Mbunge Ngassa: Wananchi mpo salama kwenye mikono ya CCM

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945
WhatsApp Image 2023-07-11 at 13.49.11.jpeg


Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa amewasii wakazi wa Jimbo la Igunga wasiteteleke kwa kauli mbalimbali za upotoshaji kuhusu maendeleo na kuwahakikishia kuwa chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wapo mikono salama na waendele kupokea miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kupitia Ilani ya CCM.

Mheshimiwa Ngassa (MB) ametoa rai hiyo wakati akiongea na Wananchi kwenye mikutano aliyofanya kwenye Vijiji na Vitongoji vya Kata ya Kinungu.

WhatsApp Image 2023-07-11 at 13.49.10(1).jpeg


"... Kinungu Tumeleta Umeme, Tumeleta Barabara, Tumeleta maji ya visima na sasa Mnajiandaa kupokea Maji ya Ziwa Victoria kutoka mradi unaotekelezwa kwa Shilingi Bilioni Ishirini (Tshs 20,000,000,000/=) kutoka kwenye Tenki linalojengwa Mlima wa Bulenya, Watoto wanasoma Elimu bila Ada na Tumeongeza upatikanaji wa madawa na vifaa tiba kwenye vituo vya afya na zahanati za vijijini. Haya ndio maendeleo tuliyoahidi Mwaka 2020 kwenye kampeni na tunaendelea kutekeleza..."

Wananchi wamejitokeza kwa wingi kusikiliza taarifa ya utekekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuwasilisha kero mbalimbali zilizopata ufumbuzi kutoka Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.

WhatsApp Image 2023-07-11 at 13.49.09(1).jpeg


"KAZI NA MAENDELEO"

Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Igunga
11 Julai, 2023
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-07-11 at 13.49.09.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-11 at 13.49.09.jpeg
    115 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-07-11 at 13.49.10.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-11 at 13.49.10.jpeg
    137.8 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-07-11 at 13.49.11(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-11 at 13.49.11(1).jpeg
    76.3 KB · Views: 1
Back
Top Bottom