Mbunge wa CHADEMA ahukumiwa jela

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
JUMAMOSI, JULAI 21, 2012 09:23 NA JOHN MAKAMBO, TABORA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora, imemhukumu Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbai (Chadema), kifungo cha miezi minne jela ama kulipa faini ya Sh 100,000, baada ya kumtia hatiani.

Mahakama hiyo, ilimtia hatiani Kasulumbayi kwa kosa la kumshambulia aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario ambaye sasa amehamishiwa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.

Mbali ya Kasulumbayi, mahamaka hiyo ilimhukumu kifungo cha miezi minne jela ama kulipa faini ya Sh 100,000 mwanachama mwingine wa chama hicho, Robert Magilani (30) kwa kupatikana na kosa hilo.

Washitakiwa wengine, Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Kiwanga na Katibu wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Wilaya ya Igunga, Anuary Kashaga waliachiwa huru na mahakama, baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa yao.

Kasulumbai pamoja na kupatikana na hatia ya kosa hilo, pia alitiwa hatiani kwa kosa la shambulizi la lugha chafu dhidi ya Kimario.

Pia mahakama hiyo, ilimwamuru Magilani kulipa faini ya Sh 50,000, ama kutumikia kifungo cha miezi mitatu jela.

Mahakama hiyo pia iliwahukumu washitakiwa hao wawili kumlipa fidia Kimario ya Sh 100,000, kila mmoja kutokana na kumsababishia madhara kwenye mwili.

Akisoma hukumu hiyo, iliyochukua muda wa dakika 30, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora, Thomas Simba, alisema mahakama imewatia hatiani washitakiwa hao katika makosa mawili ambayo ni shambulio na kutumia lugha ya matusi dhidi ya Kimario.

Hata hivyo, alisema mahakama ilifuta mashitaka mengine mawili yaliyokuwa yakiwakabili washitakiwa hao, ambayo ni kumwibia simu mbili za mkononi aina ya Nokia na kumweka chini ya ulinzi isivyo halali.

Baada ya kuwatia hatiani washitakiwa hao, wakili wa utetezi Mpogolo aliiomba mahakama kutotoa adhabu kali dhidi ya mshitakiwa huyo, kwa sababu ana umri wa miaka 62, wake watatu na watoto 27, huku akiwa na maradhi ya ugonjwa wa moyo na miguu kwa muda mrefu hivyo ana majukumu makubwa kifamilia.

Huku Magilani akielezwa kuwa ni kijana mdogo, ana mke na mtoto mmoja hivyo kupewa kwake adhabu kali kutaiathiri familia.

Itakumbukwa mapema mwaka huu, Kimario alikutwa na viongozi wa Chadema katika Kijiji cha Isakamaliwa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, akifanya mikutano na viongozi wa Serikali za vitongoji, kata, vijiji na madhehebu ya dini kinyume na sheria za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

SOURCE: MTANZANIA

I thought CHADEMA walishinda hiyo Kesi; Sasa Iweje huyo Mbunge ahukumiwe faini au Jela kwa Masumbufu ya Mkuu

Mkuu wa Wilaya na waliwakuta hawana hatia? au kuna hukumu tofauti?
 
JUMAMOSI, JULAI 21, 2012 09:23 NA JOHN MAKAMBO, TABORA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora, imemhukumu Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbai (Chadema), kifungo cha miezi minne jela ama kulipa faini ya Sh 100,000, baada ya kumtia hatiani.....
Nyie vipi? jana kuna mmoja ka post thread humu jf akidai kuwa CDM wameshinda kesi........ au hukumu hii ina tafsiri nyingi tofauti?
 
Kwanini Fatma Kimario alihamishiwa Pwani kama hamuendelezi udini na taswira mbaya kwa taifa?Hii serikali imeingia kwenye mtego mbaya sana.Kila inalofanya halina taswira ya umoja,badala yake wanadhani wanadhoofisha vyama vya upinzani kumbe wanaharibu taifa.
 
Aende jela akaendeshe harakati kwa wafungwa, chadema wawe na Tawi la Gerezani!
 
nyie vipi? jana kuna mmoja ka post thread humu jf akidai kuwa CDM wameshinda kesi........ au hukumu hii ina tafsiri nyingi tofauti?

Yeah, Sasa Mimi ndio nimeuliza walitoa wapi hiyo ya kushinda na kutupilia mbali issue ya Mkuu wa Wilaya na wakati

Stori hii inaoyesha walitoa hukumu ya kumsumbua Mkuu wa Wilaya
 
nimeshndwa kuelewa!

Kiasi ushindwe kuelewa maana huyu hakimu hajui kazi yake ,hapa alitakiwa atoe fundisho ,yaani kama miaka 7 au 10 ,ili iwe somo la bure kwa wengine.Miezi minne ,mwizi wa kuku anaweza kupoteza maisha au kula miaka ap jela,hakimu usikosee tena kutoa hukumu ya aina yake haswa kwa hawa watu wa siasa .wote bila ya kuheshimu anatoka chama gani.
 
nyie vipi? jana kuna mmoja ka post thread humu jf akidai kuwa CDM wameshinda kesi........ au hukumu hii ina tafsiri nyingi tofauti?
unakera sana unapo quote habari defu kisha comment zako zinakosa mashiko

jirekebishe mkuu ikiwezekana taja id yake kisha link ujumbe ataupata tu
 
Kiasi ushindwe kuelewa maana huyu hakimu hajui kazi yake ,hapa alitakiwa atoe fundisho ,yaani kama miaka 7 au 10 ,ili iwe somo la bure kwa wengine.Miezi minne ,mwizi wa kuku anaweza kupoteza maisha au kula miaka ap jela,hakimu usikosee tena kutoa hukumu ya aina yake haswa kwa hawa watu wa siasa .wote bila ya kuheshimu anatoka chama gani.

Hapo penye red ; Ina maana alitakiwa ajitungie adhabu au atoe adhabu kutokana na sheria inavyosema?
 
CCM imepora uhuru wa Mahakama
JUMAMOSI, JULAI 21, 2012 09:23 NA JOHN MAKAMBO, TABORA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora, imemhukumu Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbai (Chadema), kifungo cha miezi minne jela ama kulipa faini ya Sh 100,000, baada ya kumtia hatiani....
 
Pamoja na hukumu hii, ila salam ziliwafikia ma-DC wote, na wale wote wanaoleta ukada wao kwenye mambo ya Umma.
 
Pamoja na hukumu hii, ila salam ziliwafikia ma-DC wote, na wale wote wanaoleta ukada wao kwenye mambo ya Umma.

hakimu katumia hekima alijua wazi ni kesi ya kuwakomoa cdm akatoa option ya faini ili wasiende jela
 
Hapo penye red ; Ina maana alitakiwa ajitungie adhabu au atoe adhabu kutokana na sheria inavyosema?
NAni kakwambia kama kuna sheria au kifungu ,hakimu tu inavyomsanifu anakusweka ,sema huwa anaongezea kaneno haka...iwe fundisho kwa wengine...! Basi huwa amefunga kazi. Hapo hakuna kuhoji tena kama amefuata sheria au hakufuata.
 
Baada ya kuwatia hatiani washitakiwa hao, wakili wa utetezi Mpogolo aliiomba mahakama kutotoa adhabu kali dhidi ya mshitakiwa huyo, kwa sababu ana umri wa miaka 62, wake watatu na watoto 27, huku akiwa na maradhi ya ugonjwa wa moyo na miguu kwa muda mrefu hivyo ana majukumu makubwa kifamilia.

Huko Chadema kuna mambo, huyu Slyvester Kasulumbai ni uamsho wa aina fulani hv....
 
Back
Top Bottom