Asante kwa taarifa mkuu,amefia India?Habari nilizozipata ni kuwa aliyewahi kuwa naibu waziri wa fedha na mbunge wa Arumeru mashariki bwana Sumari ameaga dunia.
Poleni wafiwa.
Source: MOI
Nafikiri hakuapa sababu ya kuumwa! RIP MH SUMARIJe, mpaka anafariki alikuwa mbunge? Poleni sana wafiwa.
Nilisikia muda mrefu kuwa yu mgonjwa lakini sikusikia kama aliwahi kupelekwa India kwa matibabu kama wenzie................. Hivi kumbe kupelekwa India kwa matibabu inategemea na nafasi uliyo nayo serikalini!
Mungu amlaze mahali pema peponi...............Amina
RIP Bwana Sumari
Haya mambo yanapotokea ndio tunajifunza pia hivi unaweza kukaa muda gani bila kuapa kama Mbunge mteule kwa wabunge waliochaguliwa na wananchi? Sheria zetu hazitoi muda kutengua Mbunge Mteule na kuitisha uchaguzi kama Mteule akishindwa kuapa kwa sababu yeyote? Watu wa Arumeru hawakuwa na Mbunge kipindi chote hiki na pengine ingekuwa zaidi ya hapa kama angeendelea kuumwa kwa miaka mingine? Napenda kujifunza kupitia tukio hili wakuu.Alipelekwa India kwa matibabu na taarifa hizo ziliwekwa hapa jukwaani
RIP (Mbunge mteule)