Mbunge Solwa aipa Mtihani Sheria Gharama za Uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Solwa aipa Mtihani Sheria Gharama za Uchaguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mgoyangi, Mar 24, 2010.

 1. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #1
  Mar 24, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya Mwaka 2009 iliyosainiwa kwa mbwe mbwe na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete ambayo ina lengo lake ni kudhibiti vitendo vinavyoonekana kuwa rushwa, imetahiniwa na Mbunge wa Solwa CCM - Ahmed Salum, ambaye ametoa magari mawili ya wagonjwa kama msaada kwa wananchi ikiwa ni siku chache baada ya sheria hiyo kutangazwa kuwa ianze kutumika.

  Akifungua Mkutano wa kazi wa mwaka wa TAKUKURU, jijini Mwanza, Rais Kikwete katika hatua ya kutangaza nia yake ya kidhinisha sheria hiyo kwa mbwembwe alihoji vitendo kama hivi, kwamba kwa nini iwe sasa hivi, wakati tukielekea uchaguzi mkuu na isiwe kabla.

  Lakini Mbunge huyu wa Solwa kaamua kuweka pamba Masikioni na kutoa misaada hii, ukiacha kampeni yake ya kuingiza wananchama wapya kwa kuwanunulia kadi na semina za hapa na pale na posho mbali mbali kwa wapambe.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Nani kasema hiyo sheria inazuia kutoa misaada sasa hivi? Hiyo sheria haimfungi mtu yeyote (mgombea au otherwise) kutoa misaada au kufanya mambo ambayo angeyafanya kama mbunge au mwananchi wa kawaida.
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,831
  Trophy Points: 280
  MJJ,
  Kwenye thread mama nilikuuliza hili...suala ni timing ya huu msaada...why not next year?
   
 4. Devils Advocate

  Devils Advocate Member

  #4
  Mar 24, 2010
  Joined: Dec 16, 2009
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sheria inasema kuwa misaada inayotangazwa na kupingwa ni ile iliyo na connection ya moja kwa moja na kupata ugombea ubunge( actually sheria inasema inayopokelewa au kutolewa siku 30 kabla ya uchaguzi).

  That means kwa sasa mbunge ametoa msaada kama mbunge wa jimbo na huo ni wajibu wake kikatiba. Tulipowachagua matajiri watuongoze tulitaka watoe vitu kama magari wakati unapofika. I see no harm in him doing what he did.
   
Loading...