Mbunge Ismail Jussa apeleka hoja binafsi Baraza la Wawakilishi kuhusu katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Ismail Jussa apeleka hoja binafsi Baraza la Wawakilishi kuhusu katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Mar 23, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Serekali ya Smz itowe Muuongozo kuhusu Katiba

  [​IMG]

  MAELEZO YA MHE. ISMAIL JUSSA, MJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WA JIMBO LA MJI MKONGWE, KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA HOJA BINAFSI ANAYOKUSUDIA KUIWASILISHA KWENYE MKUTANO WA BARAZA LA WAWAKILISHI UNAOENDELEA

  Leo hii asubuhi nimewasilisha kwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi taarifa ya kusudio la kuwasilisha Hoja Binafsi kwenye mkutano wa Baraza la Wawakilishi unaoendelea, chini ya Kanuni ya 49 (1) na (2) ya Kanuni za Baraza la Wawakilishi (Toleo la 2011).

  Hoja Binafsi niliyoitolea taarifa imelenga kutumia Kanuni ya 27(1)(m); 27(3); 47(2); 48(1) na 49 (1) ya Kanuni za Baraza la Wawakilishi (Toleo la 2011), kuliomba Baraza la Wawakilishi kupitisha Azimio la kuitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuchukua hatua za kuandaa mapendekezo ya mambo ya msingi ambayo Zanzibar, ikiwa mojawapo ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itataka yazingatiwe katika mfumo mzima wa utaratibu wa uandaaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Hii inatokana na hatua tuliyofikia baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi kwa Taifa aliyoitoa Desemba 31, 2010, kutangaza kusudio la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuchukua hatua zitakazopelekea kuandikwa kwa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Katika hotuba hiyo, Rais Kikwete alieleza dhamira yake ya kuunda Tume ya Katiba itakayokusanya maoni ya wananchi kutoka makundi mbali mbali ya kijamii na kisha kusimamia kazi ya kuandaa mapendekezo ya rasimu ya Katiba hiyo Mpya.

  Katika kutekeleza tamko hilo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, aliliambia Bunge la Jamhuri ya Muungano katika mkutano wake wa mwezi Februari 2011 kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano itapeleka Mswada wa Sheria kuhusu utaratibu utakaofuatwa katika kuandaa Katiba hiyo Mpya ya Jamhuri ya Muungano katika mkutano unaofuata wa Bunge utakaofanyika mwezi Aprili 2011.

  Kutokana na hatua hizo, nimeona kuna haja ya kuliomba Baraza la Wawakilishi kuchukua hatua ya kutoa azimio litakalotoa mwongozo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuweka mambo ya msingi ambayo Zanzibar, ikiwa mojawapo ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inapaswa iyawasilishe kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ili nayo yazingatiwe wakati huu Serikali ya Muungano ikiwa inaandaa Mswada wa Sheria utakaopelekwa katika mkutano ujao wa Bunge ambao utaweka mfumo mzima wa utaratibu wa uandaaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Naamini kabisa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa ndiyo yenye kushikilia dhamana ya uongozi wa Zanzibar na inayowakilisha maslahi, matakwa, matarajio, haki na wajibu wa wananchi wa Zanzibar ina wajibu wa kutayarisha mambo hayo ya msingi ambayo Zanzibar kama mshiriki mmojawapo wa Muungano inataka yazingatiwe na yaingizwe katika mfumo mzima wa utaratibu wa uandaaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ambao unapaswa kusimamiwa kwa pamoja na pande zote mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Nimeamua kutumia haki hii inayotolewa na Kanuni za Baraza la Wawakilishi kuwawakilisha wenzangu ambao nao kama nilivyo mimi wanaamini kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mali ya wananchi wa nchi mbili zinazounda Muungano huu yaani Zanzibar na Tanganyika na hivyo inapaswa kuwakilisha maslahi, matakwa na matarajio ya wananchi wa nchi hizi mbili.

  Nafanya hivi pia nikiamini kwamba Baraza la Wawakilishi, kwa mujibu wa Katiba ndiyo Mamlaka ya Kutunga Sheria na Kusimamia Utekelezaji wa Shughuli za Umma ndani ya Zanzibar, na hivyo lina dhamana ya kusimamia maslahi, matakwa, matarajio, haki na wajibu wa wananchi wa Zanzibar ambao kutoka kwao ndiko yanakotoka mamlaka ya kuendesha nchi na kutoka kwao ndiko kunakotoka nguvu na uwezo wote wa Serikali kufuatana na Katiba.
  Hatua ninayopendekeza ichukuliwe na

  Baraza la Wawakilishi ya kuiagiza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuandaa mwongozo huo ina lengo la kuepuka kurejea makosa yaliyofanyika huko nyuma wakati wa kuweka utaratibu wa kuandikwa kwa Katiba za Jamhuri ya Muungano zilizopita zikiwemo Katiba ya Mpito ya 1964, Katiba ya Muda ya 1965 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.

  Naamini Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano itakayotokana na utaratibu huu unaokusudiwa kuanzishwa kuanzia mwezi ujao inapaswa iepuke makosa ya nyuma na badala yake iweke misingi imara ya ushirikiano baina ya nchi zetu mbili zinazounda Muungano huu na ambayo itakidhi hisia, maslahi, matakwa, haki na wajibu wa wananchi wa nchi zote mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano.

  Hoja Binafsi niliyoitolea taarifa ya kusudio la kuiwasilisha naamini itaisaidia nchi yetu kufikia malengo hayo niliyoyataja. Kuwasilishwa kwa hoja hiyo hivi sasa kutategemea maamuzi ya Mheshimiwa Spika wa Baraza la Wawakilishi ambaye, hata hivyo, naamini hatakuwa na pingamizi nayo kutokana na kulenga kusaidia nchi yetu na watu wake.

  Napenda niweke wazi kwamba Hoja Binafsi niliyoitolea taarifa inalenga utaratibu wa kukusanya maoni na kuipata Katiba Mpya (process) na hailengi kujadili nini kinapaswa kuwemo kwenye Katiba Mpya (contents or substance). Hayo yatatolewa maoni na wananchi wenyewe wakati wake ukifika na kwa utaratibu utakaokubaliwa.

  Maelezo ya kina ya maazimio niliyoyapendekeza yapitishwe na Baraza la Wawakilishi yatatolewa baada ya kupata maamuzi ya Mheshimiwa Spika kuhusiana na Hoja hii. Kwa sasa naomba taarifa hii itosheleze.

  Ahsanteni sana.

  ISMAIL JUSSA LADHU
  MJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI
  JIMBO LA MJI MKONGWE (CUF)
  ZANZIBAR
  23 MACHI, 2011
   

  Attached Files:

 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,770
  Likes Received: 4,984
  Trophy Points: 280
  ..aachane na habari za kurekebisha katiba, badala yake alielekeze baraza la wawakilishi kuvunja muungano.

  ..wa-Zanzibari maneno mengi vitendo sifuri. kila siku wanasiasa wanawadanganya kwamba watavunja muungano na kuirejesha dola ya Zanzibar.

  ..sera ya CUF, kulingana na rasimu ya katiba waliyopendekeza, ni kuwa na serikali 3, na Raisi wa Zanzibar kupunguziwa hadhi yake na kubakia kuwa Gavana.
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  Hapa Mtanganyika hapanihusu, Wazanzibar uwanja wenu huo, mimi napita tu.
   
 4. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 654
  Trophy Points: 280
  Serikali tatu au nchi mbili....la sivyo
   
 5. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mh. Jussa,

  Kwa ufupi, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inahusiana na nchi mbili, yaani, Tanganyika na Zanzibar. Je hiyo nchi ya Tanganyika Raisi wake ni nani? Mipaka yake ni ipi? Iko bara gani? Bado ipo?
   
 6. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,971
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nchi mbili..., lol! Hiyo nyingine mbona mi siioni? Kazi kweli kweli. Si wangeshughulikia kuirejesha kwanza hiyo ya pili ndo mambo mengine yakafuata?!
   
 7. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mwaka huu....tutasikia na kuona mengi.....huu muungano uko taabani na unapumulia mashine
   
 8. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  kwa makinda huoni ndani
   
 9. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  wenyewe hawaitaki Tanganyika yao.
   
 10. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Juu ya milima wa kilimanjaro au ngorongoro
   
 11. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  unaboa wanaotumia simu kwa ku quote habari ndefu
   
 12. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ama kweli wewe pumba Rutakyamilwa? Makinda nani mbele ya Wzanzibar na mamuzi ya nchi yao? Wzanzibar wakishokozeka na kero za Muungano sheria ya kura ya maoni iko wazi kwetu kuvunja Muungano ambocho kitu hicho Wzanzibar wanakisubiri kwa hamu ili Baraza la Uwakilishi izinishe na Wzanzibar wachangamke.
  Jee Wzanzibar wakipiga kura ya kusema hatutaki hata aje Baraka Uboma wachilia Makinda basi hawezi kufanya lolote ikiwa Wenyewe Wzanzibar tumeamua Muungano basi, au hujuwi kitu hicho?
   
 13. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi naamini hoja ya mh.Ismail Jussa imechelewa sana kwasababu kama ni kweli mswada unatarajiwa kuweka mfumo wa mchakato utakaotumika katika kuipata katiba mpya utawasilishwa katika kikao cha bunge lijalo, bila shaka hivi sasa utakuwa tayari umeandaliwa, katika hali hiyo haitawezekana kuigiza mawazo mapya kwenye mswada huo. Hata hivyo mimi sioni mantiki ya hoja hiyo; hii ni kutokana na ukweli kwamba Zanzibar inao wabunge zaidi ya 50 katika bunge la muungano hivyo kama kuna hoja zozote serikali ya Zanzibar inataka zizingatiwa wakati wa mchakato wa kuandaa katiba mpya inaweza kuwasilisha hoja hizo kupitia kwa wabunge hao.
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Mar 23, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,770
  Likes Received: 4,984
  Trophy Points: 280
  ..sera ya CUF ni kuimarisha muungano kwa kuanzisha muundo wa serikali 3.

  ..serikali za Tanganyika na Zanzibar zitaongozwa na MAGAVANA.

  ..Raisi atakuwa ni mmoja tu wa serikali ya muungano.

  ..wanasiasa wa Zanzibar hawana majibu ya kilio cha wa-Zenj kuhusu muungano.
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,125
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Iko siku na sisi tutakuwa na nchi yetu ya tanganyika!
   
 16. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Jussa Ismail sio Mbunge bali ni Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe;alikuwa Mbunge wa Kuteuliwa na Rais kwenye Bunge lililopita ili kuimarisha "ndoa ya kisiasa"kati ya CUF na CCM;kwenye uchaguzi wa mwaka jana akagombea na kushinda Uwakilishi jimbo lililotajwa hapo juu!

  Rekebisha kichwa cha habari then tuendelee kuchangia na likely kisomeke;"Mwakilishi Ismail Jussa apeleka hoja binafsi Baraza la Wawakilishi;kuacha kichwa cha habari chenye makosa ni kutuchanganya wachangiaji mada!
   
 17. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Lala tu nchi ishauzwa...sis tukiuvunja muungano tuna nchi yetu zanzibar,na nyinyi mutaingia katika muungano wa EAC sijui mutatumia jina la tanganyika au EAC ? Mana nchi haipo..
   
Loading...