Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema apelekwa mahabusu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema apelekwa mahabusu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Henry Kilewo, Oct 31, 2011.

 1. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema , amepelekwa gerezani leo baada ya kukataa dhamana mahakamani Arusha. iIa ameacha waraka kwa wananchi wake wa Arusha mjini pamoja na watanzania wapigania haki.

  Nitauwekea waraka huwo muda simrefu.

  WARAKA WA GODBLESS LEMA KWA WANA WAARUSHA NA WATANZANIA WAPENDA MABADILIKO KOKOTE KULE WALIPO ULIMWENGUNI

  JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.

  Wapendwa wapiga kura wangu na Watanzania wenzangu.

  Sina wakati mgumu kuchukua maamuzi haya yanayotokea leo. Upendo huu nilio nao kwa watu wa Arusha na nchi yangu ni sababu ya msingi ya maamuzi haya. Nimetishwa mara nyingi, rafiki zangu wametishwa, jamii ya watu duni imeendelea kuishi kwa mashaka na matisho kwa muda mrefu.

  Katika mazingira haya, nikawaza sana kuwa anatakiwa kutokea mtu mmoja jasiri atakayeweza kuona thamani ya watu wengine. Huyo mtu anaweza kuwa wewe lakini kwa wakati huu siwezi kumsubiri tena na nimechagua kuwa mimi nikiamini kuwa utanikuta nikiendelea na safari ya ukombozi.

  Tupo wengi sana tunaotaka mabadiliko, haki na ukweli. Hata hivyo hofu, woga na mashaka yamepoteza thamani yetu yote ya maana ya kuishi.

  Waliofungwa kwa kuonewa na kuteswa, waliokosa chakula na kulala nje, waliokwenda hospitali na kukosa madawa, waliokosa ajira na kipato mpaka kujikuta wametoroka familia zao, waliopoteza matumaini ya maisha, waliopora utajiri wa nchi yetu kwa manufaa yao binafsi, walionunua haki na sheria dhidi ya wajane na wanyonge na kuwapora vipato vyao vidogo na mashamba yao, USIULIZE SABABU NINI!

  Nimetafakari sana na nikatambua kuwa sababu ni mimi pale nilipokuwa kimya wakati wajane na wanyonge wanaonewa.

  NIliposikia wengine wanaandamana kupinga uovu, uonevu, wizi, ufisadi na ukandamizaji wa haki nikasema ni hao na wala sio mimi, kumbe nilipaswa kuwa mbele katika harakati hizi.

  Nilipoona wenzangu hawawezi kupata matibabu nikasema mimi sio mgonjwa, nilipopata taarifa za rafiki zangu kufungwa kwa makosa yasiyo yao, nilipoona watoto wa mitaani wanaomba chakula, nilipoona wazee wamepoteza matumaini ya kuishi katika uzee wao, nilipoona vijana hawana ajira, nilipoona mabinti wasichana wadogo wameamua kufanya biashara ya ukahaba, NIKATAFAKARI,TENA NIKATAFAKARI, dhahabu zetu, almasi yetu, Milima na mabonde yetu, Tanzaninte yetu, samaki wetu, Uranium yetu, makaa ya mawe yetu, utalii wetu, ardhi na kilimo chetu na zaidi utu na mahusiano yetu.

  Na sasa siwezi kukaa kimya tena. NI afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu. Na katika msingi huu hofu na mashaka vimekosa thamani kwangu, sitamwogopa mtu yoyote, mwenye silaha yoyote, mwenye cheo chochote na wala sitaogopa jela yoyote katika kupigania haki, utu wa kweli katika jamii yangu.

  Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendela kutunyanyasabila sababu ya msingi LAKINI SISI TUNAJUA TUTASHINDA KWA SABABU HAKI TUNAYOIPIGANIA NI MAKUSUDI YA MWENYEZI MUNGU.

  Leo nitakwenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa NIA YA KUJITAFUTIA UTUKUFU WANGU bali ," JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.

  Kila mara nilipotishiwa nikagundua wanaonitishia, wananitishia kwa jela na mauti. Na mimi nikagundua na nikatambua ni afadhali kuishi miaka hamsini jela huku sababu ikiwa ni kupinga uonevu na ukandamizaji kuliko maisha ya woga na anasa yasiyo na kusudi katika kutetea utu na heshima ya mwanadamu mwenzangu.

  Wale mlionitishia kunipeleka jela sasa nimetangulia kwa hiari yangu na wale mliobaki msiogope jela endeleeni kupigania ukombozi utakaoleta usawa katika nchi yenu.

  Watakaotubeza na kututukana wasameheni kwani wanahitaji ukombozi wa fikra, watakaotupongeza na kutuonea huruma wafundisheni ujasiri na waambieni mapambano bado yanaendelea tunahitaji umoja wao. Nitarudi mapema. MSIOGOPE, MSIOGOPE, MSIOGOPE , MUNGU YUPO UPANDE WETU.

  Mhe Godbless Lema (MB) – Arusha Mjini 31 Oktoba 2011.


  wengine mnaweza kudownload View attachment lema.pdf
   
 2. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hizi mbwembe zingine bwana... Siasa za utoto.
   
 3. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu, tunasubiri waraka mkuu...
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,001
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Heee! Hivi hawa polisi wa arusha mjini akili zinawatosha kweli?
   
 5. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #5
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,001
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mkuu bora siasa za utoto zinaeleweka, kuliko siasa hizi za CCM.
   
 6. Mbushuu

  Mbushuu JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2011
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 988
  Likes Received: 1,006
  Trophy Points: 180
  Hebu mwaga data mkuu kwa kesi ipi?
   
 7. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kesi ipi iliyomuweka ndani?
   
 8. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,359
  Likes Received: 3,124
  Trophy Points: 280
  hii ndo ccm bana chama chenye dola..

  Demokrasia inaminywa kwa ujasiri wa kifisadi Tz
   
 9. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hilo kosa ni la kupelekwam gerezani kweli? Lazima tuwe serious. Mnaacha kuwapeleka gerezani wezi wanaoendelea kuifilisi nchi yetu kila siku mnamsumbua mwakilishi wa wananchi. U-jinga huu utaisha lini nchi hii?
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Basi mji wa Arusha utakuwa na hali tete sana!

  Lakini bado siamini kuwa Lema anaweza kukosa MDHAMANA kwa Arusha hii!....Hata ingekuwa ni Milioni 50, wengi tu watazichanga fasta!

  Unless kuna sababu zinginezo zinazosababisha wampeleke huko.
   
 11. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #11
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  cku hizi siasa ni DILI tena kubwa.
  ukifanikiwa kutaka jamii through hii kitu umeukata,sema watu hawajatambua
   
 12. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  mleta habari bado hajatuwekea wazi hii habari..kakosa mdhamini kwamba hakukua na watu mahakamani au hadhaminiki?
   
 13. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,996
  Likes Received: 2,651
  Trophy Points: 280
  Kazi ndio inaanza sasa ukiona shida,matatizo,manyanyaso,uonevu vimekuandama ujue mwisho wake umekaribia,tuwekee waraka wake mkuu ili tujue.
   
 14. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Cdhani kama kuna ukweli hapa!ngoja ntajaribu kupata ukweli!najiuliza iweje Lema akose wadhamini hapa?sijui
   
 15. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuuu,sijakuelewa.mwisho hupi wa kufa au siasa
   
 16. Kimbojo

  Kimbojo JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 12, 2009
  Messages: 387
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Toa chanzo cha habari, hata akienda gerezani atatoka kwa remove order kesho. huko ataona kero nyingi za wananchi wasio na hatia waliowekwa ndani.
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ile ni Mahakama inafuata sheria na siyo siasa.
   
 18. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Poa tu! ukombozi wa nchi unakaribia, kwani hata wakoloni waliwaweka ndani wazee wetu waliokuwa wanaipigania nchi hii ili kuwatia hofu wengine. Kazi ni mmoja tu kupambana na ukoloni wa ccm.
  Kamanda Lema atakuwa huru muda si mrefu.
   
 19. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Duh Omutwale angalia wasije sema wewe ni Ngongo.

   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nasikia mtaani walikuwa wanaogopa kuanika madhambi yake kwa sababu ni mheshimiwa sasa nasikia kila kitu kinaanikwa ile mbaya, Aisee jamaa kumbe alikuwa noma.
   
Loading...