Mbunge CCM akamatwa kwa tuhuma za rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge CCM akamatwa kwa tuhuma za rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 27, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]ALHAMISI, SEPTEMBA 27, 2012 07:25 NA MAREGESI PAUL, ALIYEKUWA KISARAWE

  TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, imemtia mbaroni Mbunge wa Viti Maalum, Zainab Vullu (CCM) kwa tuhuma za rushwa.

  Vullu alikamatwa juzi pamoja na wenzake wawili ambao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT), Wilaya ya Kisarawe ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Asia Madima pamoja na Katibu wa UWT wa wilaya hiyo, Mwajuma Mombwe.

  Chanzo chetu cha habari kilichopo wilayani Kisarawe kilisema jana, kuwa Vullu na wenzake hao, walikamatwa juzi saa 12 jioni baada ya kudaiwa kugawa fedha kwa wajumbe waliohudhuria kikao cha Baraza la UWT, Wilaya ya Kisarawe kilichokuwa kikifanyika makao makuu ya CCM, Wilaya ya Kisarawe.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, Vullu, Asia na Mwajuma, walikamatwa na Kamanda wa TAKUKURU, Wilaya ya Kisarawe, aliyetajwa kwa jina moja la Noel.

  “Kabla hawajakamatwa, tuliingia katika kikao cha Baraza la UWT la Wilaya ambako tulichagua wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji.

  “Tulipomaliza kuchaguana, akaja Mama Vullu (Zainab Vullu), akapewa nafasi ya kuzungumza, akatwambia kwamba, Oktoba 3 mwaka huu, baadhi yetu tukalale nyumbani kwake na wengine tukalale katika ofisi za chama chetu hapa Kisarawe kwa ajili ya kufika mapema kwenye uchaguzi wa jumuiya yetu utakaofanyika Oktoba 4 katika Ukumbi wa Filbert Bayi.

  “Yeye Mama Vullu ndiye Mwenyekiti wa UWT, Mkoa wa Pwani na anatetea nafasi yake, kwa hiyo, alitwambia atakayeshindwa kufuata maelezo yake, ajue hatapata kitu.

  “Alipomaliza kuzungumza hayo, yule Asia Madima, akaanza kutugawia Sh 10,000 kila mmoja kwa wajumbe wote 44 tuliokuwa katika ukumbi huo. Wakati fedha zikiendelea kugawiwa, yule Kamanda wa TAKUKURU wa Wilaya anaitwa Noel, akaingia ukumbini akiwa na mwenzake mmoja.

  “Walipofika, wakamkamata Asia akiwa na burungutu la noti ambalo alikuwa akiendelea kuligawa kwa wajumbe, akakamatwa pia Mama Vullu na Mwajuma na kupelekwa katika ofisi za TAKUKURU pale chini.

  “Kwa ujumla, viongozi wetu walipokamatwa, ilikuwa ni mshike mshike maana watu walijaa hapa ofisini kisha kule TAKUKURU kwa sababu walitaka kujua hatima ya viongozi hao,” kilisema chanzo chetu hicho.

  Kamanda Noel alipopigiwa simu na MTANZANIA ili kuzungumzia tukio hilo, alipokea simu, lakini mwandishi wetu alipojitambulisha, alikata simu na alipopigiwa tena simu yake ilikuwa ikiita bila majibu.

  Kamanda wa TAKUKURU, Mkoa wa Pwani, Joyce Shirima, alipozungumza na MTANZANIA kwa simu juu ya tukio hilo, hakukubali wala kukataa ila akasema anasubiri taarifa kamili kutoka wilayani Kisarawe. Pia aliahidi kumpigia simu mwandishi wetu baada ya muda lakini hakufanya hivyo.

  Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Fatuma Kimario, alipozungumza na MTANZANIA kwa simu, alipokea simu lakini mwandishi wetu alipojitambulisha, alisema yuko kwenye kikao hawezi kusema chochote. Hata hivyo, alipopigiwa tena, simu yake haikupatikana.

  Wakati hayo yakiendelea, Vullu na Asia walizungumza na waandishi wa habari na kukiri kwamba walikamatwa na TAKUKURU ingawa hawakujua ni kwa nini walikamatwa.

  Katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa CCM, Wilaya ya Kisarawe, Mbunge Vullu alisema, “Ni kweli TAKUKURU walitukamata mimi na huyu mwenzagu Asia pamoja na Mwajuma.

  “Mnajua katika vikao kuna posho zinazotolewa kihalali na ndiyo maana waliokuwa wakipokea hizo Sh 10,000 tulizokuwa tukiwapa, walikuwa wakisaini, jamani haikuwa rushwa hata kidogo, hizo siyo rushwa kwa sababu rushwa mtu hasaini.

  “Pia mimi (Vullu) sikukamatwa na fedha zozote, aliyekuwa akigawa fedha ni huyu Asia, yeye ndiye anayejua alizitoa wapi, lakini bado nasema tulikuwa hatutoi rushwa na kwa kuzingatia hilo, hata tulipopelekwa pale ofisi za TAKUKURU tulikataa kujaza fomu alizotupatia yule Noel kwa sababu hatukuwa na kosa.

  “Pamoja na hayo, naomba mkamuulize huyo Noel ni kwa nini alikuja kutukamata na ‘gate keeper’ (mlinzi wa getini) anaitwa Kingu, hivi huyo Kingu ni nani hapo, mkamuulize,” alisema Vullu.

  Kwa upande wake, Asia alisema wakati anakamatwa alikuwa na burungutu la noti zenye thamani ya Sh 550,000 kwa kuwa baadhi ya wajumbe alikuwa ameshawasainisha kiasi fulani cha fedha.

  “Kikao kilikuwa na wajumbe 49 na mhudumu mmoja, kwa hiyo hao TAKUKURU walipofika hapa, walitukamata na wakachukua fedha zangu ambazo baadaye nitazifuatilia ili wanirudishie maana hizo hazikuwa rushwa bali ni posho za kawaida ambazo nimezipata kwa njia halali.

  Kwa mujibu wa Asia, maofisa hao wa TAKUKURU mbali na kuchukua fedha hizo, walichukua pia Katiba ya UWT, walichukua nyaraka za vikao, orodha ya wajumbe waliokuwa wakitakiwa kusaini posho na kitabu cha Kanuni.

  Juzi, Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akifungua kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Mjini Dodoma, alikemea vitendo vya rushwa ndani ya chama hicho na kuwataka wana CCM wasijihusishe na rushwa kwa kuwa rushwa inakichafua chama.  [h=4][/h]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ina Maana watakwenda JELA au ni bunja akili...?
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ngoja tusikie watamfikisha wapi!

  Hiyo ndiyo ccm,ccm,ccm,ccm

  Utasikia haikuwa hivyo!
   
 4. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  CCM wote ni wala rushwa, sasa kwanini TAKUKURU wamebagua na kumkamata huyu dagaa?

  Ooh NO! nimekumbuka ni usanii tu, ili waonekane wako kazini! Hakuna kitu hapo
   
 5. A

  August JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  mimi ninavyo jua alikuwa amewakopesha hizo hela, hivyo alikuwa anawarudishia, na wengine ndio walikuwa wana mkopa
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Takrima hizo! Asante kwa taarifa, sote tunajua ndani ya ccm rushwa siyo dhambi, bali ni kanuni ya kuwapitisha wagombea
   
 7. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  it might be mixed opinion mkuu.
  Inawezekana huko mbele ya safari tukaja kukubali kuwa PhD ya Edward Hosea ni halali kwa kujitahidi kufanya kazi kadri ya anavyoweza kutokana na uwezo na rasilimali zilizopo lakini anakwamishwa na upande wa pili.
  Hili ni suala la historia na ngoja tuone tu, huko mbele ya safari watajua ukweli. ....uliwahi kuona hata mtu mmoja anasimama hadharani kutetea 'AZIMIO LA ZANZIBAR'? Historia itatueleza tu

   
 8. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  SSM imekosa maadili sana, ni chama kipi kianze kufutwa? SSM au CDM? Tendwa unasemaje babu? Kapumzike umri umeenda na katiba mpya ni lazima msajili wa vyama vya Siasa apatikane kwa open search itakayosimamia na neutral bodies na si kwa kuteuliwa na Rais aliye madarakani?
   
 9. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Simply and unianimously CCM and Kikwete are run out of tricks. They spectacularly fail on very first step of each new trick! Deary me!!!!

  How the might has fallen!
   
 10. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,777
  Trophy Points: 280
  Uyu mbunge wa vitanda maalum amezoea mteremko sana.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 11. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Tuko ukurasa mmoja mkuu, lakini si unajua historia inatengezezwa?
  So muda huu tunaijenga/tunaitengeneza ili huyo hakimu MUDA akija, ahukumu kwa haki kama kawaida yake
   
 12. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,507
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  akili mukichwa
   
 13. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mswahili Haachi Asili..Amezaliwa kwenye rushwa! Amelelewa Kwenye Rushwa! Amefaulu kwa rushwa! Amepata cheo kwa rushwa! Rushwa na yeye! Yeye na rushwa! Pete na kidole!

  GARBAGE IN..GARBAGE OUT!!!!!
   
 14. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,655
  Likes Received: 3,307
  Trophy Points: 280
  Wale wagawa rushwa wa uchaguzi mkuu wangeshughulikiwa kwanza ndiyo waendelee kutupigisha stori vinginevyo siwaamini hawa tukukuru kabisa.
   
 15. a

  afwe JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Mh! Makongoro Mahanga alikamatwa na box la kura bandia na hakuna kesi mpaka leo sembuse na hawa?
   
 16. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145

  yaani mpishi akionja chumvi ni mbaya?mbona hayo ni ya kawaida kwa ccm labda tu hao takukuru anataka asikike
   
 17. Fekifeki

  Fekifeki JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,163
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Huu ni msitu wa magamba ambao unahitaji kuchomwa na kupanda miti ya aina zingine! Napendekeza uwe unaitwa MSITU WA MAGWANDA.
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Huwezi kutenganisha CCM, wanaCCM na vitendo vya rushwa. Shida ni kuwa takukuru hawana ubavu wa kuisimamia hii kesi so itaisha tu!!!
   
 19. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  MBUNGE wa Viti Maalum, Zainab Vullu (CCM), Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), Wilaya ya Kisarawe, Asia Madima na Katibu wa UWT wa wilaya hiyo, Mwajuma Mombwe, wako hatarini kung’olewa katika nafasi wanazogombea.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, aliiambia MTANZANIA kwa simu jana, kwamba baada ya vyombo vya habari kuripoti jana, kwamba Vullu na wenzake hao walikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Wilaya ya Kisarawe, Kamati ya Maadili ya CCM itakwenda Kisarawe kuchunguza tuhuma hizo.

  source: Mtanzania
   
 20. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  IJUMAA, SEPTEMBA 28, 2012 08:16 NA ARODIA PETER


  [​IMG]
  Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Zainab Vullu

  *Ni anayedaiwa kukamatwa kwa rushwa Kisarawe
  *Nape asema atachunguzwa na Kamati ya Maadili


  MBUNGE wa Viti Maalum, Zainab Vullu (CCM), Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), Wilaya ya Kisarawe, Asia Madima na Katibu wa UWT wa wilaya hiyo, Mwajuma Mombwe, wako hatarini kung’olewa katika nafasi wanazogombea.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, aliiambia MTANZANIA kwa simu jana, kwamba baada ya vyombo vya habari kuripoti jana, kwamba Vullu na wenzake hao walikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Wilaya ya Kisarawe, Kamati ya Maadili ya CCM itakwenda Kisarawe kuchunguza tuhuma hizo.

  Kwa mujibu wa Nape, kama kamati hiyo ikithibitisha kwamba Vullu, Asia na Mwajuma walikamatwa wakigawa rushwa, wataondolewa mara moja kwenye mchakato wa kugombea nafasi mbalimbali za chama hicho.

  Vullu ndiye Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani na anatetea nafasi yake.

  “Mgombea yeyote atakayebainika kukiuka maadili kwa kutoa rushwa katika chaguzi mbalimbali zinazoendelea ndani ya chama, ataondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi.

  “Nasema hivyo kwa sababu majina ya wanachama yaliyopitishwa katika vikao vya chama hayamaanishi kwamba wagombea wamehakikishiwa ushindi wa kufanya watakavyo.

  “Chama hakitasita kumwondoa mwanachama yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati huu wa mchakato ndani ya chama.

  “Sasa nasema hivi, Kamati ya Maadili itakwenda huko Kisarawe kuchunguza tuhuma hizo na kama ikibainika wanachama hao wamejihusisha na vitendo vya rushwa, wataondolewa mara moja kwenye mchakato wa uchaguzi.

  “Ni juzi tu Halmashauri Kuu imeonya wote wanaodhani kwamba kupitishwa kwa majina yao katika vikao vya Halmashauri Kuu ni tiketi ya kufanya watakavyo, wanajidanganya.

  “Kupitishwa majina yao ni jambo moja na kushiriki mchakato wa uchaguzi ni suala jingine, hivyo wakibainika kukiuka maadili, nasema wataondolewa mara moja kwenye mchakato,” alisema Nape kwa kifupi.

  Juzi TAKUKURU, Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, iliwatia mbaroni Mbunge wa Viti Maalum, Zainab Vullu (CCM), Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT), Wilaya ya Kisarawe ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Asia Madima, pamoja na Katibu wa UWT wa wilaya hiyo, Mwajuma Mombwe, kwa tuhuma za rushwa.

  Chanzo chetu cha habari kilichopo wilayani Kisarawe kilisema kuwa, Vullu na wenzake hao, walikamatwa Jumanne wiki hii, saa 12 jioni, baada ya kudaiwa kugawa fedha kwa wajumbe waliohudhuria kikao cha Baraza la UWT, Wilaya ya Kisarawe, kilichokuwa kikifanyika makao makuu ya CCM, Wilaya ya Kisarawe.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, Vullu, Asia na Mwajuma, walikamatwa na Kamanda wa TAKUKURU, Wilaya ya Kisarawe, aliyetajwa kwa jina moja la Noel.

  Kamanda Noel alipopigiwa simu juzi na MTANZANIA ili kuzungumzia tukio hilo, alipokea simu, lakini mwandishi wetu alipojitambulisha, alikata simu na alipopigiwa tena simu yake ilikuwa ikiita bila majibu.

  Kamanda wa TAKUKURU, Mkoa wa Pwani, Joyce Shirima, alipozungumza na MTANZANIA kwa simu juu ya tukio hilo, hakukubali wala kukataa, ila akasema anasubiri taarifa kamili kutoka wilayani Kisarawe. Pia aliahidi kumpigia simu mwandishi wetu baada ya muda lakini hakufanya hivyo.

  Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Fatuma Kimario, alipozungumza na MTANZANIA kwa simu, alipokea simu lakini mwandishi wetu alipojitambulisha, alisema yuko kwenye kikao hawezi kusema chochote. Hata hivyo, alipopigiwa tena, simu yake haikupatikana.

  Wakati hayo yakiendelea, Vullu na Asia walizungumza na waandishi wa habari na kukiri kwamba walikamatwa na TAKUKURU ingawa hawakujua ni kwa nini walikamatwa.

  Katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa CCM, Wilaya ya Kisarawe, Mbunge Vullu alisema, “Ni kweli TAKUKURU walitukamata mimi na huyu mwenzagu Asia pamoja na Mwajuma.

  “Mnajua katika vikao kuna posho zinazotolewa kihalali na ndiyo maana waliokuwa wakipokea hizo Sh 10,000 tulizokuwa tukiwapa, walikuwa wakisaini, jamani haikuwa rushwa hata kidogo, hizo siyo rushwa kwa sababu rushwa mtu hasaini.

  “Pia mimi (Vullu) sikukamatwa na fedha zozote, aliyekuwa akigawa fedha ni huyu Asia, yeye ndiye anayejua alizitoa wapi, lakini bado nasema tulikuwa hatutoi rushwa na kwa kuzingatia hilo, hata tulipopelekwa pale ofisi za TAKUKURU tulikataa kujaza fomu alizotupatia yule Noel kwa sababu hatukuwa na kosa.

  “Pamoja na hayo, naomba mkamuulize huyo Noel ni kwa nini alikuja kutukamata na ‘gate keeper’ (mlinzi wa getini) anaitwa Kingu, hivi huyo Kingu ni nani hapo, mkamuulize,” alisema Vullu.

  Kwa upande wake, Asia alisema wakati anakamatwa alikuwa na burungutu la noti zenye thamani ya Sh 550,000, kwa kuwa baadhi ya wajumbe alikuwa ameshawasainisha kiasi fulani cha fedha.

  “Kikao kilikuwa na wajumbe 49 na mhudumu mmoja, kwa hiyo hao TAKUKURU walipofika hapa, walitukamata na wakachukua fedha zangu ambazo baadaye nitazifuatilia ili wanirudishie maana hizo hazikuwa rushwa bali ni posho za kawaida ambazo nimezipata kwa njia halali.

  Kwa mujibu wa Asia, maofisa hao wa TAKUKURU mbali na kuchukua fedha hizo, walichukua pia Katiba ya UWT, walichukua nyaraka za vikao, orodha ya wajumbe waliokuwa wakitakiwa kusaini posho na kitabu cha Kanuni.

  Juzi, Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akifungua kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Mjini Dodoma, alikemea vitendo vya rushwa ndani ya chama hicho na kuwataka wana CCM wasijihusishe na rushwa kwa kuwa rushwa inakichafua chama.

   
Loading...