Miaka 58 ya Muungano; Maoni mbalimbali yaliyopata kuzungumzwa juu ya Muungano

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
MIAKA 58 YA MUUNGANO;MAONI MBALIMBALI YALIYOPATA KUZUNGUMZWA JUU YA MUUNGANO.

Leo 12:15pm 26/04/2022

Muungano wetu ni muungano wa pekee na wa aina yake duniani,hakuna Muungano mwingine wowote kama huu Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar kuzaa Tanzania,bado najiuliza jina la Tanganyika lilikufia wapi ilihali jina la Zanzibar bado lipo,kitu kingine,Miuungano mingine yote ni miungano ya mikataba, kwenye kila mkataba lazima kuwepo na kipengele cha kuvunjika kwa mkataba, lakini huu muungano wetu adhimu, sio mkataba, Wanyakyusa wanasema (it's not a contract, it's never a contract) ni muungano wa makubaliano, agreement. Zile Articles of Union sio contract ni agreement, hazina kipengele cha kuvunja muungano, hivyo muungano wetu ni muungano wa maisha,for life!.tulichanganya mchanga na muungano wetu ukawa wa milele!.

Miungano ni kitu kizuri kama itasimamiwa na kuendeshwa kwa faida ya wote,Ubaya wa miungano tunayoifanya sisi Afrika ni wanasiasa tu ndio wanaoamua kila kitu bila ya kuwashirikisha wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa miungano hii,kuna msemo wa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu,Miungano inayosimamiwa na kuendeshwa kwa haki,usawa na mgawano wa tija kwa wanachama wake basi huwa inawavutia wengi kutaka kujiunga na miungano hiyo,EAC si umeona Rwanda na Burundi wamejiunga karibuni tu baada ya kuona kuna faida...Huu wa kwetu sisi jee? Kuna nchi ambayo imeshawahi kutuma maombi ya kutaka kujiunga nasi? Kwa sababu gani?

Hivi karibuni tumesikia maneno mengi kuhusu Muungano,mfano Zanzibar inapendelewa, Watanzania hawaruhusiwi kununua ardhi Zanzibar,Sasa watu wengi hatuujui huu Muungano vizuri,pengine ni mgawanyo ulio sawa,pengine ni kubalance maendeleo,lakini ebu tujiulize maswali,Je kama watanzania tutaambiwa tupige kura juu ya huu muungano wetu nini kitatokea? Nauliza swali hili kwa sababu mijadala ya muungano naisikia zaidi kwa wanasiasa tu, sijui kiundani wananchi wa kawaida wana mtazamo gani. Na kama hiyo kura itapigwa ni wazanzibar ndio watakaouunga mkono muungano au ni Watanganyika? Tuna mtazamo gani juu ya hili?

Inawezekana suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar linaibua hisia kali miongoni mwetu lakini hoja ndizo zitakazofanya mjadala kuwa wa maana,tunaweza kuuchambua ndani nje bila jazba na kuona uzuri wa Muungano,kasoro zake na kero zake pia tunaweza kupendekeza namna ya kuziondoa,Muungano au jumuiya ziko nyingi duniani na ni dalili ya nguvu...kwa hiyo lamsingi sisi kama wananchi ni kusimamia Muungano uwe wa haki na usawa ili ulete manufaa kwa pande zote mbili za Muungano,tuanze na hoja iliyopata kutokea mnamo mwaka 1993,hoja ya Serikali tatu iliyopata kuletwa na Wabunge 55 waliojulikana kwa jina la G55.

-Hoja binafsi ya Mh Njelu Kasaka,Bunge la Bajeti Mwaka 1993.

Katika kikao cha Bunge la Bajeti cha mwaka 1993, aliyekuwa Mbunge wa Chunya, Mheshimiwa Njelu Kasaka aliwasilisha hoja binafsi bungeni ya kudai Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano. Wabunge 55 waliokuja kufahamika kama G55, wakiongozwa na mtoa hoja, Njelu Kasaka, waliiunga mkono hoja hiyo na pia ikapata baraka za Waziri Mkuu wa wakati huo, John Samwel Malecela 'Cigwiyemisi' na kupitishwa na Spika wa Bunge , marehemu Chifu Adam Sapi Mkwawa ili ijadiliwe. Baadaye walikuja kuongezeka na kufikia 65 (G65?)

Hii hapa ni orodha ninayoamini ilikuwa ya G55 ingawa natanguliza samahani kuwa sina hakika na majina mawili matatu na wapo niliowasahau ila kwa msisitizo; Jaji Sinde Joseph Warioba hakuwa moja wao. Kwamba Jaji alikuwa kwenye G55 ni habari ambayo chanzo chake ni CCM katika jitihada za kujaribu kuinusuru CCM kwa kumpaka matope huyo shujaa wa Watanzania,lakini pia natoa nawapongeza kwa dhati G55 kwa hoja yao ya Kizalendo kwa Taifa lao la Tanganyika lililokuwepo kabla ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika,1964, Shukrani kwa mashujaa wafuatao;-


1.John Samwel Malecela, (Mtera, Waziri Mkuu)
2.Horace Kolimba?
3.Njelu Kasaka (Lupa)
4.Mateo Tluway Qaresi (Babati)
5.Jenerali Twaha Khalfani Ulimwengu (Taifa/Jumuiya ya Vijana)
6.Ahmed A. Mpakani (Iringa Magharibi)
7.Paschal K. Mabiti (Mwanza)
8.Luteni Lepilal Ole Moloimet (Monduli)
9.Lumuli Alipipi Kasyupa (Kyela)
10.Profesa Aaron Masawe (Hai)
11.Arcado Ntagazwa (Kibondo).
12.Phineas Nnko (Arumeru Mashariki)
13.Paschal Degera (Kondoa Kusini)
14.Mussa Nkhangaa (Singida Mjini)
15.Halimenshi Kahema Mayonga (Kigoma Kaskazini)
16.Said Abdallah Nakuwa (Lindi Mjini)
17.Mosi Tambwe (Taifa/Wanawake).
18.Luteni Kanali John Mhina (Muheza)
19.Charles Kagonji (Mlalo),
20.Kisyeri Werema Chambiri (Tarime)
21.Tobi Tajiri Mweri (Pangani)
22.William H. Mpiluka (Mufindi)
23.Aidan Livigha (Ruangwa)
24.Philip Sanka Marmo (Mbulu)
25.Erasto K. Lossioki (Simanjiro)
26.Shamim Khan (Morogoro Mjini)
27.Raphael Shempemba (Lushoto)
28.Pachal Degera (Kondoa)
29.Tuntemeke Sanga.[Makete]
30.Mbwete Polile Hombee (Mbeya Vijijini)
31.John Byeitima (Karagwe)
32.Chediel Yohane Mgonja (same)
33.Japhet Sichona (Mbozi),
34.Benedict Losurutia (Kiteto)
35.Dk. Mganga Kipuyo (Arumeru Magharibi)
36.Stanley Kinuno (Nyang'hwale)
37.Dk. Aaron Chiduo (Gairo)
38.Edward Oyombe Ayila (Rorya)
39.Shashu Lugeye (Solwa).
40.John Mwanga (Moshi Mjini)
41.Dk. Deogratius Mwita (Serengeti)
42.Abel Mwanga (Musoma Mjini)
43.Juma Jamaldin Akukweti (Tunduru)
44.Patrick Silvanus Qorro (Karatu)
45.Steven Mwaduma (Iringa Mashariki)
46.Dk. Ndembwela Ngunangwa (Njombe Kusini),
47.Richard Koillah (Ngorongoro),
48.Leipilal Ole Molloimet [Monduli]
49.Phares Kabuye (Biharamulo - alihamia CUF)
50.Evarist Mwanansao (Nkasi)
51.Mussa Masomo (Handeni)
52.Jared Ghachocha (Ngara)
53.Mariam Kamm (Taifa/Wanawake).
54.Kuwayawaya Stephen
Masoud Masoud (Temeke) ?
55.Gerald Gachocha?
56.John Elikana Byeitima?
57.Mrs Tabitha Siwale ?
58.Laipalal Ole Moiloitmet (Lo

Kutoka kwenye hoja ya Mh Njelu Kasaka,1993 hivi leo 2022 miaka 29 iliyopita nami kuna mambo nayaona kama ni kiini macho katika Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar ni kuwepo kwa mambo ya Zanzibar tu,na hatuisikii Tanganyika kutajwa(badala yake inatajwa Tanzania bara. When did Tanganyika change the name to become Tanzania bara?), kuwepo kwa mambo ya Zanzibar tu, hii ipo na kuwepo kwa mambo ya Muungano(Tanzania)hii pia ipo,hebu tupate muda kufikiria haya, kwa nini mwanachama mmoja katika Muungano aamue kupoteza jina lake la asili,kiasi iwe ni dhambi au kama kosa la jinai kulitaja jina lake? Na hapa nakusudia Tanganyika.

Jee kuna faida gani kuwafanya watu wauchukie utaifa wa awali?

Katika muungano wetu kuna pande mbili na kila upande unategemea kutetea maslahi yake ndani ya muungano, jee kukosekana kuonekana kwa uwazi wawakilishi wa upande mmoja kunasaidia vipi kuudhofisha muungano huu?
Kuna kitu gani hapa ambacho viongozi wetu wanakifanya kuwa ni siri kubwa sisi wananchi wa kawaida tusijue,tusielewe?

Mfano huu tunaweza kuusogeza kwenye EAC. Tanzania ni member hapo jee tutanufaika vipi kama hatuna muwakilishi wetu huko? Au tukijifanya kuwa Tanzania hai-exist?

Je umeshajitayarisha kuachana na utanzania pale Comoro na Congo zitakapojiunga nasi kama inavyodokezwa anga za kimataifa? Utaifa wetu mpya utakuwa Utanzanconcomia! Tan-zan-con-com-ia.

Je umeshajitayarisha kuwa mui-east afrika na kuachana na utanzania litakapokuja East African federation?

Nimalizie kwa kusema sababu ya kuwa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sasa tuziangalie upya,tunahitaji tu kuwa na ushirikiano kama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Yeyote anayetaka ridhaaa ya kura za Wazanzibari kwa sasa lazima aongelee "sovereignty ya Zanzibar" as a country.Zanzibar ilikuwa tajiri sana kuliko Oman kabla ya mwaka 1960 na ndiyo sababu Sultan Seyyid Said alihamisha Makao makuu ya Sultanate of Oman kwenda Zanzibar mmamo 1840. Mwaka 1960 kwa mfano Zanzibar ilikuwa na kilometres 22 za barabara ya lami wakati Oman ilikuwa haina. Leo hii Oman ni nchi tajiri sana baada ya kugundua raslimali za mafuta mpaka imekuwa nchi mfadhili,Mimi ni Mtanganyika kwa maana ya Mtanzania bara naamini kuwa muda wa kuendelea kuishikilia Zanzibar umekwisha,tuwaache wapate maendeleo kipitia OIC na waanzishe bandari huru kama ilivyo Singapore na Dubai,pengine Zanzibar imecheleweshwa mno kiuchumi kwa kuwa ndani ya Tanzania.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Back
Top Bottom