Mbunge Lema akamatwa na Polisi!

Mbunge Lema akamatwa na Polisi!

UFUNUO WA TANZANIA

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
471
Reaction score
166
Baada ya mabishano ya muda mrefu nyumbani kwa kada huyu na Mbunge wa Arusha mjini na uvamizi onevu wa Polisi wakati huu wa usiku; Mh. Lema amekubali kukamatwa na amechukuliwa na gari la polisi wakati huu na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Arusha yaani Central Polisi.

Wananchi wengi wamejitokeza ku-support mbunge wao na huenda Asubuhi wananchi wakawa wengi zaidi.

Scene two ni hali itakavyokuwa huko polisi.

Updates
Sasa wamefika CLocktower anasindikizwa na msululu wa magari ya makada waliojitokeza ku-support kuelekea kituo cha polisi.

Baada ya kumfikisha Lema Central police Arusha amesachiwa na kuingizwa ndani. Kamanda Lema alikuwa ameambatana na magari ya makamanda waliomsindikiza ili kushuhudia kinachojili hapo kituoni.

Hivi sasa polisi wamewafukuza makamanda wote hapo kituoni na kuwaambia hawatakiwi kuonekana hapo. Makamanda wameondoka kwa amani na kwenda kupaki Safari hoteli wakisubiriana kupata mwongozo.

03:41am
Wamekutana pembeni ya kituo cha polisi na wamekubaliana kuwa watawanyike wakalale hadi kesho asubuhi watajuzwa kinachoendelea. Hivyo, Lema yupo ndani na wananchi waliomsindikiza wametawanyika kwenda kulala. Tutaonana asubuhi kwa yale yatakayojiri.

11:15am
Kwa sasa Lema bado yuko ndani na bado hajahojiwa. Kwa sasa anasubiriwa Mwanasheria wake ili ahojiwe. Mpaka sasa hakuna tamko lolote juu ya sababu za kukamatwa kwake. Baada ya kuhojiwa huenda mwanasheria wake atasema kilichojiri. Watu waharuhusiwi kukaa au kusimaa vikundi vikundi eneo la polisi.

Tayari uongozi wa chama mkoa chini ya katibu wa mkoa wameshaongea na RCO, muda si mfupi kamanda Lema atachukuliwa maelezo, ndiyo taratibu zingine zitafuata ikiwa ni pamoja na dhamana.
Earlier by Emanzi:
Emanzi said:
Nipo hapa naangalia kinachojiri kati ya police na Kamanda Lema, pia ninarecord video tukio zima, nitarusha soon.

Wameamua kuvunja mlango na kuingia ndani, wameshamuweka pingu kamanda Lema, sasa wanasearch kila sehemu, laptop, ipad, simu vipo mikononi mwa police.
Maofisa wa Jeshi la Polisi, waliokuwa na mbwa, mabomu ya machozi na silaha nyingine za moto, usiku wa kuamkia jana waliruka ukuta na kuingia katika eneo la makazi ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ambako walizingira nyumba yake kwa zaidi ya saa nne.

Operesheni ya kutiwa mbaroni Lema iliogozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD), Gillel Muroto ambaye alifuatana na askari zaidi ya 25 waliokuwa na silaha hizo.

Walifika nyumbani kwa Lema saa 5:00 usiku lakini walilazimika kusubiri hadi saa 9:10 walipomkamata Mbunge huyo baada ya yeye mwenyewe kujisalimisha. Habari zinasema Lema aliyekuwa akihojiwa na polisi hadi jana jioni, alinyimwa dhamana kwa maelezo kwamba "anaweza kuhatarisha amani".

Mashuhuda waliokuwa karibu na anakoishi Lema, eneo la Njiro Mwisho wa Lami, walisema polisi hao walifika wakiwa kwenye magari manne na kwamba ili kuchunguza ndani ya uzio wa nyumba yake, walipanda juu ya mabega ya wenzao huku wakielekeza mitutu ya bunduki tayari kukabiliana na lolote ambalo lingejitokeza.

Baada ya kuchungulia baadhi yao walitumbukia ndani ya uzio na kwenda kusimama mbele ya milango na madirisha ya nyumba ya Lema na huku nyuma wengine walipanda tena kwenye mabega ya wenzao kuendelea kuweka ulinzi kwa walioingia ndani.

Askari hao wanadaiwa kwamba waliwataka walinzi wa nyumba hiyo iliyopo karibu na Chuo cha Ufundi Veta, kuwafungulia mlango, lakini walinzi hao walikataa hivyo kuzua mabishano makali.

Kutokana na mabishano hayo, Lema aliyekuwa ndani amelala alishtuka na kuanza kufuatilia na kubaini kuwapo kwa polisi nje ya nyumba yake hiyo. Mke wa Lema, Neema alimpigia simu Katibu wa Wilaya wa Chadema, Aman Golugwa kumwarifu kuhusu uwepo wa watu walioruka ukuta.

Golugwa jana alithibitisha kupokea simu ya mke wa Lema na kwamba alipopata taarifa hizo alimwarifu Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) wa Mkoa wa Arusha, Camillius Wambura ambaye baadaye alimuahidi kwamba angefuatilia suala hilo.

"Baadaye alithibitisha kuwapo kwa polisi waliotumwa kwa ajili ya kumkamata Lema lakini akasema amewapa maelekezo ya kufuata taratibu za kawaida,"alisema Golugwa na kuongeza:"Baada ya hapo, wale askari waliokuwa wameruka ukuta walitoka nje ya uzio".

Habari zinasema wakati baadhi ya askari wanaruka ukuta, wengine walibaki nje wakizingira uzio wa nyumba ya Lema huku wakiwazuia viongozi wa Chadema waliokuwa eneo hilo kusogea.

Kukamatwa kwa Lema katika mtindo wa aina yake kumefanywa saa chache tangu alipotoa kauli ya kukataa kujisalimisha polisi, kutokana na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo. Mulongo aliagiza Lema akamatwe kwa tuhuma kwamba alichochea vurugu katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA).

Katika vurugu hizo, wanafunzi hao walimzomea Mulongo na kurushia mawe msafara wake wakati alipokwenda kusikiliza malalamiko yao yaliyotokana na kuuawa kwa mwanafunzi mwenzao, Henry Kago (22) ambaye alichomwa kisu na watu wasiofahamika wakati anatoka kujisomea saa 4:00 usiku.


source: Gazeti la mwananchi
 
What ila wameenda na hati, au ndio wataitengeneza kesho asubuhi.

Shame on serikali. Inaudhi sana kusikia mambo haya yanaendelea nchini kwetu.

Nyerere atakuwa anasikitika kuona wanaaribu chama chake jamani.
 
Nipo hapa nacheck movie ya
police na Kamanda Lema,pia ninarecord video tukio zima,nitarusha
soon,wameamua kuvunja mlango na kuingia ndani wameshamuweka pingu
kamanda Lema,sasa wanasearch kila sehemu,laptop,ipad,simu vipo mikononi
mwa police.

ameelezwa anachotuhumiwa?
 
" Lema akirudi Bungeni nitakunywa sumu" .... Nchi ameshaharibika, mkuu wa mkoa alimwambia atampa kesi, anatimiza azima yake...
 
Bado narekodi kwa kalamu/pen nitawajuza soon
 
km unapicture hadi hapo hakuna shida,copy haraka ulichokipata kiondoshe.kesho wakimleta kaumia raia watadeal nao.wakunyang'anya sasa hivi.

Kuna haja ya kuwa na virus wa ku kukopy data ya polis wakiconect na gadget za lema na baadae kuharibu machine ya polisi au kutembea na machine yote ili kuwapeleza na wao.
 
Wamekuta mikanda mingine ya kigaidi?
 
Bado narekodi kwa kalamu/pen nitawajuza soon

Aminia mkuu.ccm hawajui karibu police wote wanalinda mabenk nyumba za wakuu ,wanaweza tumia sila kusaidia mapinduzi au hata mtungua mkuu yoyote.wengi wamechoka hadi sasa ni maadui wa serikali na jeshi lao.
 
Lazima wanaenda kubadili mida kwenye simu zake na kujitumia messagess na kusema Lema nae alituma hivi.

Wanataka lazima kumbikia kesi, wana Chadema akina Lissu wahini Arusha.

Mie ni mTZ nisiopenda watu kuumizwa hivi.
Kaka kuwa makini basi usiseme data unapataje wasije kukunasa hapo, ukimaliza ukapata muda wako wewe edit post yako ya kwanza ku update tutakufatilia kusoma unaweza weka mida pia itakuwa poa.

Mungu awe nanyi wapenda haki na Lema na familia yake.
 
km unapicture hadi hapo hakuna shida,copy haraka ulichokipata kiondoshe.kesho wakimleta kaumia raia watadeal nao.wakunyang'anya sasa hivi.

Kuna haja ya kuwa na virus wa ku kukopy data ya polis wakiconect na gadget za lema na baadae kuharibu machine ya polisi au kutembea na machine yote ili kuwapeleza na wao.
 
inasikitisha sana, tz tuna watawala madikteta
 
Back
Top Bottom