Mbunge Esther Malleko Aibana Wizara ya Afya Kuhusu Hospitali ya KCMC

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MHE. ESTHER MALLEKO AIBANA WIZARA YA AFYA KUHUSU HOSPITALI YA KCMC

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Esther Edwin Malleko leo tarehe 12 Juni, 2023 Bungeni jijini Dodoma ameibana Wizara ya Afya kwa Maswali kuhusu ukarabati, huduma na watumishi katika Hospitali ya KCMC

"Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha huduma za hospitali ya KCMC ambayo inatoa huduma za afya kwa Kanda ya Kaskazini" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Serikali imeboresha huduma za hospitali ya KCMC kwa kupeleka fedha za Miradi mbalimbali kulipia mishahara pamoja na ufadhili wa Masomo kwa Wataalam kama ifuatavyo;
1. Serikali inalipa stahiki na mishahara ya watumishi 905 waliopo KCMC ambapo jumla ya Shilingi Milioni 983,612,500 hutumika kila mwezi

2. Katika mwaka wa fedha 2022-2023 Serikali ilipelekea Shilingi Bilioni 1.8 kwaajili ya Dawa na vifaa tiba

3. Katika mwaka wa fedha 2022-2023 Serikali imetoa fedha Shilingi Bilioni 5.9 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya Hospitali na Shilingi Milioni 263.9 kwaajili ya uendeshaji

4. Katika mwaka wa fedha 2022-2023 Serikali imetoa ufadhili wa Masomo ya ubingwa bobezi kwa watumishi 15 Kada ya Afya wa KCMC wanaosoma ndani ya nchi na nje ya nchi" - Mhe. Godwin Mollel, Naibu Waziri Afya

"Je, ni lini Serikali itatekeleza maombi ya kibali cha mabadiliko ya mishahara Katika Hospitali ya KCMC ambacho wameomba tangu mwaka 2011?" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Kun upungufu mkubwa wa Wafanyakazi Katika Hospitali ya KCMC, Je, Serikali imejipanga Vipi kuweza kutatua changamoto hiyo ukizingatia Hospitali ya KCMC ni ya Kanda?" - Mhe. Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"KCMC ni miongoni mwa Hospitali ambazo ziko kwenye mchakato ambao kuna mjadala kati ya Wizara ya Afya, Wizara ya fedha na Wizara ya Utumishi kwaajili ya kupitia kiwango cha mishahara ambacho Mbunge amekitaja" - Mhe. Godwin Mollel, Naibu Waziri Afya

"Kuna watumishi 905 wanaolipiwa na Serikali lakini wao wenyewe wanalipwa kwa mapato ya ndani zaidi ya watumishi 400. KCMC wana watumishi karibia 1300. Tutaenda kuangalia kama kuna upungufu unatokana na nini" - Mhe. Godwin Mollel, Naibu Waziri Afya.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-06-12 at 17.35.56(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-12 at 17.35.56(2).jpeg
    28.5 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-06-12 at 17.35.55.jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-12 at 17.35.55.jpeg
    48.7 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-06-12 at 17.35.56(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-12 at 17.35.56(1).jpeg
    25.2 KB · Views: 6
Ukifika pale hosp ni kama iko vizuri tu kuanzia wafanyakazi mpaka mazingira huwezi jua kuna changamoto
 
Back
Top Bottom