Mbunge: Heri tufe kuliko Muungano kuvunjika

Shein anasema yeye ataulinda Muungano, anautaka Muungano, urekebishwe, na hauvunjiki.

Lakini mimi mwenye maoni tofauti nisubiri Tume nikatoe maoni! .....hahahahahahaaa.... how preposterous is that?

Kashaanza kuwaweka sawa marefa kwa kuwaonyesha Tume ya Katiba msimamo wa mamlaka ya nchi ni upi, keshaanza kupiga tizi kwa kujaribisha hoja zake mbele ya jamii ili kupima upepo, keshaanza kuwaandaa watazamaji kwa kuwaambia hii mechi anashinda, Muungano hauvunjiki, lakini mimi anasema nitulie ndani nisubiri mechi! ...heck no! ... such incorrigibly ridiculous leaders we have!

Warioba amesema wameshaanza kupokea maoni kwa njia mbali mbali zikiwemo social media, kwa hiyo kama ambavyo Tume imemsikia Shein leo kwenye traditional media anatoa maoni yake na mimi pia inawezekana Tume Ya Warioba ipo hapa inatusoma, sasa kwa nini ya Shein yasikilizwe sasa ya kwangu nisubiri Tume?!! ... heck freaking no! Ukisema Muungano hauvunjiki na mi nasema Muungano tunauvunja!
 
Sijawa na uhakika kama kuna mauaji yamefanywa kwa wale wanaotofautiana nao kimawazo.

Ndani ya CCM wanatofautiana Mawazo

Hawauani

Ila sijui Kaka


Au kuna ushahidi?

Na dhambi za ccm za kudiriki kuwatoa roho wale wanaotofautiana nao kimawazo unaziweka kundi gani?
 

hawa viongozi wetu ni mabogas kweli na wanafikiri watu wote ni wapumbavu kama wao na ukishakuwa mtawala ndo ushakuwa mungu, juzi tu makamo wa pili iddi alisema serikali haina maoni ssa leo huyu mkuu wa mchamba wima anatuletea maoni ya smz then watu wasubiri tume hivi hawa magamba sijui kama wanaakili timamu na kwa mtizamo huu na ukiritimba wa hawa magamba sijui kama tutafika 2015 bila hili taifa kuingia mgogoro, duh tena huyu mkuu wa mchamba wima wa mara hii ndo anaboa kinoma.
 
Hapa Dr. Shein atakuwa amewaudhi UAMUSHO kupita kiasi.

Vipi Dr. Shein makanisa yaliyochomwa moto utayafidia kwa kutumia kodi za Wazanzibari?

Bobuk,
Baada ya utekwaji wa Dr Ulimboka, siamini tena kwamba uamsho ndio wachomaji wa makanisa.
 
Kifo cha Marehemu Horace Kolimba kilisikitisha sana; hususan katika Bunge na CCM. Ahadi yake ilifika na alikufa kwa shinikizo la damu; kwa bahati mbaya watu waliweka dhana kuwa ni CCM ndio ilimuua. sio kweli, kwani postmortem ilisema ni hypertension.

Wakatabahu

 

Una matatizo ya akili wewe,CHADEMA inahusikaje hapo?
 
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...udi-kwanza-ndipo-rasimu-ya-katiba-ifuate.html

 
Kauli kama hii inatia shaka juu ya uwezo wa wawakilishi wetu bungeni. Nani kamtuma kusema "heri kufa.." Katika kipindi hiki ambacho nchi zilizoendelea zinaungana, Euro, Falme za Kiarabu, USA, na sasa EAC kuelekea kwenye Political Federation ili kuwa na nguvu ya maamuzi kiuchumi, kisiasa, kijamii, nk, mtu anakurupuka kusema eti 'muungano umewatoa kwenye ramani ya dunia'. Hivi visiwa vya ZNZ vimepelekwa ramani ipi? Ya Jupiter, Mars au Pluto?

Nadhani mheshimiwa anapaswa. pamoja na wanaoshabikia kuvunjwa Muungano kuangalia faida wanazozipata na opportunity cost ya kuvinjwa Muungano, zaidi ya kuongea kauli hewa. Hivi itasaidia nini ZNZ 'kurudi kwenye ramani' huku ikabaki pekee yake kupambana na ubepari unaozikumba nchi zetu na wananchi kuendelea kuishi ktika umaskini?

Ni bora kuvunjwa kwa Muungano ikawa hatua ya mwisho baada ya kuainisha hatua kadhaa zinazopaswa kuchukulia kama hatua zinazochukuliwa na serikali za EA kuelekea kwenye Political Federation.

Wanansiasa msikurupuke na kuonesha ujinga wenu na uwezo mdogo wa kupambanua maswala mazito, mnajishushia heshina na kuonesha wazi kuwa hamjui kilichowapeleka mjengoni.
 
JITU JINGA LAZIMA LIONYESHE UJINGA WAKE TU

ZAMA ZA KARUME, HUYO ALIKUWA ANATANDIKWA bAKORA NA HAPEWI TENA FURSA YA KUTAPIKA UTUMBO KAMA HUO

 
Yeye amewekwa na wananchi na ndio wenye maamuzi sio yeye najua ameapa ataulinda muungano lakini afahamu katiba sio msahafu si kigezo kuwa hakivunjiki iko siku wananchi watachoka kuburuzwa
 

Mohammed Amour Chombo Mbuge(ccm)





na Danson Kaijage, Dodoma


MZIMU wa Muungano umeibuka tena bungeni jana baada ya mbunge wa Micheweni, Haji Khatibu Kai (CUF), kudai kuwa Wazanzibari wako tayari kufa njaa kuliko kuendelea na Muungano aliodai hauna tija.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu, alidai kuwa wananchi wa Zanzibar hawanufaiki na Muungano wakati wanaonufaika ni watu wa upande wa Tanzania Bara.
Mbunge huyo alisema muungano huo umeiondoa Zanzibar katika ramani ya dunia, hivyo ni bora ukavunjwa na kila upande ukaendelea kuwa nchi inayojitegemea.
Hata hivyo, Mbunge wa Magomeni, Muhammad Amour Chomboh (CCM) alitoa taarifa kwa Spika akidai kuwa kinachosemwa na mbunge huyo wa CUF ni mawazo yake.
“Nataka kumpa taarifa mbunge mwenzangu kuwa Wazanzibari ambao ni wazawa na wazalendo wa Zanzibar siyo kweli kuwa wanaukataa Muungano na wala hawako tayari kufa kwa njaa kwa ajili ya kuukataa,” alisema Chomboh.


 
Sasa njaa na muungano vinahusiana nini? Siasa za wabongo bwana cheap kweli. Our politicians can't make serious politics except they will find a way to win cheap popularity through religion, tribalism, sectarianism, etc. Useless politicians!
 
Alikosea sana. Alitakiwa aseme maneno hayo halafu aonyeshe mfano kwa kuwaaga wabunge wenzake na kuondoka Dodoma moja kwa moja arudi zanzibar akafe njaa huko. Na bila shaka wazenji wenzake wangemuunga mkono waondoke wote bungeni. Kinachoendelea kumuweka Dodoma ni nini?!
 
Huyo Chombo ni mpumbavu tuu..! huyo ni sawa na wawakishi wa Dole na Chwaka (ccm) kwa UFUU TUNDU NA kukurupuka.

Kama ni mwanamme aende huko Magomeni akaseme pumba zake, ubunge wenyewe kapewa kwa njia ya wizi wa kura kwa hio wacha ATETEEE muungano.
 

Hapo kwenye blue, yaani niliogopa sana, hapa nina atlas - Mbona Zanzibar naiona kwenye ramani?huyu mbunge vip?
 
Pamoja na talalila zote hizo, lakini tufike mahali tukiri kwamba zanzibar wana haki ya kujiamulia mambo yao wenyewe. Sidhani kama muungano wa tanganyika na zanzibar uliletwa na Mungu hivyo hauwezi kuvunjika. Iwapo USSR ilivunjika sembuse Tz?
 
Hivi mtu akisema hiki kitu sikitaki kwanini usiheshim mawazo yake? Uko wapi uhuru? iko wapi democrasia. Hivi akidai unamburuza utakataa? Au kuburuzwa ni kupi?
 
tatizo la wana visiwa hivi ni roho ya kupenda madaraka makubwa tu wanasingizia kero za muungano na malalamiko lukuki yasiyo na ukweli

Watu wa Tanganyika ndiyo wangelalamika kwani rasmali zetu nyingi zinatumika kuwalea wao mfano suala la umeme pia wapo bungeni wakula posho kupisha bajeti hata za wizara zisizo wahusu kazi kusema ndiyoooooooooooo

ndiyo maana mtu asema hata yale ambayo hakutumwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…