Mbunge Prof. Jay aangua kilio hadharani, baada ya mauaji yaliyofanywa na polisi jimboni kwake

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,832
18,827
Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ameangua kilio hadharani kwenye mkutano aliokuwa amefanya na wananchi wa kijiji cha Ruhembe wilayani Kilosa na kuwaomba Waziri wa mambo ya ndani na waziri mkuu wachukue hatua kabla ya wananchi kujichukulia hatua

Wananchi hao pia waligoma kuzika mwili wa mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Salim Said Mheka mwenye umri wa miaka 17 aliyeuawa na polisi wa kitengo maalumu kwa madai kuwa alikuwa ni mhalifu wa Kibiti

Kijana huyo alimaliza kidato cha nne katika shule ya sekondari Ruhembe,

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro amesema kijana huyo alikuwa anajihusisha na ugaidi

 
Mwambie asilie maana vijana wamekuwa waktili kuliko umri wao sasa na asishangae kijana kafanya mauwaji makubwa sana.
Ndugu yangu kijana kamaliza form four mwezi uliopita , sasa hayo mauaji ya kibiti alikuwa anafanya saa ngapi ?

Kama kweli polisi wanafanya intelejensia ya kutosha, wangejua huyu ni mwanafunzi wangeangali attendency register alikuwa anafika shule kila siku, kama anamiliki simu je minara ya kibiti imesoma kwenye simu yake??? ... Tukiri wazi jeshi la polisi halina ueledi wa kutosha wanatumia nguvu nyingi Sana kwenye kwenye mambo ya kutumia akili
 
Si jambo jema kumuua huyo kijana ikiwa ulikuwepo uwezekano wa kumkamata uyo mtuhumiwa na kwa mujibu wa iyo taarifa bado wapo vijana wengine eneo hilo . Naomba polisi wafanye juhudi za kuwakamata hao watuhumiwa bila kutumia nguvu kupita kiasi, mnaweza kujikuta mnajaribu kutatua tatizo mmoja na kuanzisha jingine kwani wananchi si rahisi kuamini kama mtuhumiwa alihusika na mauaji ya kibiti.
Wazazi nasi tunatakiwa kufuatilia nyendo za watoto wetu na kuchukua hatua.
 
Ao nahis walikua askari wa TANAPA, maana wenyewe khusu kufyatua risas co ishu xana, coz wanafnya kaz na wanyama na majangiri. Ila kma polis nao wameanza kuwinda watu na mtutu mtaani, hata kma ni wahalifu tunahtaj kupaza sauti, maana hata mhalifu chini ya katiba anahaki ya kuishi.
 
Hee...yaani Tanzania hii imefika hatua mbaya,yaani mtu anapigwa risasi kwa kudhaniwa ni gaidi!

Ukimsikiliza RPC hapo ndio utaona hatupo salama hata kidogo....anasema alidhaniwa,na anasema kuna mwingine anadhaniwa kuwa ni gaidi amekamatwa na anahojiwa kuona kama kweli ni mharifu au laah! Hii inamaanisha polisi hawana uhakika sasa.

Balaa hii sasa.
 
Ndugu yangu kijana kamaliza form four mwezi uliopita , sasa hayo mauaji ya kibiti alikuwa anafanya saa ngapi ?
Halima, we baki kwenye kusasambua.
Kijana wa miaka 17 ni mwanajeshi kabisaaa...huko kongo, somalia na sudani...madogo wa miaka 10-17 wameamgamiza maelfu ya watu. Huo umri usikuzibe macho.
Hivi we hujiulizi, ilikuwaje katika mazingira ya kitanzania, polisi waende kumwandama kijana wa miaka 17 hadi huko kijijini kwao?
Unadhani walifunga safari yote hiyo kwa bahati mbaya?
 
Hakuna haja ya vyama vingi...bado nchi haiko tayar....kila mda siasa tuuu...hakuna polisi mjinga wa kwenda kumpiga risasi kijana wa miaka 17 ....!!! Kama wamejiridhisha the only solution is to kill them...huwez cheka na kifo
 
Ni mara ngapi polisi hawa hawa wanatuambia wananchi tusicjichukulie sheria mikononi pindi tunapowakamata wahalifu? imekuwaje wao wamuue mtu wanaemhisi ni mhalifu? Au alikuwa anajibizana nao kwa risasi? Hawa askari ni taka taka kbs, hawafai hata kidogo!
 
Back
Top Bottom