Mbunge CCM atoa nguo ya ndani mkutanoni

Huyo mwanamama lazima atakua ni wale wazoefu wa kazi yao kuvua viwalo vyao vya ndani hovyo ndio maana hajaona soo kuvua mbele ya waheshimiwa..si unajua bana ngingi likikubuhi inakua tena aibu hakuna
 
Mbunge huyo ni Florence Kyendesya na alikusudia kumvalisha hiyo sidiria Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa aitwaye Aden Mwakyonde. Ni kijana mdogo sana kwa kumlinganisha na Mama Kyendesya ni sawa na mjukuu wake.

Kyendesya alikuwa akimlalamikia Mwakyonde kwamba aliingilia kampeni za UWT Mkoa kwa kumpigia kampeni pinzani wake katika nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa wa jumuiya hiyo ambapo yeye alikuwa akitetea kiti hicho.

Alitoa sidiria hiyo kwa lengo la kumvalisha Mwakyonde akiashiria naye ni mwanamke kwa vile kama alivyodai Kyendesya mwenyewe aliingilia mambo ya wanawake kwa kumuunga mkono mpinzani wake anayefahamika kwa jina la Mboma.

Taarifa toka ndani ya duru za CCM mkoania Mbeya zinaeleza kuwa kitendo cha baadhi ya viongozi kumuunga mkono mpinzani wake kilimlazimisha kutumia fedha nyingi mno kuweza kukitetea kiti hicho na baadhi wanadai ni alitumia zaidi ya shilingi milioni 30!

Kwa ufupi ni kitendo cha aibu, lakini hashangazi kwani hata wakati wa ziara ya Lowasa mkoani Mbeya wakati huo akiwa Waziri Mkuu aliwahi kutamka kuwa wanaume wanaowafuatafuata wanafunzi wa kike waache upuuzi huo na badala yake wamtongoze yeye!

Ikimbukwe huyu ni mtu wa karibu sana na Apson!

Huku kwetu huku, bado kidogo tu, kidogo sana, yaani ile kiduchu......
 
Halafu mnashangaa ati kwanini Tanzania haiendelei. hebu fikiria mtu huyo kesho au keshokutwa anaenda kuwakilisha nchi yetu kwenye mikataba au mikutano ya kimataifa.
 
Halafu mnashangaa ati kwanini Tanzania haiendelei. hebu fikiria mtu huyo kesho au keshokutwa anaenda kuwakilisha nchi yetu kwenye mikataba au mikutano ya kimataifa.

Unafikiri kwa nini mikataba yao inasainiwa bedroom hotelini?
 
Sina hakika huyo mama wa chama alikuwa na nia gani hasa. Ila napenda kuchukua fursa hii kutoa angalizo hili: Utamaduni wa wanawake kuvua nguo kama ishara ya kupinga jambo fulani ni utamaduni wa muda mrefu na unaoheshimika sana barani Afrika. Ila hii ni silaha ambayo huwa inatumiwa baada ya silaha nyingine za mapambano kushindwa kufua dafu. Huwa ni ishara ya kutoa laana. Kama mnakumbuka, baadhi ya wastaafu wa Afrika Mashariki waliitumia hii mbinu ya mapambano hivi karibuni wakati wakidai mafao yao.Turejee historia ya mapambano ya wanawake waafrika toka enzi za Me Katilili, Mwami Ntare, Yaa Asantewaa, Lilian Ngoyi na Bibi Titi Mohammed tuone ni jinsi gani kuvua nguo ni silaha kali sana katika harakati za ukombozi.
 
Halafu mnashangaa ati kwanini Tanzania haiendelei. hebu fikiria mtu huyo kesho au keshokutwa anaenda kuwakilisha nchi yetu kwenye mikataba au mikutano ya kimataifa.
Choveki,
Watu kama hawa ndio wanaokuwa mabubu kuanzia mwanzo wa mkutano hadi mwisho.Huko watamsaulia nani??
 
hivi huyo mama alikosa njia ya kumtongoza huyo kijana mpaka akatumia njia hii? na ana matatizo gani mpaka anamtakas huyo kijana? njaa au kiu kikali saana? na kwa nchi za wenzetu angekuwa ameisha jiuzulu.lakini kwa sababu ni tanzania na ni wa ccm, vbasi hakuna katika chama atakaye nyanyua mkono au mdomo, kukilaani kitendo hichi na kumuomba muhusika achukue njia ifaayo kulinda heshima ya chama , nchi na ya kwake mwenyewe. na usalama wa taifa wasiwe wanaajiri watu kama hawa, ndio wanadumaza nchi.
 
Sio kitu nzuri kuonyesha nguo za ndani hadharani,Ila hata hivyo mtoa habari jua kutofautisha sidiria na chupi.ACHANA NA KITU CHUPI!
 
Wakubwa huyu mama ni nani? Jee alikuja na underwear ya aina gani? Inawezekana Taiwan yake alinunua enzi zile za mzee ruksa.
 
Huyo ana dalili zote za ukichaa. Unajua katika hali ya kawaida hasa kwenye mikutano huwezi kuonyesha nguo za ndani zitakazoonekana ni za juu tu.

Ila siwezi kushangaa wale wakaka wa kileo wanovaa "Mlegezo" eti wanaenda na wakati. Wadada nao hatuko mbali sana tunavaa nguo vibana makalio huku vyupi vya kisasa eti THONG viko nje. Huu ni ushamba anayefanya hivyo aache tu hakuna watu wako interested.

Inawezekana huyo mama kama chupi ilionekana alikuwa akidumisha huu mfumo hewa wa kisasa.
 
Caroline, hali halisi yaonyesha kwamba nyakati hizi za leo kuna haja medical files za hawa 'waheshimiwa' ziwekwe wazi. Siku tutakuja 'kumteua' pyschopath! kushika uongozi wa nchi.
 
Back
Top Bottom