Mbunge Ole Sendeka atishia kumharibia Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Ole Sendeka atishia kumharibia Rais Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ochu, Oct 31, 2009.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mbunge Ole Sendeka atishia kumharibia Rais KikweteMbunge wa Simanjiro,Christopher Ole Sendeka, ametishia kuiharibia serikali ya Rais Kikwete iwapo itaendekeza hoja ya "posho mbili" ili kudhalilisha wabunge.Ataka serikali iwakamate kwanza nafisadu badala ya kuibua hoja ya 'posho mbili'

  Daniel Mjema, Dodoma

  SUALA la wabunge kuhojiwa na Takukuru, juzi lilichukua sura mpya baada ya Mbunge wa Simanjiro,Christopher Ole Sendeka kugeuka msumari wa moto kwa serikali akitaka iwakamate kwanza wabunge mafisadi wanaohusika na kashfa za Kagoda na Deep Green Finance kabla ya kuwaandama wabunge.

  Katika kashfa hizo, Kampuni ya Kagoda Agriculture inadaiwa kuchota kifisadi Sh40bilioni kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wakati Deep Green Finance inadaiwa kukwapua Sh9 bilioni kutoka kwenye akaunti hiyo.

  Kwa mujibu wa taarifa za kutoka ndani ya kikao cha faragha cha wabunge wa CCM kilichofanyika mjini Dodoma,inaelezwa kuwa Sendeka alihoji kama kweli agizo la kuwahoji wabunge lilitolewa na Ikulu.

  Huku akishangiliwa na wabunge wengine, Sendeka aliibana serikali akitaka kujua iwapo Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah ametumiwa na mafisadi au kweli katumwa na Rais Jakaya Kikwete kuwadhalilisha wabunge.

  Sendeka alitoa kauli hiyo juzi usiku mjini Dodoma katika kikao cha faragha cha wabunge wa CCM kilichofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa chini ya Katibu wa Kamati ya Wabunge wa chama hicho, Ali Ameir na taarifa zake kulifikia gazeti hili.

  ‶Kuna mambo mawili ambayo tunayaona katika suala hili; ama Dk Hoseah anatumiwa na mafisadi au ametumwa na rais kuwadhalilisha wabunge kwa sababu Takukuru siyo taasisi inayojitegemea bali iko chini ya rais,※ chanzo chetu kilimkariri Sendeka akisema ndani ya kikao hicho.

  Alisema hawaelewi na hawaamini kama rais ndiye ameagiza wabunge wadhalilishwe, lakini kama ndivyo awaeleze ili nao waende majimboni kwa wananchi kuwaeleza mabaya ya serikali wanayoyafahamu.

  Huku akipigiwa makofi na wabunge karibu wote waliohudhuria kikao hicho, Ole Sendeka alisema baada ya kuwaeleza wananchi, wao ndio watapima ni nani wasafi kati ya wabunge, serikali na Takukuru.

  Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho, zimedokeza kuwa Sendeka alitaka Rais Kikwete azungumze na Mkurugenzi wa Takukuru kabla mambo hayajaenda kombo.

  Kikao hicho kilikuwa mahususi kwa kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM kutoa taarifa ya ujio wa kamati ya Mzee Ali Hassan Mwinyi, lakini Ole Sendeka akakitumia kuibua suala la uchunguzi huo wa Takukuru.

  ‶Tunafahamu Hoseah anajua humu ndani wapo wanaohusika na kashfa za Kagoda, Meremeta na Deep Green Finance awakamate kwanza, tuone kama kweli anakerwa kwa dhati na tatizo la rushwa,※alikaririwa Ole Sendeka.

  Mbunge huyo machachari alisema endapo suala ni malipo ya posho kwa wabunge, iundwe tume huru ya pamoja kuchunguza na uchunguzi huo ufanyike kwa mihimili yote mitatu ya dola kwa maana ya Bunge, Mahakama na Serikali.

  Chanzo hicho cha habari kimedokeza kuwa Ole Sendeka alisema endapo uchunguzi huo utabaini wabunge wamekula fedha haramu, wako tayari kuzirejesha lakini, akasema nao watatumia nguvu ya umma kupasua mabomu ya serikali.

  Alidai kuwa hata yeye Hoseah na taasisi yake (Takukuru) ilipokuwa inataka Bunge lipitishe muswada wa marekebisho ya Sheria ya Rushwa, aliandaa semina kwa wabunge na kuwalipa posho kama ilivyo kwa taasisi nyingine.

  Ole Sendeka alimtaka Dk Hoseah kama ana hoja ya msingi katika uchunguzi wake asubiri kwanza Bunge limalizane na suala la Richmond wiki ijayo, ndio waendelee na uchunguzi wao.

  ‶Baada ya uchunguzi wao watupigie mahesabu kama kuna fedha haramu tumekula, tupo tayari kuzirejesha lakini uchunguzi huo uendelee pia kwa mihimili mingine ya dola ambayo ni serikali na mahakama," alikaririwa Sendeka.

  Katika kikao hicho Ole Sendeka alihoji ni mkuu wa mkoa gani au waziri anayesafiri kwenda wilayani au mikoani ambaye hata kama amelipwa posho stahiki, husafiri na chakula chake bila kukirimiwa na halmashauri anakokwenda.

  Habari kutoka katika kikao hicho, zimezidi kueleza kuwa Ole Sendeka aliitaka serikali kuwasiliana na Spika wa Bunge au katibu wake ili kupata ufafanuzi wa posho hizo vinginevyo iwaite wabunge wote na kuwahoji.

  Wakati mvutano huo ukiendelea, zipo taarifa kuwa Takukuru imekuwa ikijiandaa kuwakamata baadhi ya wabunge siku moja au siku ya mjadala wa Richmond ikiwa ni mbinu ya kudhoofisha mjadala huo.

  Habari zilizowakariri baadhi ya wabunge zinadai kuwa mpango huo umeandaliwa mahususi na wapo wabunge kwa majina ambao wanaandaliwa mpango wa kuwakamata, ila wanasubiri kwa hamu hilo litokee.

  Wiki hii, Mbunge wa Kyela, Mwakyembe alinukuliwa na vyombo vya habari akisema hatua hiyo ya Takukuru kutaka kuwahoji wabunge sasa, ina lengo la kuwafunga midomo wasijadili kashfa ya Richmond.

  Alhamisi wiki hii, Spika wa Bunge,Samuel Sitta alisema wabunge wataendelea kupokea posho kwa kuwa ni halali na serikali ilileta bajeti zake bungeni na zikapitishwa na kuitaka Takukuru ishughulikie mambo ya msingi.

  Msuguano huo kati ya Serikali na Bunge umekuja wakati wiki hii Bunge linatarajiwa kujadili ripoti ya serikali ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge yanayoitaka serikali kutekeleza maazimio yote bila kusitasita.

  Miongoni mwa maazimio hayo ya Bunge ni kuwajibishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Hoseah kwa namna alivyoficha ukweli kuhusu Richmond hadi kamati ya Bunge ilipogundua uozo mkubwa.

  Kashfa ya Richmond ndiyo iliyosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu akifuatiwa na mawaziri wengine wawili, Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi ambao waliitumikia Wizara ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti wakati wa mchakato wa zabuni iliyoipa ushindi kampuni hiyo.

  Pamoja na kujiuzulu huko maazimio ya Bunge yalitaka pia kuwajibishwa kwa aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali, Johnson Mwanyika na katibu mkuu wa Wizara ya
  Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi ambao wamestaafu kwa mujibu wa sheria. Wabunge wanataka suala la utekelezaji wa maazimio hayo ya Bunge limalizike katika Bunge hili la 17, lakini hadi jana kulikuwa na usiri mkubwa wa lini ripoti hiyo ya serikali ya wa maazimio hayo itawasilishwa bungeni.

  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=15689
   
 2. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Kutambiana sasa kumekuwa kwingi nadhani Takukuru wafanye kweli then tuone response maana kama asemavyo Masatu Shamba la Bwana Heri na Mbuzi mali yake .So am watching
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hii habari imeandikwa vibaya sana. Ninaituma tena:

  Mbunge Ole Sendeka atishia kumharibia Rais KikweteMbunge wa Simanjiro,Christopher Ole Sendeka, ametishia kuiharibia serikali ya Rais Kikwete iwapo itaendekeza hoja ya "posho mbili" ili kudhalilisha wabunge.Ataka serikali iwakamate kwanza nafisadu badala ya kuibua hoja ya 'posho mbili'

  Daniel Mjema, Dodoma

  SUALA la wabunge kuhojiwa na Takukuru, juzi lilichukua sura mpya baada ya Mbunge wa Simanjiro,Christopher Ole Sendeka kugeuka msumari wa moto kwa serikali akitaka iwakamate kwanza wabunge mafisadi wanaohusika na kashfa za Kagoda na Deep Green Finance kabla ya kuwaandama wabunge.

  Katika kashfa hizo, Kampuni ya Kagoda Agriculture inadaiwa kuchota kifisadi Sh40bilioni kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wakati Deep Green Finance inadaiwa kukwapua Sh9 bilioni kutoka kwenye akaunti hiyo.

  Kwa mujibu wa taarifa za kutoka ndani ya kikao cha faragha cha wabunge wa CCM kilichofanyika mjini Dodoma,inaelezwa kuwa Sendeka alihoji kama kweli agizo la kuwahoji wabunge lilitolewa na Ikulu.

  Huku akishangiliwa na wabunge wengine, Sendeka aliibana serikali akitaka kujua iwapo Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah ametumiwa na mafisadi au kweli katumwa na Rais Jakaya Kikwete kuwadhalilisha wabunge.

  Sendeka alitoa kauli hiyo juzi usiku mjini Dodoma katika kikao cha faragha cha wabunge wa CCM kilichofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa chini ya Katibu wa Kamati ya Wabunge wa chama hicho, Ali Ameir na taarifa zake kulifikia gazeti hili.

  “Kuna mambo mawili ambayo tunayaona katika suala hili; ama Dk Hoseah anatumiwa na mafisadi au ametumwa na rais kuwadhalilisha wabunge kwa sababu Takukuru siyo taasisi inayojitegemea bali iko chini ya rais,” chanzo chetu kilimkariri Sendeka akisema ndani ya kikao hicho.

  Alisema hawaelewi na hawaamini kama rais ndiye ameagiza wabunge wadhalilishwe, lakini kama ndivyo awaeleze ili nao waende majimboni kwa wananchi kuwaeleza mabaya ya serikali wanayoyafahamu.

  Huku akipigiwa makofi na wabunge karibu wote waliohudhuria kikao hicho, Ole Sendeka alisema baada ya kuwaeleza wananchi, wao ndio watapima ni nani wasafi kati ya wabunge, serikali na Takukuru.

  Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho, zimedokeza kuwa Sendeka alitaka Rais Kikwete azungumze na Mkurugenzi wa Takukuru kabla mambo hayajaenda kombo.

  Kikao hicho kilikuwa mahususi kwa kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM kutoa taarifa ya ujio wa kamati ya Mzee Ali Hassan Mwinyi, lakini Ole Sendeka akakitumia kuibua suala la uchunguzi huo wa Takukuru.

  “Tunafahamu Hoseah anajua humu ndani wapo wanaohusika na kashfa za Kagoda, Meremeta na Deep Green Finance awakamate kwanza, tuone kama kweli anakerwa kwa dhati na tatizo la rushwa,”alikaririwa Ole Sendeka.

  Mbunge huyo machachari alisema endapo suala ni malipo ya posho kwa wabunge, iundwe tume huru ya pamoja kuchunguza na uchunguzi huo ufanyike kwa mihimili yote mitatu ya dola kwa maana ya Bunge, Mahakama na Serikali.

  Chanzo hicho cha habari kimedokeza kuwa Ole Sendeka alisema endapo uchunguzi huo utabaini wabunge wamekula fedha haramu, wako tayari kuzirejesha lakini, akasema nao watatumia nguvu ya umma kupasua mabomu ya serikali.

  Alidai kuwa hata yeye Hoseah na taasisi yake (Takukuru) ilipokuwa inataka Bunge lipitishe muswada wa marekebisho ya Sheria ya Rushwa, aliandaa semina kwa wabunge na kuwalipa posho kama ilivyo kwa taasisi nyingine.

  Ole Sendeka alimtaka Dk Hoseah kama ana hoja ya msingi katika uchunguzi wake asubiri kwanza Bunge limalizane na suala la Richmond wiki ijayo, ndio waendelee na uchunguzi wao.

  “Baada ya uchunguzi wao watupigie mahesabu kama kuna fedha haramu tumekula, tupo tayari kuzirejesha lakini uchunguzi huo uendelee pia kwa mihimili mingine ya dola ambayo ni serikali na mahakama," alikaririwa Sendeka.

  Katika kikao hicho Ole Sendeka alihoji ni mkuu wa mkoa gani au waziri anayesafiri kwenda wilayani au mikoani ambaye hata kama amelipwa posho stahiki, husafiri na chakula chake bila kukirimiwa na halmashauri anakokwenda.

  Habari kutoka katika kikao hicho, zimezidi kueleza kuwa Ole Sendeka aliitaka serikali kuwasiliana na Spika wa Bunge au katibu wake ili kupata ufafanuzi wa posho hizo vinginevyo iwaite wabunge wote na kuwahoji.

  Wakati mvutano huo ukiendelea, zipo taarifa kuwa Takukuru imekuwa ikijiandaa kuwakamata baadhi ya wabunge siku moja au siku ya mjadala wa Richmond ikiwa ni mbinu ya kudhoofisha mjadala huo.

  Habari zilizowakariri baadhi ya wabunge zinadai kuwa mpango huo umeandaliwa mahususi na wapo wabunge kwa majina ambao wanaandaliwa mpango wa kuwakamata, ila wanasubiri kwa hamu hilo litokee.

  Wiki hii, Mbunge wa Kyela, Mwakyembe alinukuliwa na vyombo vya habari akisema hatua hiyo ya Takukuru kutaka kuwahoji wabunge sasa, ina lengo la kuwafunga midomo wasijadili kashfa ya Richmond.

  Alhamisi wiki hii, Spika wa Bunge,Samuel Sitta alisema wabunge wataendelea kupokea posho kwa kuwa ni halali na serikali ilileta bajeti zake bungeni na zikapitishwa na kuitaka Takukuru ishughulikie mambo ya msingi.

  Msuguano huo kati ya Serikali na Bunge umekuja wakati wiki hii Bunge linatarajiwa kujadili ripoti ya serikali ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge yanayoitaka serikali kutekeleza maazimio yote bila kusitasita.

  Miongoni mwa maazimio hayo ya Bunge ni kuwajibishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Hoseah kwa namna alivyoficha ukweli kuhusu Richmond hadi kamati ya Bunge ilipogundua uozo mkubwa.

  Kashfa ya Richmond ndiyo iliyosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu akifuatiwa na mawaziri wengine wawili, Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi ambao waliitumikia Wizara ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti wakati wa mchakato wa zabuni iliyoipa ushindi kampuni hiyo.

  Pamoja na kujiuzulu huko maazimio ya Bunge yalitaka pia kuwajibishwa kwa aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali, Johnson Mwanyika na katibu mkuu wa Wizara ya
  Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi ambao wamestaafu kwa mujibu wa sheria. Wabunge wanataka suala la utekelezaji wa maazimio hayo ya Bunge limalizike katika Bunge hili la 17, lakini hadi jana kulikuwa na usiri mkubwa wa lini ripoti hiyo ya serikali ya wa maazimio hayo itawasilishwa bungeni.

  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=15689
   
 5. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2009
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  • Alisema hawaelewi na hawaamini kama rais ndiye ameagiza wabunge wadhalilishwe, lakini kama ndivyo awaeleze ili nao waende majimboni kwa wananchi kuwaeleza mabaya ya serikali wanayoyafahamu.
  Kwa hiyo mabaya ya serikali mnayafahamu lakini mpaka mshikwe pabaya ndio mnatishia kuyaweka bayana......hii inaonyesha wazi hamtendei haki wapiga kura wenu.
  • Chanzo hicho cha habari kimedokeza kuwa Ole Sendeka alisema endapo uchunguzi huo utabaini wabunge wamekula fedha haramu, wako tayari kuzirejesha lakini, akasema nao watatumia nguvu ya umma kupasua mabomu ya serikali. Baada ya uchunguzi wao watupigie mahesabu kama kuna fedha haramu tumekula, tupo tayari kuzirejesha lakini uchunguzi huo uendelee pia kwa mihimili mingine ya dola ambayo ni serikali na mahakama," alikaririwa Sendeka.
  Huu utamaduni wa 'kurejesha' pesa baada ya kuiba uko katika sheria ipi katika jamhuri ya muungano? Kwa kawaida ukibainika kuwa ulipata mapato isivyo halali unachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kurejesha pesa si kwamba ukisharejesha pesa kesi imekwisha. Kama utaratibu ungekuwa hivyo basi magereza yangekuwa matupu kwani wengi wanaosota huko wana uwezo wa kurejesha mali walizoiba.
  • Alidai kuwa hata yeye Hoseah na taasisi yake (Takukuru) ilipokuwa inataka Bunge lipitishe muswada wa marekebisho ya Sheria ya Rushwa, aliandaa semina kwa wabunge na kuwalipa posho kama ilivyo kwa taasisi nyingine.
  Mhishiwa Sendeka...kosa moja halihalalishi jingine. Kama Takukuru nao walifanya makosa wabanwe kama ninyi mtakakavyobanwa.
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ustaadh,

  Umesema baba, umesema.Sasa hapa tuache wapigane vita mwananchi afaidike.Hawa wabunge wengine ubunge sijui wanapataje, wanaongea kama mafia bosses zaidi ya wabunge.

  Mi naona uongozi wetu wote mbovu, si wabunge, dola, TAKUKURU, kote kumeoza.
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lunyungu,

  Nina wasiwasi na elimu ya Sendeka na uwezo mzima wa kufikiri. Kama ni kweli haya yananayo daiwa kusemwa na yeye basi hafai kuwa Mbunge.

  Kuna kitu kinaanza ku surface katika ulingo wa siasa Bongo, the so called "wapiganaji" kadiri tunavyo karibia uchaguzi mkuu mwakani wanachachawa sana na kutoa kauli tata, kulikoni?
   
 8. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Safi sana Ole Sendeka kwa uliyoyasema kama ni kweli. Tunamatatizo makubwa ya Kagoda, Meremete na Mengineyo mengi ambazo ni wizi wa kufikia kabisa. Na hakuna chochote kilichofanyika juu ya hayo zaidi ya kuambiwa ni issue za usalama wa taifa na ajeshi! siku vyombo hivi vikisema sijui itakuwaje? tunaombea isiwe hivyo kabisa.

  Hebu tuiangalie hii issue kwa mapana na marefu.
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Oct 31, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  "Chanzo hicho cha habari kimedokeza kuwa Ole Sendeka alisema endapo uchunguzi huo utabaini wabunge wamekula fedha haramu, wako tayari kuzirejesha lakini, akasema nao watatumia nguvu ya umma kupasua mabomu ya serikali."

  Hapa ni kurejesha fedha haramu peke yake au kuna kushtakiwa and if possible kufungwa jela? Mbona "wapiganaji" akina Ole Sendeka ni wepesi sana kusahau sheria walizotunga wenyewe?
  Halafu kwa nini "wapiganaji" wanakuwa na akiba ya mabomu ambayo huwa wanatishia kuyatoa pindi wanaposhambuliwa? (wako tayari kuzirejesha lakini, akasema nao watatumia nguvu ya umma kupasua mabomu ya serikali.")Kumbuka kauli ya Dkt Mwakyembe bungeni kwa wale waliokuwa wanachokonoa kiaina mambo ya Richmond baada ya yeye kutoa Ripoti yake: "Kama kuna watu wataendelea kuzungumizia mambo ya Richmond tutasema yale ambayo hatukuyasema ili kutokuiumbua Serikali!" Hapa Tz umdhaniye ndiye kumbe siye!
   
 10. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Hawa wote wanajuana mbinu zao zote sasa ni kutishana ukimwaga mboga mi namwaga ugali ngoma droo

  Serikali imekaa kifisadi na waliochangia kumuweka jk madarakani waliwekeza so ni lazima iwalipe. Wanajua wote mambo yao na chama chao. Hii vita yao inaweza kuja kutuletea nchi mpya wakishindwa kukaa chini pamoja. Hapo kila mtu anamuona mwenzie anavypiga sasa mmoja kaamua kuonyesha mwenzie basi balaa. Nani asiyejua posho mara 2 zimeanza miaka mingi iliyopiata hata jk kalamba sana mawaziri, wakuu wa mikoa, nk wanakula mara 2? Tazama bajeti ya posho uone na hapo inaisha na inakula mafungu mengine
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,791
  Trophy Points: 280
  sirikali inatakiwa ijiuzulu kuanzia mkulu..........Au nani atatolewa kafara tena??? wabunge???
   
 12. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,073
  Likes Received: 4,001
  Trophy Points: 280
  Jamani naomba kwanza niwasalimie wana-JF mimi ni mgeni hapa ila nina machache ya kusema

  Kwa aliyesema ati Wabunge wameiba hizo posho nathani anapotosha wana-jamii hizo posho ziliidhinishwa na nashangaa leo serikali kuanza kuwapakazia wabunge ati wameidanganya! Kitendo cha TAKURURU kuanza kutafutana uchawi (Tit for tat) hakiwezi kusifika hata kidogo hebu tujiulize hawa TAKURURU walikuwa wapi kipindi chote mpk pale wanapoona mabwana wao EL na RA wanaadhirika ndo wanakuja juu na kuvumbua kesi feki! hebu niambieni tuwe wakweli mnathani kuna Mb. anaweza kufungwa kwa kupewa posho ambayo sheria iliruhusu? Tuacheni matusi jamani hii serikali inaanza kututukana inataka kuuza Richimond case for posho! Jamani wabunge wenu wanastahili more than that siyo fedheha za kufungwa mdogo na posho za laki moja! Tuweni wakweli jamani na tujiulize kama Richmond imechukua zaidi ya miaka mitano bila ufumbuzi inakuwaje swala la posho linachukua chini ya miezi miwili kushughulikiwa!

  Jamani nataka kulia mwenzenu, hii nchi ina wenyewe na dunia hii hakuna kitu kinaweza kufanyika kama tutaanza "mambo ya mbona mbona nyingi" yaani serikali baada ya kuona imekabwa koo inaanza kusema mbona wabunge wanapewa posho mara mbili au mbona hivi na vile ati mbona Mwakyembe committee was given over Tshs400 mio. jamani ile kamati ilikuwa na watu chungu nzima na walisafiri mpka US kutafuta ushaidi kama wanaona hela zilitumika vibaya then waulize breakdown ya matumizi! Na kwanini haya yote now? Tuwe makini kuona hapa kuna what we call silencing the Bunge! Hakuna chochote cha maana kila kitu kina wakati wake sasa hivi swala muhimu kwa nchi hii miaka mitano baada ya kununua umeme feki na kupoteza over US$176 mio. tujuwe yamefika wapi? umeme uko wapi? Na waliojikwapulia hela wamefanywa nini? Tuelezwe na sio tunakaa na watu kama wakina Nimrod Mkono wanaenda majimboni kufungua mashule na ukiuliza ni kivipi wamefanikiwa unakuta wao ndo walikuwa legal representatives wa Richmond na makampuni chungu nzima yanayokwapua nchi hii halafu wanajifanya wana uzalendo juu wa nchi hii! Tufikie wakati tuseme hizi siasa zinaelekea pabaya maana kama Mb. yuko kwenye chamber halafu huyohuyo anapewa kazi za serikali jamani "where is conflict of interest" heshima iko wapi kwenye fani ya sheria? kuna watu wanatajirika kwa mitaji ya serikali halafu haohao unawaona wanapita mitaani wakijitamba ati ni wabunge wanawakilisha wananchi, kwenye nini haswa kama sio kwenye kuwaibia rasilimali zao ni kampuni gani itataka kuwa na legal representative zaidi ya huyu bwana ambae anaweza ku-lobby bungeni wapate tax cuts na vitu vingine kemu kemu? Why shouldn't Mwanza ana Mara and Shinyanga be like J'burg? hivi mshawahi kujiuliza? ni nani wachawi wenu? au mshafika mkaona watu walivyo wanateseka huko na Migodi iko pembeni mwao? Mtashangaa wazawa wa huko huko ndo wachawi wenu! kuanzia wakina Chenge, Hosea na mpk wakina Mkono!

  Fungukeni macho! narudia acheni njaa kwa wale waliopewa upofu ghafla kuhusu swala la Richmond kwa kuuziwa posho za wabunge (kubadilishiwa picha)! Ifike wakati watu waseme sasa tosha hatutaki hadithi za abunuasi! Tunataka mwenye Richmond aadhibiwe plus mwenye kumkingia kifua Richmond!
   
 13. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kuhojiwa inaonekana kama kuonea hivi ..gosh! hawa wabunge vipi..sheria wanataka iwahoji wananchi wa kawaida siyo wao shame!
  Halafu hii habari ya ukisema na mimi ntasema ndio nini ala! mimi nafikiri sendeka na timu yake "WAMEKOSA DIRA NA MWELEKEO" hawa jamaa siyo viongozi ila mapunguani..
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Buchanan,
  Hii kanuni ya kurejesha fedha bila kuchukuliwa hatua imeanzishwa na kulelewa na serikali ilipojikuta katika hali mbaya kuhusiana na sakata la EPA.
  Umeshaona mahali gani mwizi anakiri "guilty" kwa kurudisha mali na hakimu wala asimtaje mwizi huyo au kumpa adhabu?
   
 15. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2009
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  kwa hiyo wakishazirejesha ndo basi tena? hiyo ndo sheria mpya siku hizi? oooh nilisahau kuwa EPA wameset precedent
   
 16. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #16
  Nov 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Bongo utamaduni wa posho ni wa siku nyingi, Imefikia wakati mtu unaandaa mafunzo kwa wabongo unawapa bure lakini watakudai posho ya wewe kuwaandalia mafunzo, yaani ni tabu tupu. Magari ya kifahari ya wafanyakazi wa serikali na NGO maranyingi yanaendeshwa kwa posho kama sio pia mengine huwa yamenunuliwa kwa posho.

  Mishahara imekuwa midogo sana kiasikwamba inabidi wafanyakazi watafute mbinu za kuishi ikiwemo posho za vikao na safari nyingine za kuchongwa tu ambazo hazina tija kwa nchi hii. Posho za ajabu ajabu ni janga la kitaifa, kuziondoa inahitajika mikakati wa kuboresha mafao ya wafanyakazi wa sekta zote ili kupunguza usanii wa kusogeza maisha kwa kutumia mbinu za kifisadi.
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Nov 1, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu Masatu maneno haya yanayo semwa yana maana nyingi na watu wana conf maana wanajua kwamba Serikali imeoza ndilo naweza kusema.Mbunge kutishia kuhubiri uchafu wa serikali yake si jambo la kawaida ni kwamba wamechoka na mambo ya Chama chao na serikali yao ya sasa .

  Wanaona kuna double standards na wamejua na wanajua kwamab CCM na yeye mwenyewe they have never been there for Nchi yangu .Wanajua kwamba hata kura huwa hawashindi na wakiamua kusema kama PCCB itakaza uzi ina maana watasema yale ambayo siku zote tunalia .Wamesha sema kwamba kwa nini Deep Green , Kagoda nk hawakamatwi ama kuhojiwa huo ni mwanzo hata wao wanajua kwamba Rais ana watu wake ama CCM imegawanyika. Sikubaliani na Mbunge huyu anaye leta vitisho ili kulinda ujinga. Alikuwa wapi siku zote ? CCM hakika ina sura kadhaa na inatisha . Nakubaliana na PCCB waendelee na kazi nanakubaliana na Bunge liendelee kujadili hoja ya Richmond.
   
 18. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Sasa ndo filamu ya pambano inaanza.
  Richmondi ilikuwa trela.
  In the Blue Corner:RA,EL wakisaidiwa na wapambe TAKUKURU
  In the RED Corner: Spika 6,DR Mwakyembe,Ole Sendeka na wapambe wananchi
  SIFA:Wote wana uwezo na sifa ya UFISADI PAPA na Ufisadi posho

  Pambano hili ni la kitaifa
  VENUE: Dodoma Bungeni
  Sasa hili pambano sijui kama litakuwa THRILLER IN MANILA au RUMBLE IN THE JUNGLE
  Watazamaji kaeni mkao wa kuona masumbwi ya faulo na yale yanayopiga below the belt.
  REFA:UCHAGUZI 2010
   
 19. W

  Wasegesege Senior Member

  #19
  Nov 1, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtu mwenye akili huficha upumbavu wake
   
 20. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #20
  Nov 1, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  yetu macho na masikio twasubiri huo mpambano
   
Loading...