Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Aliyekuwa mume wa nyota wa Filamu za Bongo, Wastara Juma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge (CCM), Zanzibar, Sadifa Juma ameibua jambo zito miongoni mwa jamii akidai kuwa, mtalaka wake, Wastara Juma amekuwa akimroga.
Madai hayo aliyatoa Alhamisi iliyopita baada ya gazeti hili kumuuliza habari zilizoenea kwamba, amemuangukia Wastara akitaka warudiane kwani yaliyopita si ndwele.
Sadifa alisema kuwa, aligundua hilo la kurogwa baada ya Wastara kuondoka nyumbani kwake na kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa, amepewa talaka mbili.
Akizungumza kwa dakika 25, Sadifa alikwenda mbele zaidi kwa kusema: “Ukimwangalia Wastara harakaharaka unaweza kusema ni mwema sana lakini hana wema wowote. Hivi Wastara ni wa kuniroga mimi kweli?”
Alipoulizwa kuwa amepata wapi hizo habari za kulogwa Muheshimiwa akasema:
“Niliambiwa na watu wawili, mmoja dereva wangu, mwingine ni kijana wangu. Tena hao wameniambia juzi tu baada ya mambo kuharibika. Wakasema kuna siku walikwenda na Wastara kwa huyo mganga. Wastara alikuwa na ndugu yake mmoja.
Walipofika, vijana wangu hawakuingia. Kwa hiyo hawakujua walifuata nini! Mara ya pili akawaambia kuwa, wamekwenda pale kuchukua dawa eti ili isaidie ndoa yetu iwe na amani na mimi niache macho juujuu. Akapewa kombe kama unalijua kombe, aitie kwenye maji anipe ninywe."
“Sasa wale vijana wangu wakamshauri Wastara kwamba, kama maji hayo ya kombe atanipa yeye ninywe nikigundua itakuwa balaa, wakamwambia awape wao ndiyo wanipe mimi ninywe ili nikijua wataniambia ni dawa ya kukinga mwili. Lakini wao hawakunipa na wanayo mpaka leo (juzi, Alhamisi)!”
Akizungumzia suala la kupigia magoti Wastarra ili warudiane Sadifa alisema,
“Kwanza hizo habari si za kweli. Mimi wale mashemeji zangu waliniomba gari wamfuate ndugu yao. Nilitoa kwa ubinadamu tu, nikawawekea na mafuta.” na akadai kuwa mtu anayejitambulisha kuwa babu yake Wastarra sio babu yake ni bwana ake.
“Yule si babu yake Wastara. Yule ni bwana’ake kama hamjui. Mimi juzi tu ndiyo baadhi ya ndugu zake wameniambia ukweli kwamba yule babu, si babu yao bali alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu Sajuki (Juma Kilowoko, aliyekuwa mume wa Wastara).”
“Sasa wewe jiulize, mkeo mnagombana, anakwenda kwa rafiki wa marehemu mume wake. Kwa nini asiende kwao? Kule anakaa kufanya nini? Yule Babu ndiye amenirithi mimi kwa Wastara.”
“Kuna wakati fulani Wastara aliumwa, dokta akamwambia atulie kwa muda asitembeetembee. Kesho yake akaniambia anakwenda Morogoro kwa huyo babu yake. Nilimkatalia, akalazimisha, akaenda. Sasa mke anawezaje kwenda mahali bila ridhaa ya mumewe?
“Alipokuwa kule, nikawa nampigia simu hapokei kwa muda wa siku tatu. Siku moja nyumbani alikuja kijana wake anayemfanyia biashara, nikamwambia Wastara yupo Morogoro, akampigia simu mbele yangu, akapokea, wakaongea. Walipomaliza, mimi nikampigia, hakupokea!”
SIKU YA WASTARA KUONDOKA NYUMBANI
“Mimi sikuwahi kutoa talaka kama Wastara anavyoeneza hizi habari. Siku hiyo anaondoka nyumbani mimi nilikwenda kwenye kamati za bunge, wakati naingia akanipigia simu na kusema anataka tuongee.
“Nilimwambia tutaongea baadaye yeye akataka muda uleule, nikakataa. Akasema anachotaka yeye nimpe shilingi milioni kumi afanye biashara. Nikamwambia sina, ndiyo akaondoka. Sasa jamani, mkeo kama anataka pesa ukamwambia huna ndiyo aondoke nyumbani? Mimi naona alifuata pesa tu.
Source: Gazeti letu pendwa