambavyo amekuwa msikivu na mtekelezaji pale anapopelekewa jambo la Morogoro Mjini. Mhe Mbunge amesema kuwa Serikali ya Mhe. Rais Samia ni Serikali sikivu na mama yetu kipenzi Rais Samia anapambana na kuhakikisha wananchi wake wanapata kile wanachokiitaji.

Mhe Mbunge akijibu risala yao amesema ili waweze kujenga BWENI NA UKUMBI lazima wawe na eneo kubwa la kujenga majengo hayo. Kwahyo Mbunge akawaahidi jambo la kwanza ataenda kuzungumza na mkuu wa chuo cha kilimo yaani SUA ambao ndo wamiliki wa eneo kubwa linalozunguka Shule hiyo ili wakipata eneo ndo waanze taratibu za ujenzi.

Kwa ukosefu wa vifaa vya tehama kama vile projecta na kompyuta mpakato (laptop) Mhe Mbunge ametoa vifaa hivyo mbavyo ni LAPTOP NA PROJECTA.

Kwa uchakavu wa majengo, kwa changamoto hii Mhe Mbunge ametoa mifuko ya SARUJI MIFUKO MIAMOJA (SIMENTI 100) kwaajili ya kuanza ukarabati huo.

Kwa changamoto ya viti, meza na uzio Mbunge amesema kuwa atashirikiana na Mhe Diwani wa kata ya Mafiga kuhakikisha viti, meza na uzio vinakuwepo.

HITIMISHO
Mhe Mbunge amewashukuru wazazi na kuwasii waendelee kushirikiana na Shule hiyo ili kupandisha ufaulu wa Shule hiyo.

IMG-20231020-WA1073.jpg
 
Walimu wakuu WA siku hizi ni machawa balaa yahn mahafali ya watoto wanageuza inakuwa kama shughuli ya chama.
 
Back
Top Bottom