Mbunge Ghati Chomete apongeza Ujenzi Bukira Sekondari

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,895
940
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Ghati Zephania Chomete ameendelea na ziara yake katika maeneo mbalimbali ya miradi ya kimakakati mkoani Mara huku akishiriki ziara ya Kamati ya Siasa Wilaya Tarime kuhusu Ukaguzi wa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika maeneo mbalimbali ndani ya Jimbo la Tarime Vijijini, Machi 03, 2023.

WhatsApp Image 2023-03-04 at 08.21.34.jpeg

Aidha, Chomete amechangia fedha kwa ajili ya hafla ndogo ya kuwapongeza Walimu na Wanafunzi waliofanya vizuri kwenye Mitihani yao ya mwisho ya Kidato cha Nne (4)-2022 Shule ya Sekondari Nyanungu iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini wakati wa Ziara ya Kamati ya Siasa ya Wilaya Tarime kuhusu Ukaguzi wa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Machi 03, 2023.

Chomete amepongeza ujenzi wa Bukira Sekondari na kusema kuwa ni mradi mzuri ambao thamani ya majengo inaendana na kiwango cha fedha ambazo Serikali imetoa kwa ajili ya mradi huo.

WhatsApp Image 2023-03-04 at 08.21.34(1).jpeg

Chomete amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za miradi ya Elimu. Pia, amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya, Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Halmashauri (Mhe. Saimon) kwa kusimamia vizuri ujenzi wa miradi.

WhatsApp Image 2023-03-04 at 08.21.31.jpeg

Chomete amewaomba na kuwasisitiza Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Halmashauri kuwa wasisite kuwapa fedha pindi watakapoomba ili kumalizia mradi kwa sababu juhudi za kukamilika kwa mradi ni nzuri na zitazaa matunda kwa sababu kazi imeshafanyika vizuri sana.
 
Back
Top Bottom