PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,202
- 8,781
Mbunge wa Nccr Mageuzi Moses Machali akizungumza leo ktk kipindi cha Hamza Kasongo kwenye Mada inayosema MUSTAKABALI WA TANZANIA KWA MUJIBU WA NCCR MAGEUZI ameshindwa kabisa kuongelea hoja hiyo na badala yake akajikita kuiponda CHADEMA akisema viongozi wake walichukua mashangingi ya Ubunge wakati waliyakataa, na kuwa CHADEMA wanakituhumu chama chao na cha CUF kuwa ni Mamluki wa CCM.
Mwanamtwara mmoja akipiga simu amezidi kumwaibisha Mbunge huyo kwa kumtaka aeleze ukweli wa nini kilimpata Mbatia akiwa jukwaani, lakn Machali amemtetea bosi wake kwa kukataa katakata kuwa hakushushwa jukwaani, bali ni propaganda za CHADEMA.
Ni masikitiko mno kwa kijana wa umri wake kutoeleza msimamo wa chama chake, badala yake ameongea off-points na kuchemka, huku maongezi yakijikita kwenye jazba na lawama tupu.
NCCR Mageuzi jipangeni upya.