Mbunge huyu wa CHADEMA hovyo kabisa!

Rich Dad

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
748
133
Huyu mama viti maalum chadema - maryam msabaha kweli ni mzigo. Inaonekana aliandaliwa points na Tundu Lissu lakini kashindwa kuwakilisha.
 
Acha unafik mkuu nimemsikiliza mwanzo mwisho utamcompare na Lucy Mayenga aliyetoka nje ya mada? Na kuanza mipasho sijui nan kanuna kakosa uwaziri mara ana cpa! Mariam kajitahd sana.
 
Ya anaongea kwa kasi ila yuko fit sana mie nimekosa mtu ambaye sio makini ndani ya chadema mpaka sasa; kumbe tuna wazanzibar sasa tukachukue nchi ya zenj maana haina wapinzani tena huko tetetetetete
 
Huyu mama viti maalum chadema - maryam msabaha kweli ni mzigo. Inaonekana aliandaliwa points na Tundu Lissu lakini kashindwa kuwakilisha.
acha unafki. Je Zainabu Kawawa aliedai muongozo feki? mpk Ndugai kamuumbua. Maryam kaongea fact kbs!.
 
mbona humu ndani sioni uzi za chadema tu sio za cuf wala ccm aisee mmekuaje wanajamvi..
 
Yule mama alikuwa na maandalizi fulani ya kuongea alichokosa kidogo ni mtiririko wa mada tu, amejitahidi kwa kiasi chake kwa mwonekano wa shule haba.
 
Mariam ni Kichwa .kanikuna sana.

Kweli huyu Mh. Mariam Msabaha kajitahidi sana. Kati ya pointi nyingi alizoongea, kuna moja imenigusa sana; japo alikuwa anailenga Serikali lakini pia chama chake - CHADEMA ni muhimu mno wakaifanyia kazi. Maraiam kashauri hivi: Serikali iache tabia ya kupuuza wasiosoma; hata wasiosoma pia wapatiwe ajira. Tena baadhi ya wasomi (anawaita wezi wa kalamu) ndio walioifikisha nchi pabaya kwa habari ya ufisadi. Hivyo, si kila kitu kuendekeza MSOMI, MSOMI, MSOMI!

USHAURI WANGU KWA CHADEMA: Kuna dhana inayotaka kujengeka kwamba CHADEMA ni chama cha wasomi pekee hasa kwenye nafasi mbalimbali iwe ni katika chama au uwakilishi. Tena kuna mada fulani iliwahi kujadiliwa hapa hapa JF kwamba eti 2015 CHADEMA isimamishe hadi wenyeviti wa mitaa "wasomi" angalau wenye degree. Ingelikuwa Marekani hii ingeweza kuwa pointi muhimu lakini kwa nchi kama Tanzania yenye maamuma wengi hili ni kosa kubwa; wasiosoma ndio wengi na ndio wapiga kura mahiri.

Daima falsafa ya CHADEMA isiwe usomi wa mtu (kama anavyodai Mh. Maryam) hasa katika nafasi ambazo hazihitaji utaalamu maalumu, bali UZALENDO wake kwa taifa. Usomi iwe ni ziada tu tena ije baada ya UZALENDO. Kama mtu ni mzalendo hata kama hajasoma na anaijua na kuiishi falsafa ya Chama kwa maneno na matendo yake na akaieleza kwa umma akaeleweka vizuri; mimi sioni tatizo hata kama akiwa raisi wetu.

Wanamapinduzi mahiri duniani akiwepo Mao Tse Tung walilikamata tabaka la wanyonge kwanza; haya mengine ya wasomi, matajiri, n.k. yanakuja baadaye. CHADEMA; dakeni hiyo.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Zainabu kaharibu nini tena? Mbona ni Kichwa chetu?

Aliomba mwongozo kwamba aliona kama Msabaha alikuwa kama anasoma wakti anachangia; Ndugai akasema hakuona Msabaha akisoma popote ila alikuwa akichomoa kigongo baada ya kingine! Basi wakashangilia
 
Mh. Mariam Msabaha FOR PRESIDENT OF ZANZIBAR IN 2015.

huyu mama nilimsikia kwa mara ya kwanza kwenye ziara yao ya nyanda za juu kusini ni kichwa cha uhakika na ana ujasiri wa ajabu kama chadema wako makini wangeanza kumuandaa huyu mama kugombea urais wa zanzibar mwaka 2015 kwani kuna uwazi mkubwa sana ulioachwa na CUF. mama huyu akiandaliwa vizuri kwa maana ya kumpa resources za kutosha na kumpiga shule kidogo (crash course ya uchumi, katiba na manifesto) anaweza akafanya maajabu makubwa Zanzibar mwaka 2015 kwani zanzibar sasa kunaitajika damu mpya wazanzibar wamechoka na
siasa za cuf na ccm kwahiyo mpinzani wa kweli atatokana na chadema hakuna mwingine kwani kwa hivi sasa ccm na cuf ni km chama kimoja.
 
Back
Top Bottom