Mbunge Peter Msigwa awataja waliohusika kununua Madiwani Iringa, vilitumika vifaa vya Australia

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa biashara ya kununua madiwani wa CHADEMA pia ilifanyika Iringa Mjini na kusema kuwa wao walitumia vifaa kutoka Australia kubaini hilo.

Peter Msigwa amesema hayo leo jijini Dar es salaam baada ya kutoka Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambapo walikwenda kuwasilisha ushahidi wa rushwa dhidi ya kununuliwa kwa madiwani hao na wateule wa Rais John Pombe Magufuli.

"Iringa Mjini biashara nayo ilifanyika. Nina ujasiri mkubwa kwamba muhusika mkuu wa biashara ya kununua madiwani Iringa Mjini ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya pamoja na baadhi ya Polisi, hiyo mliona 'Episode' ya Arusha vilitumika vifaa vya Uingereza kule Iringa tulitumia vifaa vya Australia na sisi tutafungua jalada kama ambavyo Mkurugenzi wa TAKUKURU ametushauri.

"Kwa hivyo tusubiri sababu tumekabidhi kwenye korido za Serikali na tunataka sheria zichukue mkondo wake huu uongo uongo wa kusema watu wanaunga mkono utendaji wa Serikali tunataka ufike mwisho ili watu wakae kwenye nafasi zao kwa haki na jinsi ambavyo watu waliamua kuwachagua". alisema Mchungaji Peter Msigwa.

Chanzo: East Africa Radio
 
Kwa hiyo Msigwa nae ana video..?

Hivi ukishapeleka ushahidi TAKUKURU nani mwenye wajibu wa kufungua shauri.?

Na kwa nini Msigwa hajakabidhi ushahidi wa video TAKUKURU.?

Halafu tofauti ya vifaa vya AUSTRALASIA na UK ni ipi.....kwamba vya kwa Msigwa ndio bora zaidi ama ushahidi wa Msigwa ndio bora zaidi kuliko wa Lema na Nasari.?

Au anatafuta kiki za pikipiki....
 

Mpaka watage safari hii
 
Wataalamu wetu hawajaweza kutengeneza vifaa hivyo hapa Tz? Kusifu vya wenzetu th kama vile ndio vinahalalisha ushahidi.
 
Tulizana acha kukuru kakara! Chama cha wahuni mafisadi na wauaji rushwa ni jadi yenu.



 
Kwani kuna secret camera zinazotengenezwa Tanzania hadi aseme ni vifaa kutoka Australia sijui Uingereza?
 
Ama kweli watoa rushwa vs dola yao

Nyoka atakula nyoka?

Mbwa atakula mbwa?
 

Tofauti ni mtengenezaji
 

Tulia. Acha kurukaruka kama kicheche.
 
Reactions: BAK
Ma limbukeni hao akili ndogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…