Mbunge mmoja amwita Spika Sitta 'Madam'

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KATIKA kile kilichoelezwa kuwa ni homa ya uchaguzi mmoja wa wabunge jana alimwandikia ujumbe Spika wa Bunge Samuel Sitta, ukiwa na anuani 'Madam Spika'.

Tukio hilo la aina yake lililoibua hisia tofauti na kuwafanya wabunge waangue vicheko, lilitangazwa na Spika wa Bunge mwenyewe muda mfupi baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa wajumbe wa bodi mbalimbali za vyuo vikuu.

"Naona wabunge wana homa ya uchaguzi, nalisema hili kwani naona dalili. Kwa mfano mheshimiwa mmoja ameniita Madam Spika," alisema Spika Sitta na kuwafanya wabunge waangue vicheko.

Lakini Spika pamoja na maelezo hayo aliwaasa wabunge kutokuwa na homa ya uchaguzi kwa kuwa Mungu ndiye anayempangia kila mwanadamu bahati yake ambayo haiwezi kubadilishwa na mwanadamu mwingine.

"Tusiwe na homa ya uchaguzi, hii yote ni homa tu, Mungu amekupangia maisha yako, hata watu wabaya wakufanyeje hawawezi kukuharibia," alisema Spika na baada ya hapo kuendelea na matangazo mengine kabla ya uchaguzi wa wajumbe hao.

Katika uchaguzi huo wajumbe wawili wa bodi ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam (Udsm) walipita bila kupingwa baada ya kukosa wapinzani ambao ni Profesa Feetham Banyikwa (Mb) na Ruth Msafiri.

Katika bodi ya Chuo Kikuu cha Biashara Stadi, Daniel Nsanzugwako (Mb) alichaguliwa kuwa mjumbe na Pindi Chana alichaguliwa kuwa mjumbe wa bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, wote hawakuwa na wapinzani.

Hata hivyo nafasi moja ya ujumbe wa Bodi ya Tume ya Vyuo Vikuu ilikuwa na ushindani ambapo Mbunge wa Kisesa, Johnson Mpina alichuana na Mbunge wa Muyuni, Dk Haji Mwita Haji.

Katika uchaguzi huo Mpina alimshinda Dk Haji kwa kupata kura 117 kati ya kura 197 zilizopigwa huku mpinzani wake akipata kura 70 na kura tano ziliharibika.
 
Huyu mbunge aliyemuandikia ujumbe Spika na kumuita MADAM alifanya makusudi wala sio homa ya uchaguzi!! Huyu bwana lazima anatoka kundi la Lowassa na wanajaribu kumpelekea ujumbe Sitta kuwa wamekwisha muandaa Spika wa kumbadili katika bunge lijalo naye atakuwa MWANAMKE!! Sio coincidence kuwa hata magazeti ya mafisadi siku hiyo hiyo yalikuwa yanagawiwa bure bungeni!!
 
........
"Tusiwe na homa ya uchaguzi, hii yote ni homa tu, Mungu amekupangia maisha yako, hata watu wabaya wakufanyeje hawawezi kukuharibia," alisema Spika na baada ya hapo kuendelea na matangazo mengine kabla ya uchaguzi wa wajumbe hao.
........


Spika Sita kama Sofia Simba, kwenye mipasho yumo.

By the way, what is the 'eligibility' ya kuwa board member kwenye vyuo vikuu?
 
Back
Top Bottom