Mbunge Prof. Jay aangua kilio hadharani, baada ya mauaji yaliyofanywa na polisi jimboni kwake

Kwahyo Km Ni Gaidi Umwue?Kuna Haja Gani Yakumpiga Risasi Mtu Ambaye Hana Silaha?Tunakoenda Tanzania Nikama Tumepotea
Sabab n muislam ....Yule kijana bodaboda simkumbk alikamatwa na Bomu akilipua mkutano wa chadema hakuitwa gaid na hajulikan kes imeishia wap
 
Jeshi hili limejaa watoto wa mjomba, vinginevyo haiwezekani mtu aliyafauru vyema mitihani yake ya upelelezi akimbilie silaha ya moto kwa mwanafunzi anayeishi kijijini. Ni kashfa tu. Polisi walipaswa kujikita kwenye upelelezi kijijini hapo mpaka wajiridhishe kama kweli mlengwa ni musika ama laa na bado walikuwa na uwezo wa kumtia mbaroni ili kuendeleza upelelezi ili ikibidi kupata taarifa zaidi.lakini kilichofanyika ni aibu kwa jeshi letu
Utakuta ni wivu wa mapenzi tu
 
Hana haja ya kulia. Haya mambo ni ya kitaalam sio siasa kwahiyo awaachie wataalam.
Utaalamu wa kuua? Vyombo vya sheria vipo na vina kazi hiyo ya kutoa haki. Kama ushahidi umejitosheleza aende mahakama lakini ukimuua utajuaje kama kweli ni mhalifu.Usiongee hivyo kwakua sio Ndugu yako au mwanao.
 
hivi magaidi wa kibiti walikua wanataka nini? ....mana imeshakua sababu ya kufanya mauaji ya watu wasio na hatia ....mwanafunzi atoke Mbeya akafanye ugaidi kibiti kwanini asifanyie kwao Mbeya....ripoti ya mahudhurio nina uhakika haitaonyeshwa...watafanya kama kwa lissu zile CCTV camera walivyozitoa kabisaa

claytonx

Mkuu,
Mbeya na kibiti mbona ni ulimi na meno kabisa!!

Kumbuka, Aliyetoka Dodoma , akenda Mwanza kisha akavuka mpaka Kenya kule kwenye campus ya Garisa na kufanya mauaji akiwa na magaidi wenzake?

Tena naye alikuwa mwanafunzi wa secondary age yake kati ya 17-19 years old!!

Ugaidi ni zaidi ya jinsi unavyoweza kuona tukio linapotokea.

Ila mifumo yake ni complex and sophisticated sana.

Kwa hiyo, akionekana tu gaidi anapewa ganzi ya milele.

Polisi kazi yenu ni nzuri sana.

Tunahitaji kuwa na amani nchini Tanzania
 
Chukuen mwili mkazike n makosa kwa sheria ya kiislam kuukalisha mwili mda wote huo bila kuzika ...hatutarajii haki kutoka kwa mataghut ....wameshakubaliana kuuwa waislam ila watalipa kila tone la damu wanalomwaga
 
Mk
Halima, we baki kwenye kusasambua.
Kijana wa miaka 17 ni mwanajeshi kabisaaa...huko kongo, somalia na sudani...madogo wa miaka 10-17 wameamgamiza maelfu ya watu. Huo umri usikuzibe macho.
Hivi we hujiulizi, ilikuwaje katika mazingira ya kitanzania, polisi waende kumwandama kijana wa miaka 17 hadi huko kijijini kwao?
Unadhani walifunga safari yote hiyo kwa bahati mbaya?
Kudhani, kudhani, kudhani... we mwenyewe unadhani polisi walifunga safari yote hiyo kwenda kuua mtu? Ndio unadhani hivyo??

Huyo polisi anayeongea hapo kasema amedhaniwa na bado upelelezi unaendelea sasa kumdhania mtu ndio umuue?
 
Maxmizer ,

Mkuu mtu akitajwa tu kuwa gaidi hapo tunazungumzia vifo vya watu wasiokuwa hatia kutokea siku chache zijazo.

Bora aondolewe tu mapema.


Polisi wanafanya kazi nzuri sana. Tukicheka na nyani tutavuna mabua mapemaaaa asubuhi kabla hakujakucha.

Hivyo, ni bora wapumzishwe kwa amani magaidi wote kabla hatujaanza kukimbia miji na vijiji kama ilivyo Nigeria, Cameroon, Somalia, na Kwengineko kote.

ama kweli msiba uusikie kwa jirani tu
 
Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ameangua kilio hadharani kwenye mkutano aliokuwa amefanya na wananchi wa kijiji cha Ruhembe wilayani Kilosa na kuwaomba Waziri wa mambo ya ndani na waziri mkuu wachukue hatua kabla ya wananchi kujichukulia hatua

Wananchi hao pia waligoma kuzika mwili wa mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Salim Said Mheka mwenye umri wa miaka 17 aliyeuawa na polisi wa kitengo maalumu kwa madai kuwa alikuwa ni mhalifu wa Kibiti

Kijana huyo alimaliza kidato cha nne katika shule ya sekondari Ruhembe,

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro amesema kijana huyo alikuwa anajihusisha na ugaidi



Dah! Kwa hiyo, ukishatuhumiwa tu ruksa kuuawa na polisi?
 
Hana haja ya kulia. Haya mambo ni ya kitaalam sio siasa kwahiyo awaachie wataalam.
Kwa gaid n nan na kwa mujib wa nan ....if kuua ndo ugaid bas wao n magaid wakubwa walivoua mamia ya waislam mwembechai ....... Tuwaachie wataalam ambao wao ndo wamemuua ....
 
Sabab n muislam ....Yule kijana bodaboda simkumbk alikamatwa na Bomu akilipua mkutano wa chadema hakuitwa gaid na hajulikan kes imeishia wap

ya na wameua waislam wengi sana, kwa style hiyo hiyo hadi yule mwanafunzi wa chuo waliua kama huyo
 
ama kweli msiba uusikie kwa jirani tu

Saju b ,
Mkuu,
Tofautisha msiba wa mgonjwa au ajali na msiba wa wayi kama vile mwizi, jambazi, au gaidi.

Naelewa uchungu wa misiba ila siyo wa wakosefu na magaidi.

Polisi kazi nzuri. Tunahitaji amani nchini Tanzania kuliko wakati wowote ule wa kuumbwa hii dunia.
 
claytonx

Mkuu,
Mbeya na kibiti mbona ni ulimi na meno kabisa!!

Kumbuka, Aliyetoka Dodoma , akenda Mwanza kisha akavuka mpaka Kenya kule kwenye campus ya Garisa na kufanya mauaji akiwa na magaidi wenzake?

Tena naye alikuwa mwanafunzi wa secondary age yake kati ya 17-19 years old!!

Ugaidi ni zaidi ya jinsi unavyoweza kuona tukio linapotokea.

Ila mifumo yake ni complex and sophisticated sana.

Kwa hiyo, akionekana tu gaidi anapewa ganzi ya milele.

Polisi kazi yenu ni nzuri sana.

Tunahitaji kuwa na amani nchini Tanzania
umenena vema ...magaidi wa Kenya wanataka Kenya iondoe majeshi Somalia... hawa wa kwetu wanataka nini?
 
Hakuna haja ya vyama vingi...bado nchi haiko tayar....kila mda siasa tuuu...hakuna polisi mjinga wa kwenda kumpiga risasi kijana wa miaka 17 ....!!! Kama wamejiridhisha the only solution is to kill them...huwez cheka na kifo

This kind of reasoning only leads to vicious consequences.
 
Back
Top Bottom