Mbunge Peter Msigwa awataja waliohusika kununua Madiwani Iringa, vilitumika vifaa vya Australia

Wataalamu wetu hawajaweza kutengeneza vifaa hivyo hapa Tz? Kusifu vya wenzetu th kama vile ndio vinahalalisha ushahidi.
Kutengeneza vifaa si sera za viwanda inayoongelewa majukwaani na wanasiasa uchwara
 
Kwa hiyo Msigwa nae ana video..?

Hivi ukishapeleka ushahidi TAKUKURU nani mwenye wajibu wa kufungua shauri.?

Na kwa nini Msigwa hajakabidhi ushahidi wa video TAKUKURU.?

Halafu tofauti ya vifaa vya AUSTRALASIA na UK ni ipi.....kwamba vya kwa Msigwa ndio bora zaidi ama ushahidi wa Msigwa ndio bora zaidi kuliko wa Lema na Nasari.?

Au anatafuta kiki za pikipiki....
Wewe nawe!!! Soma uelewe. Anasema ametoka TAKUKURU kukabidhi. Rushwa ni jinai, jalada linafunguliwa na Jamhuri sio Msigwa
 
Tumetaja nchi vilikotengenzwa vifaa vilivyorekodi kuepuka msije sema vifaa visivyojulikana kama mlivyozoea chama cha fisiemu
 
46805424a52e82b240855a3fc1aa00ad.jpg
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa biashara ya kununua madiwani wa CHADEMA pia ilifanyika Iringa Mjini na kusema kuwa wao walitumia vifaa kutoka Australia kubaini hilo.

Peter Msigwa amesema hayo leo jijini Dar es salaam baada ya kutoka Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambapo walikwenda kuwasilisha ushahidi wa rushwa dhidi ya kununuliwa kwa madiwani hao na wateule wa Rais John Pombe Magufuli.

"Iringa Mjini biashara nayo ilifanyika. Nina ujasiri mkubwa kwamba muhusika mkuu wa biashara ya kununua madiwani Iringa Mjini ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya pamoja na baadhi ya Polisi, hiyo mliona 'Episode' ya Arusha vilitumika vifaa vya Uingereza kule Iringa tulitumia vifaa vya Australia na sisi tutafungua jalada kama ambavyo Mkurugenzi wa TAKUKURU ametushauri.

"Kwa hivyo tusubiri sababu tumekabidhi kwenye korido za Serikali na tunataka sheria zichukue mkondo wake huu uongo uongo wa kusema watu wanaunga mkono utendaji wa Serikali tunataka ufike mwisho ili watu wakae kwenye nafasi zao kwa haki na jinsi ambavyo watu waliamua kuwachagua". alisema Mchungaji Peter Msigwa.

Chanzo: East Africa Radio

Its apparent that opposition kama ruling party nako kuna serious problems. Tunajua ukishakuwa kwenye power matatizo ni sehemu ya kazi zako, kuna a lot of misunderstanding, chuki, wivu, mizengwe na kila jambo ambalo litaonesha kuwa huwezi kuongoza. Opposition nao wanakuja na evidences ambazo ni confusing..... hebua angalia evidences ambazo zinaletwa mbele ya watu jinsi zilivyo
 
Tumia hivyo vyombo kuiba kura,kupiga kampeni na kuchukua uraisi.

Siyo vyombo tu kufuatilia ununuzi wa madiwani.
 
Hawa wapinzani kupata kura/kula za raia ni kuwapa wanachohitaji, yaani, maji, umeme, huduma za afya, elimu, miundo mbinu n.k. Sasa kama wewe mbunge wa upinzani unakomalia mambo kama haya sidhani kama unamtosheleza raia, wakijitihadi kwa yaliyosemwa mbona fresh tu, sasa wao kutwa kulalamika, vifaa sijuwi, kununuliwa, sijuwi nini..Ndio wanazidi kuonekana wababaishaji..Wabadilishe mbinu tu..
 
Back
Top Bottom