Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Nassari Joshua akamatwa na Polisi na kuachiwa kwa masharti

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Nasari S. Joshua amekamatwa na Polisi.

Ni baada ya kupigiwa simu na Issaya Mngulu kuwa anahitajita Polisi na alipofika akaambiwa na RCO kuwa yuko 'under arrest' kwa tuhuma za kushambulia watu huko Monduli na hajaambiwa ni watu gani aliowashambulia...

Nawasilisha...

======
UPDATES:

Nassari ameachiwa baada ya CHADEMA Makao Makuu kuingilia kati lakini kwa masharti kuwa arejee kituoni siku atakayopangiwa kuandika maelezo.

=====

28 July, 2013 - Mtanzania

JESHI la Polisi mkoani Arusha, jana lilimuweka chini ya ulinzi kwa muda wa saa tano Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), kwa tuhuma za kumshambulia aliyekuwa wakala wa CCM, Hussein Warsama, wakati wa uchaguzi mdogo Kata ya Makuyuni, Monduli.

Mbunge huyo hivi karibuni alidai kujeruhiwa wakati akishiriki katika uchaguzi huo, alikwenda kituo cha Polisi mjini Arusha baada ya kupigiwa simu na Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Makao Makuu, Kamishna Isaya Mngulu, aliyeomba waonane na baada ya kufika alijikuta akiwekwa chini ya ulinzi.

Akizungumzia tukio hilo, Nassari alisema Kamishna Mngulu alimpigia simu juzi akiomba waonane, hata hivyo hawakuweza kukutana naye na hivyo kumuomba waonane jana.

Alisema baada ya kushindikana kuonana juzi, huku akiwa hajui alichoitiwa, jana alipokea simu ya Kamishina Mngulu akiomba wakutane, hatua iliyomfanya ashangae kwa kuwa ilikuwa ni siku ya mapumziko.

"Aliponipigia nilishangaa, nikamuuliza mbona leo ni siku ya mapumziko unafanya kazi? Nilidhani ilikuwa ni (issue) jambo la kijamii, hivyo nikaamua kumsikiliza.

"Nikiwa kituoni nilipokelewa na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha (RCO) Nyanda na kisha akaniweka chini ya ulinzi," alisema Nassari kwa mshangao.

Alisema baada ya kuwekwa chini ya ulinzi aliomba kujulishwa makosa yanayomkabili, ambapo alielezwa kuwa anakabiliwa na tuhuma za kushambulia watu wilayani Monduli.

Alisema baada ya kujulishwa tuhuma hizo, ndipo walipomtaka aandike maelezo yake, hatua ambayo aliikataa akidai hakuwa tayari kufanya hivyo kwa sababu hakujua alichoitiwa.

"Nimegoma kuandika maelezo yangu, nimewaambia sina maelezo ya kuandika. Sikujua nakuja kufanya nini polisi.

"Nimewaambia mpaka nitakapokuwa na mwanasheria wangu, nilimtafuta Mabere Marando sikumpata, nikamtafuta Tundu Lissu sikumpata pia.

"Baada ya kuwakosa wote ndipo wakaanza kuniambia niwekwe ndani, nikawaambia sawa, hivyo nikavua saa na miwani yangu.

"Nilipovua vifaa vyangu, wakabadilisha mawazo wakasema nipelekwe Monduli. Askari mwingine akasema gari haina mafuta, nikiwa nasubiria wafanye nini Kamishna Mngulu aliwasili na kutoa maagizo ya kunitaka nijidhamini mwenyewe.

"Tangu saa 2 asubuhi walikuwa wananishikilia hadi Saa 6 mchana walipoamua kuniachia kwa kujidhamini mwenyewe, wakisema eti watanipigia simu," alisema Nassari.

Nassari alionyesha kushangaa hatua ya polisi kumuweka chini ya ulinzi kwa tuhuma za kumshambulia Warsama, huku akidai kuwa yeye ndiye aliyenusurika kutekwa na kupigwa na watu aliodai kuwa ni wafuasi wa CCM siku ya uchaguzi huo, ambao Nassari alikwenda kwa ajili ya kusimamia na kuwa wakala wa mgombea wa Chadema, Japhet Sironga.

Hata hivyo kwa upande wake RCO Nyanda, alipotafutwa kuzungumzia suala hilo aligoma, akidai kuwa atafutwe Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ambaye ndiye msemaji wa jambo hilo.

"Naelekea Dodoma, mtafute RPC ndiye msemaji wa Polisi Mkoa," alisema RCO Nyanda kwa njia ya simu.

Taarifa za kiintelijensia zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa Nassari alianza kutafutwa na askari wa polisi tangu Julai 23, mwaka huu, huko wilayani Arumeru, ambapo jeshi hilo lilikuwa likisubiri amalize matibabu kisha limhoji.

Wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli, Nassari anadaiwa kumpiga wakala wa CCM aliyejulikana kwa jina la Warsama au Msomali.

Ilidaiwa kuwa hatua hiyo iliibua hisia kwa vijana wa Kimasai (Morani), walioanza kumsaka mbunge huyo ambapo alijikuta akijeruhiwa shingo na hivyo kusababisha kulazwa Hospitali ya Selian Arusha, kisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
 
Polisi hao wanaendelea na ujinga wao wakidhani kuwa wataiokoa CCM. Baada ya kwenda Airport kukamata wahalifu wanaopita na madawa ya kulevya baada ya kutumwa na viongozi wa juu wa Serikali wanazubaa na kuwakimbilia wanasiasa.

Shime waTanzania kwanini tusiungane kwa njia salama kupinga udhalimu huu wa Jeshi la Polisi. Leo WaTZ wenzetu watatu wanakamatwa Hongkong na wamepita Airport zetu ambazo hivi vyombo vya usalama vipo.

Mi kwa sasa nimepoteza imani na vyombo vyote vya usalama kasoro jeshi la Magereza na JWTZ kidogo
 
Hivi hawa Polisisiem hawajajifunza kilichotokea nchi za kaskazini mwa Afrika?Hivi hawaijui nguvu ya umma?hivi ni kesi ngapi wameshinda mahakamani za aina hii?.Time will tell,no more no less.
 
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Nasari S. Joshua amekamatwa na polisi, baada ya kupigiwa simu na Issaya Mngulu kuwa ana hitajita polisi na alipo fika plisi akaambiwa na RCO kuwa yuko 'under arrest' kwa tuhuma za kushambulia watu huko Monduli na haja ambiwa ni watu gani aliowashambulia....

Nawasilisha...

Kupigwa apigwe yeye na ndani awekwe yeye.. mbona majanga....!! Muendelezo wa amri ya Pinda.... mbona hakuna rangi tutaacha ona mwaka huu...!?? !
 
polisi, polisi, polisi!!!!
Angalieni sana maana kitu kinachowafanya waelevu waichukie historia ni kwa sababu siku zote inaeleza ukweli, hata iwe baada ya miaka mingapi. Na historia inawachukia wanadamu wajinga bila kujali wametumwa au wamejituma wao.
 
panapofuka moshi...? ngoja vijana wetu wamalize mafunzo yao ya RED :painkiller:BRIGADE ili tuweze pata ulinzi madhubuti dhidi ya magumashi kama haya ya rijeshi ra porisi. kuna siku nyie mapolisi mtachezea :boxing: na :fencing:.
 
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Nasari S. Joshua amekamatwa na polisi, baada ya kupigiwa simu na Issaya Mngulu kuwa ana hitajita polisi na alipo fika plisi akaambiwa na RCO kuwa yuko 'under arrest' kwa tuhuma za kushambulia watu huko Monduli na haja ambiwa ni watu gani aliowashambulia....

Nawasilisha...

Yupo hapo kituo kikuu mkuu?
 
Hivi hawa Polisisiem hawajajifunza kilichotokea nchi za kaskazini mwa Afrika?Hivi hawaijui nguvu ya umma?hivi ni kesi ngapi wameshinda mahakamani za aina hii?.Time will tell,no more no less.

Hawa wanatuandaa kinamna, wameshatuzoesha vipigo na mabomu ... huóni saivi vibaka wanaenda kupora vituoni, imebaki nini hapo..!?
 
shame upon them, ngoja tuna video yote namna wasomali walivyo mpiga Nassari.
utawala umefitinika daima hawana lolote shame upon them policccm
 
Back
Top Bottom