Hii ni hatari kubwa, wabunge wengi wa CCM wanapochangia hoja bungeni mawazo yao huwa ni jinsi gani ya kuwadhibiti wana chama wa CHADEMA, CUF na vyama vingine vyenye upinzani wa kweli. Lakini atambue kuwa kuna maandamano mengine ambayo hayafungamani na siasa bali maisha ya kila siku, mfano huko jimboni Bumbuli kulitokea mauaji ambapo polisi waliwapiga risasi waandamanaji, lakini wananchi wa jimbo hilo karibu ya wote ni wanachama na wakereketwa wa CCM, Pia kule mkoani Ruvuma ilikuwa hivyohivyo, Na hivi majuzi wajenzi wa barabara ya magari yaendayo kasi Dar es salaam waliandamana kwa ajili ya maslahi yao, bahati nzuri hakuna raia aliyepigwa risasi, ninao uhakika kuwa yale maandamano hayakuwa na kibali cha polisi, kwa hiyo kama huyu mheshimiwa angelipewa bunduki naamini angeliwashoot wote bila kuuliza sababu ya wao kuandamana.