Morogoro Mjini: Neema yaja kwa wakazi wa kata za Kihonda, Lukobe, Mkundi, Makunganya na Kiyegea

Oct 8, 2023
37
17
Serikali yadhamilia kumaliza kilio cha muda mrefu cha ukosefu wa maji kwa wananchi wa kata hizo pamoja na maeneo ya jirani, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na MHE. RAIS. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN imedhamilia kumaliza kilio cha ukosefu wa maji kwenye kata hizo pamoka na maeneo ya jirani.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini MHE. ABDULAZIZ M. ABOOD ametembelea na kukagua ulazaji wa mabomba ya maji kwenye kata hizo, Mhe Mbunge akiongea na wananchi baada ya kukagua zoezi la ulazaji mabomba amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya Mama Samia ni Serikali sikivu na imedhamilia kumaliza kabisa kilio chao cha maji.

Vilevile Mhe Mbunge amesema kuwa Serikali imeleta pesa Tsh 2,100,000,000 (BILLION MOJA NA MILION MIA MOJA) kwa Moruwassa ili kuhakikisha zoezi la kuwapatia wananchi maji linakamilika kwa wakati.

Aidha Mhe. Mbunge amewaeleza Moruwassa kuwa wahakikishe wanafanya kazi mchana na usiku ili kuendana na kasi ya Mhe Rais Samia, Serikali inaitaji wananchi wake wapate maji ndiyo maana inaleta pesa nyingi.

Pia wananchi baadhi wamepata nafasi ya kuongea mbele ya Mhe Mbunge wao, akiongea mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la RAMADHANI SAID JUMA kwa niaba ya wananchi wenzake amesema kuwa:

"Tunaishukuru sana Serikali hakika inatupenda sana hatua hii na jitihada hizi wanazozifanya kuhakikisha wanatatua changamoto zetu hatuna cha kuwalipa isipokuwa 2025 kura zetu ni kwa CCM, sisi kama wananchi tunakupongeza pia wewe Mbunge wetu kwa moyo wako wa kuhakikisha wananchi wako tunatoka kwenye changamoto hii, kutoka mioyoni mwetu tunasema Mungu akubariki sana Mbunge wewe umekuwa rafiki yetu na ndugu yetu tunakuombea kwa Mungu akulinde uwe na afya njema kila wakati na tunakuhakikisha 2025 tukiwa na uhai kura zetu zote ni kwako Mhe Abood".

ZIARA INAENDELEA JIMBONI

IMG_20231010_145437_222.jpg
IMG_20231010_142845_689.jpg
 
Kwamba alikuwa hajui kuwa maji ni tatizo? Mwambie like kisima cha mchongo alicho chimba pale kiegeya tangu aondoke 2018 hakitoi maji. Pia bomba la maji kuelekea kwa wamasai kutoka Kingolwira shule halijawahi kufanya tangu aliweke 2015
 
Ukitaka ukutane na typhod tumia maji ya mji kasoro bahari

Ova
 
Asante japokuwa umeandika kwa mhemko wa kusifia kama ilivyo jadi. Hebu radiation kusoma hizo Nambari ulizoandika na Maandishi yako ya herufi kubwa ukitaka kusisitiza kumbe ni mwongopeaji wewe!
 
Chama cha Mambuzi mko vizirì ktk maigizo,yaani mnafanya kampeni muda wote.Wakati mwingine angalau basi muwe na aibu.Mnachosha kwa kweli.
 
Serikali yadhamilia kumaliza kilio cha muda mrefu cha ukosefu wa maji kwa wananchi wa kata hizo pamoja na maeneo ya jirani, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na MHE. RAIS. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN imedhamilia kumaliza kilio cha ukosefu wa maji kwenye kata hizo pamoka na maeneo ya jirani.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini MHE. ABDULAZIZ M. ABOOD ametembelea na kukagua ulazaji wa mabomba ya maji kwenye kata hizo, Mhe Mbunge akiongea na wananchi baada ya kukagua zoezi la ulazaji mabomba amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya Mama Samia ni Serikali sikivu na imedhamilia kumaliza kabisa kilio chao cha maji.

Vilevile Mhe Mbunge amesema kuwa Serikali imeleta pesa Tsh 2,100,000,000 (BILLION MOJA NA MILION MIA MOJA) kwa Moruwassa ili kuhakikisha zoezi la kuwapatia wananchi maji linakamilika kwa wakati.

Aidha Mhe. Mbunge amewaeleza Moruwassa kuwa wahakikishe wanafanya kazi mchana na usiku ili kuendana na kasi ya Mhe Rais Samia, Serikali inaitaji wananchi wake wapate maji ndiyo maana inaleta pesa nyingi.

Pia wananchi baadhi wamepata nafasi ya kuongea mbele ya Mhe Mbunge wao, akiongea mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la RAMADHANI SAID JUMA kwa niaba ya wananchi wenzake amesema kuwa:

"Tunaishukuru sana Serikali hakika inatupenda sana hatua hii na jitihada hizi wanazozifanya kuhakikisha wanatatua changamoto zetu hatuna cha kuwalipa isipokuwa 2025 kura zetu ni kwa CCM, sisi kama wananchi tunakupongeza pia wewe Mbunge wetu kwa moyo wako wa kuhakikisha wananchi wako tunatoka kwenye changamoto hii, kutoka mioyoni mwetu tunasema Mungu akubariki sana Mbunge wewe umekuwa rafiki yetu na ndugu yetu tunakuombea kwa Mungu akulinde uwe na afya njema kila wakati na tunakuhakikisha 2025 tukiwa na uhai kura zetu zote ni kwako Mhe Abood".

ZIARA INAENDELEA JIMBONI

View attachment 2778739View attachment 2778762
Uhuni mtupu, watu wanataka maji siyo mikogo ya kusimama kwenye picha na miwani ya jua wakati kuna mawingu
 
Back
Top Bottom